Image result for PHOTO OF SIMON MSUVA IN MOROCCO
Simon Msuva ameendelea kuwa na mwendelezo mzuri katika maisha yake ya soka la kulipwa,  hiyo ni baada ya kutengeneza bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 wa timu yake Difaa Hassan El Jadida dhidi ya Chabab Rif Hoceima kwenye Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida.
Msuva alipiga krosi katika dakika ya 64 katika mchezo wa Kombe la Ligi Morocco ikatua kichwani kwa Adnane El Ouardy akaudondoshea mpira nyavuni kuipatia bao la kwanza Jadida, kabla ya Hamid Ahadad kufunga la pili dakika ya 89.
Hivyo, Jadida metinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya wiki iliyopita kufungwa 2-1 Uwanja wa Mimoun Al Arsi mjini Al Hoceima, siku ambayo Msuva aliifungia timu yake bao muhimu la ugenini.
Katika mchezo huo wa wikiendi hii ya jana, Msuva alipumzishwa dakika ya 92 na nafasi yake kuchukuliwa na Tarik Astati.
Baada ya mchezo huo, Difaa ambayo ina viporo viwili dhidi ya FUS Rabat na Wydad Cassablanca, itamenyana na FAR Rabat Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat

No comments: