Chadema: Tundu Lissu Apumulia Mipira, Lakini Jasiri, Tuendelee Kumuombea

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezungumzia maendeleo ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyejeruhiwa vibaya hivi karibuni baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema, amesema hali ya Lissu imekuwa ikibadilika mara kwa mara na inaonesha alipigwa zaidi ya risasi tano za kivita kwenye mwili wake, zilizomjeruhi vibaya sana. Viongozi hao wa Kamati Kuu ya Chadema wamesema mbele ya mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi yao iliyoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwamba hawana imani na jeshi la polisi na serikali katika kuwatafuta na kuwabaini waliokula njama za kumshambulia mbunge huyo

No comments: