Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar
Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH ikiingia katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Oman ikiwa na Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo,ikiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi wa Serikali ya Oman.
Meli ya iliyobeba ujumbe kutoka Oman ijulikanayo kwa jina la Fulk Al Salamah ikiwasili katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa na ujumbe wa watu takribani 350 kutoka Oman.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussen Mwinyi akimlaki Waziri wa Mafuta na Gesi toka Oman Dkt. Mohamed Hamed Al- Rumhi ambaye ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman uliowasili na meli ya mfalme ya Fulk Al Salamah katika bandari ya Dar es Salaam leo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi walipokutana katika hafla ya mapokezi ya meli iliyobeba ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman uliowasili katika bandari ya Dar es Salaam leo. Katikati ni Mfanyabiashara wa Tanzania Seif A. Seif.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussen Mwinyi akiwa na kiongozi wa ujumbe kutoka Oman Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohammed Hamed Al-Rumhi wakitazama ngoma toka kwa moja ya kikundi cha watumbuizaji mara baada ya meli ya Fulk Al Salamah ikiwa na ujumbe wa watu 350 kutoka kwa mfalme wa Oman kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam leo. Picha na: Frank Shija - MAELEZO
Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika Zanzibar Oktoba 12, 2017, imeng’oa nanga leo mchana kuelekea Dar es Salaam kuendelea na safari yake ya kusambaza ujumbe wa ‘Amani na upendo’ duniani.
Taarifa kutoka ubalozi mdogo wa Oman zimeeleza kuwa, meli hiyo itakaa Dar es Salaam kwa siku nne kabla kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo hayo.
Akizungumza baada ya kuagana na ujumbe wa meli hiyo bandarini Zanzibar, Balozi Mdogo wa Oman Dk. Al Habsi, ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzbar chini ya Rais wake Dk. Ali Mohamed Shein na wananchi wote kwa mapokezi mazuri na ukarimu mkubwa waliouonesha kwa ndugu zao wa Oman.
Ameomba hali hiyo iendelee, akisema mahaba na ukarimu ndiyo mambo yanayowafungamanisha Wazanzibari na Waomani ambao kihistoria ni ndugu wa miaka mingi.
No comments:
Post a Comment