Simba 2 vs 1 Mbao FC - Penati Tata Yaipandisha Ndege Simba

Timu ya Simba Sports Club imetwaa kombe la Shirikisho Tanzania Bara kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya timu changa iliyojizolea umaarufu sana kutoka Mwanza ya Mbao FC. Magoli ya Simba yalifungwa na Fredrick Braghon na Kichuya ndani ya dakika thelathini za nyongeza. Simba imekata tiketi ya kushiriki michuano ya shirikisho barani Afrika.

No comments: