Waziri mkuu mgeni rasmi upokeaji saruji kwa njia ya reli -Moshi




Safari za treni ya mizigo kwenda mikoa ya kaskazini zilizokuwa zimesimama kwa zaidi ya miaka 13, zitaanza tena Jumamosi hii ya Julai 20, 2019 ambapo Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ataipokea treni hiyo mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro
ADVERTISEMENT

Moshi. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua treni ya mizigo Jumamosi ya Julai 20, 2019 Mkoani Kilimanjaro.
Treni hiyo itapokelewa Mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa na mabehewa 20 iliyobeba mifuko 20 ya saruji.
Kwa zaidi ya miaka 13 safari za treni hizo zilisimama kufanya kazi katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kutokana na sababu mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 15, 2019 amesema Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Hata hivyo Mwananchi limepita katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kushuhudia usafi ukifanyika katika barabara za reli  huku baadhi ya wananchi wakishangaa kuona kichwa cha treni kikipita maeneo mbalimbali.
Jana usiku kichwa cha treni kilipoonekana kikipita katika baadhi ya maeneo Mjini Moshi wananchi mkoani humo walianza kushangilia kwa furaha huku wengine wakipiga kelele za furaha.
PIA SOMA

No comments: