Mwanamitindo maarufu Tanzania ambaye kwa sasa anazungumziwa sana mitandaoni kwa sakata la kuzaa na msanii Diamond Platinumz, Hamisa Mobetto ametoa siri ambayo watu wengi walikuwa hawaifahamu kuhusu mahusiano yake na Diamond.
Mobetto alipohojiwa na baadhi ya vyombo vya habari ametaja kuwa tangu awe katika mahusiano ya kimapenzi na msanii Diamond Platinumz sasa ni takribani miaka tisa na huu unaingia mwaka wa kumi wawili hao kuwa pamoja.
Aidha ameeleza chanzo cha kumfungulia kesi mzazi mwenzake Diamond Platinumz mnamo oktoba 5 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto, amesema kuwa Diamond Platinumz ndiye aliyemshauri wafungue kesi ili kuhakikisha mtoto wake anapata haki yake ya msingi kutoka kwa baba.