ijue biashara ya kwanza aliyokuwa anafanya nick wa pili
>Biashara aliyokuwa anafanya Nikki Wa Pili kabla yakuwa msanii
Biashara aliyokuwa anafanya Nikki Wa Pili kabla yakuwa msanii
Msanii Hip hop kutoka Kampuni ya Weusi Nickson Simon maarufu kwa jina la Nikki Wa Pili aeleza ukweli wa baadhi ya mashairi ambayo yanapatikana kwenye wimbo wake mpya wa Kihasana wimbo ambao umetoka hivi karibuni akiwa amemshirikisha msanii Chin Bees kutoka Wanene Entertainment.
Nikki amesema kuwa Mashairi ambayo yanapatikana kwenye wimbo wake mpya na iliyopo katika wimbo wake huo yana uhusiano na maisha yake ambayo ameyapitia wakati ambao alikuwa bado yupo Arusha na wala hajaanza kujihusisha na muziki .
”Wimbo wangu mpya wa Kihasara ambao nimefanya na Chin Bees mashairi yaliyomo mule yana uhusiano mkubwa na maisha yangu ambayo nimeyapitia hasa suala la mimi kufanya biashara ya kuuza sambusa kwenye Bar, Sehemu wanazo uza pombe za kienyeji pamoja na maeneo mbali mbali mpaka usiku wa saa tatu ni kweli kabisa nimepitia maisha hayo” amesena Nikki Wa Pili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment