Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar ni majina matatu yaliyotajwa katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA kwa upande wa wanaume.
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo aliisadia klabu yake kushinda kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili mfurulizo huku akiibuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kupachika mabao 12.
Kwa upande wa Lionel Messi na Neymar waliisadia Barcelona kushinda kombe la Copa de Rey huku wakishindwa kuchukua kombe la ligi kuu ya Hispania La Liga.