Mahakama ya juu ya rufaa nchini Afrika Kusini imeamuru kwamba Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma lazima akabiliane na mashtaka ya rushwa, kugushi na kujihusisha na mtandao wa utakatishaji fedha.
Mahakama hiyo ilikubali uamuzi wa mahakama ya chini katika uamuzi wake ilioutoa mwaka uliopita, mahakama hiyo ikiwaamuru waendesha mashtaka wanaweza kuyarejesha mashitaka 783 ya rushwa inayohusiana na makubaliano ya kununua silaha ya mwaka 1999.