Showing posts with label udaku. Show all posts
Showing posts with label udaku. Show all posts

DAKTARI ABAINI KANUMBA ALIKUWA NA UVIMBE KICHWANI

Daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa ya binadamu na vifo vyenye kutia shaka, Innocent Mosha kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ameieleza Mahakama Kuu alichobaini baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wa msanii wa fani ya uigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba.

Dk Mosha ambaye ni shahidi wa nne wa upande wa mashtaka katika kesi ya kuua bila ya kukusudia inayomkabili msanii wa fani hiyo, Elizabeth Michael maarufu Lulu amesema walipofungua fuvu walibaini ubongo wa Kanumba ulikuwa umevimba.

Lulu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Katika ushahidi wake leo Jumatatu Oktoba 23,2017, Dk Mosha akiongozwa na Wakili wa Serikali, Faraja George mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Samu Rumanyika ameeleza akiwa kazini alipewa maagizo kuwa anatakiwa kuufanyia uchunguzi mwili uliokuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili.

Shahidi huyo amesema katika uchunguzi wa mwili wa Kanumba alibaini kuwepo uvimbe sehemu ya nyuma kwenye ubongo na walipofungua fuvu walibaini ubongo ulikuwa umevimba.

Dk Mosha alipoulizwa na wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala juu ya sampuli walizopeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu hali ya kilevi katika mwili wa Kanumba, amesema hakuwahi kufahamu matokeo ya uchunguzi.

Pia, amesema hafahamu kama Kanumba alijigonga ukutani kwa kuwa hakuwepo eneo la tukio.

OFFICE ZA BAKWATA ZAHAMIA KWA MUDA JENGO LA TIGER TOWER MTAA WA TOGO

www.kwanguleo.blogspot.com

Ndugu zangu Wanahabari,

Assalaamu Alaykum (Amani ya Mwenye ezi Mungu iwe kwenu)

Napenda kuufahamisha umma wa kiislamu kuwa kufuatia kuanza mradi wa ujenzi wa msikiti wa Mohammed VI unaojengwa katika eneo la Bakwata makao Makuu Kinondoni Road.

Hivyo basi napenda kuchukua nafasi hii kuufahamisha umma kuwa ili kupisha mradi huo Bakwata Makao Makuu imehamisha ofisi zake na kuzipeleka katika mtaa wa Togo jengo linalotambulika kama TIGER TOWER na shughuli zote zinaendelea kama kawaida.

Mwisho kabisa tunaomba radhi kwa usmbufu wowote uliojitokeza katika kipindi hiki cha ujenzi.

Wabillahi TTaufiiq

USTAADH TABU KAWAMBWA

MKURUGENZI HABARI NA MAHUSIANO.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25,2016. PICHA NA MAKTABA

IDRIS SULTAN BATA LAKARIBIA BAADA YA KUALIKWA KUIGIZA KWENYE FILAMU YENYE BAJETI YA BILLION 38

  •   Itashutiwa katika miji ya Berlin, London, Paris, Cape Town na Acapulco, Mexico

Mastaa wakubwa duniani kama Eric Dane wa Lastship ,Gerard Depardieu wa Life of Pie,  Thomas Kretschmann wa Avengers Pearl Thusi  wa  Quantico…kushiriki

NYOTA ya aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Mtanzania Idris Sultan, inaendelea kung’ara  baada ya ‘kupata shavu’ la kushiriki filamu yenye bajeti ya dola za Kimarekani milioni 17 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 38.

Idris pamoja na Mtanzania mwingine Ernest Napoleon, wataungana na mastaa wakubwa  duniani kama Eric Dame, mwigizaji Mmarekani, Gerard Depardieu wa Ufaransa, Thomas Kretschmann wa Ujerumani na wengine wengi kucheza filamu hiyo ya ujambazi wa kimataifa.

Filamu hiyo itakayojulikana kwa jina la ‘The Blue Mauritius’, inahusu majambazi watano wa kimataifa ambao wanasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika ya Kusini, kwa ajili ya kuiba vitu mbali mbali vyenye thamani kubwa duniani.

Idris na mwenzake Ernest Napoleon, watasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika kusini mapema mwakani kwa ajili ya filamu hii  kubwa kuwahi kuwahusisha Watanzania.

“D Street inayo furaha kubwa kugeukia vipaji vya waigizaji wa Kiafrika kwa kuwaunganisha na waigizaji wa kimataifa kama itakavyokuwa kwa ‘The Blue Mauritius’,” anasema Dexter Davis, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya D Street Media Group ya Marekani, inayoanda filamu hiyo

Kwa mujibu wa Davis, filamu hiyo itasambazwa siyo tu Marekani, bali pia katika majumba makubwa ya sinema dunia nzima.

“Ernest na Idris watang’ara, tunasubiri kwa hamu kuwaona tena kwenye skrini kubwa wakifanya makubwa,” anasema Davis
Mapema mwaka huu, wawili hao walicheza filamu iliyojulikana kama ‘Kiumeni’ ambayo pia Ernest alikuwa ni mzalishaji na kushirikiana na Daniel Manege kuiandika. Filamu hiyo ilishinda katika Tamasha la Timataifa la Filamu la Zanzibar ambalo Idris na washiriki wenzake walihudhuria
 “Ninayo furaha kubwa kufanya kazi na Idris katika filamu kubwa kama hii ya The Blue Mauritius. Ni mwaka wa pekee kwa mimi kufanikiwa kufanya kazi na D Street. D Street inabadilisha upepo kwa Afrika inapokuja kwenye suala la kutengeneza filamu,” anasema Ernest 
Kwa upande wake Idris anasema, “Nilikutana Dexter Davis kwenye Maonyesho ya Filamu ya Kimataifa ya Zanzibar mwezi Julai na nilifurahishwa na namna ambavyo amevutiwa na vipaji kutoka Afrika. Alivutiwa kufanya kazi na mimi baada ya kuona ushiriki wangu katika filamu ya ‘Ballin; On the Other side of the World’ na miezi miwili baadaye nilishiriki Katina filamu moja ya Kimarekani. Filamu hizi mbili zimenifanya niweze kufanya kazi nchini Marekani jambo ambalo nilitamani sana,” 
Filamu hiyo inatarajia kuanza kuzalishwa mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka ujao (2018).

ACT WAZALENDO WAPINGA UCHAGUZI ULIOFANYWA NA RAIS KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI

Jana, Oktoba 7, 2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya teuzi mbalimbali ikiwemo uteuzi wa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
ACT Wazalendo tunasikitika kusema Kwamba kama ilivyo desturi, Rais ameamua kuyaweka pembeni matakwa ya Sheria yanayoongoza mchakato wa uteuzi wa Katibu wa Bunge na kuamua kujichagulia apendavyo.

Kutokana na unyeti wa nafasi ya Katibu wa Bunge, na kwa minajili ya kuweka ‘check and balance’ pamoja na kulinda uhuru wa Bunge, kwenye mchakato wa uteuzi wa nafasi husika, sheria imeweka utaratibu wa kufuatwa kwenye uteuzi wa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo basi, mbali na Rais kuwa na mamlaka ya kumteua Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anapaswa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Sheria ya Utawala wa Bunge – The National Assembly (Admintration Act), 2015. Kwa mujibu wa Kifungu cha 7(3) cha Sheria hiyo, Rais atateua jina moja kutoka miongoni mwa majina matatu yaliyopendekezwa na Tume ya Huduma za Bunge. 

Jambo hili sio la hiyari. Ni sharti la lazima la sheria ambalo Rais analazimika kulifuata. Ndio maana kifungu husika kinasema “The Commision shall recommend three names” (Tume ni LAZIMA ipendekeze majina matatu). 
Wajumbe wa Tume ya Huduma za Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 12(2) cha Sheria ya Utawala wa Bunge ni wafuatao:
1. Ndg. Job Ndugai, Spika wa Bunge

2. Ndg. Tulia Akson, Naibu Spika wa Bunge
3. Ndugu Jenister Mhagama – Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Bunge
4. Ndg. Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni
5. Ndg. Magdalena Sakaya – Kamishna wa Bunge (CUF)
6. Ndg. Peter Msigwa – Kamishna wa Bunge (Chadema)
7. Ndg. Salim Hassan Abdullah Turky – (Kamishna wa Bunge – CCM)
8. Ndg. George Masaju
9. Ndg. Mary Chatanda (Kamishna wa Bunge – CCM)
10. Ndg. Kangi Lugola-(Kamishna wa Bunge-CCM)
11. Ndg. Mussa Hassan Zungu-(Kamishna wa Bunge-CCM)
Kwa taarifa tulizonazo, hakuna kikao chochote cha Tume ya Bunge kilichoketi na kupendekeza majina kwa Rais kwa ajili ya uteuzi wa Katibu wa Bunge. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wote wa Tume ya Huduma za Bunge waliohojiwa na vyombo vya habari wamethibitisha pia kutofanyika kwa kikao hicho.
Hitimisho:
1. ACT Wazalendo tunaona kuwa uteuzi huu si tu ni mwendelezo wa Rais kufanya maamuzi bila kuzingatia sheria za nchi bali ni ushahidi mwingine wa wazi wa kudharau mhimili wa Bunge.
2. Ni matumaini yetu kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano na watu wote wanaopenda uhuru na uimara wa Bunge watasimama imara kuupinga uteuzi huu ambao ni kinyume na sheria.
3. Kama Rais hatatengua uteuzi huu na kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria za nchi, ACT Wazalendo kitalifikisha suala hili Mahakamani ili kupata ufafanuzi wa mahakama.
4. Ni wakati muafaka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuishauri serikali kwenye masuala ya kisheria kuwajibika. ACT Wazalendo tunaamini suala hili na vitendo vingine vya huko nyuma vimetokea kwa sababu ya moja ya sababu mbili. Inawezekana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa woga au uzembe, hamshauri Rais ipasavyo au Rais hafuati ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika yote mawili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kama anataka kulinda heshima yake binafsi na ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hana budi KUJIUZULU.
Ado Shaibu

Katibu, Itikadi, Mawasiliano na Uenezi 
ACT Wazalendo 
Oktoba 8, 2017
Dar es salaam

CHIBU(PLATNUM) APELEKWA MAHAMANI NA MOBETO

Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.Image result for DIAMOND & AMISA

Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mobeto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.

Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.

Wakili Zulu amesems leo Alhamisi amesema mteja wao Hamisa Mobeto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.

“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto  (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.

Zulu amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu.

TUTARAJIE MAANDAMANO YA AMANI KUDAI KATIBAMPYA

Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Katiba nchini, (JUKATA) Hebron Mwakagenda  akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu  maandamano ya kudai katiba mpya.

Wakati Sintofahamu kuhusu katiba Mpya nchini Tanzania ikiendelea kuzidi huku Utawala wa awamu ya Tano ukiwa Kimya kuhusu swala hilo,Harakati zilizoanzishwa majuma kadhaa yaliyopita hatimaye yameanza kuzua mambo baada ya Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA kutangaza maandamano makubwa kudai kurejeshwa mchakato wa Katiba mpya.

Mchakato wa Katiba nchini ulisimama kupisha uchaguzi mkuu mwaka 2015 na Tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya Tano kumekuwa kimya huku wanaharakati wakinongona chinichini kuhusu hatma ya mchakato huo ambao unatajwa kuligharimu taifa pesa nyingi kipindi cha ukusanywaji wa maoni yake.

Wakati hayo yakitokea Leo Jukwaa la Katiba Tanzania limetangaza Rasmi azma yake ya kufanya maandamano ya nchi nzima kuishinikiza serikali Kurejesha mchakato wa Katiba mpya.

Akitangaza Maandamano hayo Leo jijini Dar es salaam wakati Wa mkutano na waandishi Wa Habari,Mkurugenzi Mtendaji Wa (JUKATA),Hebron Mwakagenda amesema baada ya mkutano Mkuu Jukwaa hilo uliofanyika mkoani Dodoma mwisho Wa wiki iliyopita wamezimia kifanya maandamano nchi mzima yenye lengo la kudai katiba mpya.

 "Tumeazimia kufanya maandamano katika ngazi ya  kitaifa yatafanyika Jijini Dar es Salaam,yakianzia ofisi za JUKUTA  hapa Mwenge Tarehe 31 mwezi huu wa kumi Saa nne asubuhi na yatahitimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja" amesema Mwakagenda.

Mwakagenda amesema Jukwaa la hilo ni teyari limeshaliandikia barua Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam kutoa taarifa juu ya kusudia kufanya maandamano hayo 

"Maandamano haya  ni ya amani ili kurudisha hamasa ya wananchi kuendelea kushiriki kwenye michakato ya kidemokrasia  hapa nchini"

"Kwa upekee na heshima kubwa sana JUKATA pia tumemwandikia barua Rais Magufuli kumwomba ayapokee maandamano yetu ya amani katika viwanja vya Mnazi Mmoja" Amongeza Kusema Mwakagenda.

Hata hivyo,Mwakagenda amesema kuwa maandamano hayo kwa upande Wa Mikoa  mingine nje ya Dar Maandamano ambapo yatafanyika kila wilaya.

Pamoja na hayo JUKATA wamesema wanaamini watapata ushiriano Wa kutosha Wa Jeshi la Polisi ili maandamano hayo yafanyike kwa amani.