ZIJUE SABABU ZA VIJANA WENGI WA AFRICA KUWA
WATEGEMEZI
Makala na;
Godson eric
Hii ni dhana ambayo haipingiki kwa
asilimia 100% kuwa vijana wengi wa Africa ni tegemezi kutoka kwa wazazi
wao.jambo ambalo halipingiki kuwa tangia kijana anapotoka kwenye tumbo la mama
yake huzaliwa akiwa na dhana ya kusikiliza maagizo pamoja na maelekezo ambayo
yanatoka kwa wazazi wao.ni kwel kijan lazima atii na kusikiliza maagizo ambayo
yanatoka kwa wazazi wao.
Kutii
wazazi sio tatizo kwan wao ndio wanakupa njia iliyo sahihi kuifuata ila vijana
wao wenyewe ni waoga kuongea na kuelezea mawazo yao yaweze kuleta tija kwenye
jamii inayowazunguka.nakuletea sababu hii ili uweze kuzijia na kuzichukulia
hatua kama wewe kijana unataka mabadiliko katika maisha yako na katika jamii
inayomzunguka kijana
Sababu
hizi hapa za vijana wengi kuwa tegemezi
WAOGA;Amini
usiamini kuwa kwa asilimia 89% ya vijana wengi ni waoga kusimama na kutetea
hoja zao lakini pia kutoa mawazo ambayo yangeweza kuwa na matokeo chanya kwenye
jamii inayomzunguka.ukipita mashule na mavyuo jambo hili halipingiki kwani hata
kwenye sehemu ya majadiliano baina yawao wenyewe pia kuna wengine hawawezi
kuongea hata baina ya wao wenyewe wanaonea aibu kuongea.kwa asilimia kubwa
wasichana ndio waoga a=zana kuongea kwenye mjumuiko wa watu wengi hasa sehemu
za majadiliano na sehemu ambazo wao wangepaswa kuwa mstali wa mbele kuelezea
adha wanayoipata kwenye matatizo kam vile matatatizo ya maji katika makazi
yao,adha wanayoipata kutokana na kushawishiwa
kujihusisha na maswala ya mahusiano.
Vijana wa kiafrika wengi wao wana ni wazuri
sana wa kuongea pembeni na kujisifu kuwa wao ni waongeaji wazuri.kijna
wakiafrika ni mwepesi kuongea kwenye watu ambao amewazoea.kama kijna ukitaka
uwe na kijana mwenye mabadiliko basi kuwa
jasiri kusimama na kuelezea
mawazo uliyonayo.
HAWAJIAMINI: Jambo
linguine ni kuwa vijana wa kiafrika hajiamini kwa mambo ambao wanayafanya
huwezi ni pinga kwa hili kwani ni
jambo ambalo linaonekana kwenye macho ya
watu wengi ndani na nje ya ardhi hii
ambayo vijana wengi bado ni wasikilizaji
wa vitu ila wao sio waanzishaji wa mada ambazo zingeweza kuwa na manufaa kwenye
maisha yao wenyewe.kwenye muktadha wa kutojiamini ni kuwa ukiangalia kiundani
ni kuwa vijana wengi wa kuafrika wanavipaji ambavyo wamezaliwa navyo
ukilinganisha na vijana wanaoishi nje ya bara hili la afrika.vijana wan je
wengi wao ujuzi wao wamepandikizwa nikimaanisha wao wanafundisha ujuzi Fulani I
basi kubla kwa Africa kijana wa kiafrika kipaji alichonacho amezaliwa nacho.
Tunaweza kuwa vijana wenye mafanikio kwa
kutoa dhana ya kutokujiamini na kujenga
dhana ya kujiamini katika kutaka kufanya kazi .
WEPESI KUSHAWISHIWA:
Nani atanipinga kwa hili hasa hapa kwetu Tanzania kwani vijana wengi ni wepesi
kushawishiwa kufanya jambo ambalo linaweza kuleta maafa kwao wenyewe.kijna hasa
wa kitanzania ni mwepesi kutoa uhai wake kwa mtu ambaye anaweza kuwa asiye na
faida kwenye maisha yake
mwenyewe.urahisi huo wa kuweza kushawishiwa unatokana na haili ambayo inawazunguka.ninakiri
kuwa vijana wenyewe umri kuanzia miaka 17-30 ni wepesi kushawishiwa na kufanya
jambo ambalo liko tofauti na upeo wao wa kuyadajili mambo kiundani na kujua
kuwa jambo ambalo wanalifanya lina mantiki gani kwenye jamii yao.
Kwenye
uwanja wa siasa kijana hutumiwa kama dhana ya ushawishi kwenye mazingira
yanawazunguka.kwenye mavyuo ,vijana hutumiwa sana katika kuleta ushawishi
kwenye siasa ambapo sasa kwa kuangalia baadhi a migomo ambayo imetokea kwenye
mavyuo asilimia kubwa vijana hupoteza maisha lakini pia hupoteza viungo vyao kwa
watu ambao wamekaa kwenye majamvi wakisubirri nini kitatokea baada ya migomo.
USIKUBALI KUSHAWISHIWA KAMA UNAIMANI KUWA UNAA MALENGO MBELENI
SIO WAGUNDUZI WA MAMBO: Wengi
wa vijana wa kiafrika sio wagunduzi wa mambo ambayo yanaweza kuwa na faida
kubwa kwenye maisha yao.kusema sio wagunduzi wa mambo ni neon lenye taswira ya
kuwaelezea vijana ambao wao huwa ni watu wa kuiga mambo amabyo nanaletwa kama
utamaduni wa mambo ya nje hasa uvaaji wa mavazi Ambayo sio tamaduni kwa mtoto
wa kiafrika ambaye anajua ni mavazi gani ambayo anatakiwa kuvaa hasa anapokuwa
kwenye mjumuiko wa watu wengi.ili tuwe kijana mwenye uwezo basi kubali kuwa kijan mgunduzi uweze
kufanikiwa.
No comments:
Post a Comment