Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka na kudai atakwenda kumuona Mkurugenzi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini Tanzania (Takukuru), Valentino Mlowola ili aweze kumpa ushahidi wa biashara haramu.
Mhe. Godbless Lema amesema hayo leo kupitia ukurasa wake twitter baada ya kupita siku moja tokea Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole kutoa kauli yake iliyokuwa inawataka viongozi wa upinzani kama kweli wanaushahidi wa madiwani saba kununuliwa ili wahamie CCM basi waweke wazi nasiyo kusema sema katika mitandao ya kijamii.
Tutakwenda kumuona Mkurugenzi wa Takukuru na kumpa ushahidi wa biashara mpya haramu ya madiwani”, amesema Lema.