Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewasili nchini China kwaajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duaniani. 
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kitendawili’, aliondoka nchini Tanzania siku ya Jumatatu akiwa ameambatana na kikundi chache cha ngoma kikiwa na jumla ya watu sita pamoja na yeye mwenyewe.
Akiongea na mwandishi wetu akiwa nchini humo baada ya kuwasili katika eneo ambalo litafanyika tamasha hilo, Mpoto amesema Alhamisi hii wataanza kufanya maonyesha hayo katika tamasho hilo ambalo linayakutanisha mataifa mbalimbali duniani.