RASHFOD AIBEBA MAN U


 Image result for PHOTO OF MARCUS RASHFORD
Marcus Rashford, jana alifunga bao pekee katika mchezo wa Champions League dhidi ya Benfica na kuiweka United kileleni mwa kundi lao lakini Rashford huyo huyo anaingia kwenye kundi la majeruhi la Paul Pogba, Eric Bailly na Morouane Fellaini.
Chelsea nao jana walikuwa uwanjani wakishuhudia timu yao ikiongoza mabao mawili na baadaye yakarudi yote lakini wakafanikiwa kutoka suluhu ya mabao matatu kwa matatu dhidi ya As Roma.
Chelsea ambao walimkaribisha Alvaro Morata aliyetoka kuwa majeruhi bado wanamkosa kiungo wao mkabaji Ngolo Kante ambaye aliumia wakati akiwa katika majukumu kuitumikia timu yake ya taifa.
Nafasi ya Kante ilichukuliwa na Tiomoue Bakayoko ambaye taarifa zinasema na yeye ameumia baada ya mchezo wa jana huku mlinzi wa kati David Luiz naye akipata majeraha yatakayomuweka nje kwa muda.
Kocha wa klabu hiyo Antonio Conte amesema hawezi kuhatarisha afya za wachezaji wake na kwa kuwa wameumia kidogo atawaacha nje ya uwanja hadi pale watakapokuwa fiti kuanza kucheza.
Wakati huo huo Antonio Conte amemuambia kocha wa Manchester United Jose Mourinho kwamba aangalie timu yake na aache kufuatilia masuala ya klabu ya Chelsea na kushangazwa na kitendo cha Mou kuwafuatilia.
Kauli ya Antonio Conte inakuja baada ya Jose Mourinho kudai kwamba kuna makocha ambao wachezaji wao wakipata maejeraha huwa wanapiga sana kelele kauli ambayo ilionekana kama kijembe kwa Conte.

No comments: