POUL MAKONDA AELEZA DHAMIRA YAKE YA KUINUA VIWANDA VIDOGO MKOANI DAR-ES-SALAAM

Ili kwenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa viwanda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda ameeleza jitihada wanazozifanya ili kufikia malengo hayo.


Akiongea na waandishi wa habari mapema leo mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa serikali ya mkoa wa Dar es salaam inafahamu kuwa kuna viwanda zaidi ya 2000 na katika viwanda hivyo kuna makundi 3 ambayo ni viwanda vikubwa, vya kati na viwanda vidogo.

Lakini wao wameamua kuwekeza katika viwanda vidogo ili viweze kuongezeka kufikia kuwa viwanda vya kati na hatimaye kuwa viwanda vikubwa, na ufanikishaji wa hili utaanza hivi karibuni kutokana kwamba wameshaongea na NSSF kuweza kuwekeza katika viwanda hivi.

Na pia Mh Makonda alisema kuwa kila halmashauri imetakiwa kutenga asilimia 10 kwa ajiri ya wazee, wakina mama na vijana, na kwa mkoa wa Dar es salaam ambao una halmashauri 5 hivyo kuna takribani bilioni sita zimetengwa kwa ajiri ya wajasiliamali wadogo na wao wanachotakiwa kukifanya ni kuleta michanganuo ya biashara zao katika ofisi ya mkuu wa mkoa na kupata fedha hizo zenye riba nafuu.

Aidha mkuu wa mkoa huyo aliongeza kwa kusema wajasiriamali wadogo watapata nafasi ya kuuza bidhaa zao katika maonyesho ya biashara yatakayokuwa yakifanyika kwa mwezi mara moja katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam na zitauzwa bidhaa za ndani peke yake na hakutakuwa na bidhaa toka nje.


Lakini pia wamachinga watatakiwa kuuza bidhaa zinazozalishwa hapa kwetu ambazo zinatoka katika viwanda vyetu kwani hii itasaidia kukuza soko la ndani na kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wa hapa nchini kwetu

No comments: