Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekunua taarifa ya kukamata watu wanaovaa vimini na kunyoa mtindo wa kiduku.
Hatua
hiyo inakuja baada ya gazeti la kila siku la Nipashe January 17 (leo)
kutoka na kichwa cha habari; Polisi yakamata wavaa vimini, kunyoa
viduku.
Akizungumza
Dar es Salaam Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema taarifa
hiyo haina ukweli wowote kwani mwandishi ameandika kitu ambacho
hakukisema.
“Nilitaka
nitoe ufafanuzi nikikanusha haya ambayo yameandikwa hayakusemwa na
Jeshi la Polisi, anayasema mwenyewe mwandishi kwa interest yake na sana
alichokuwa anatafuta ni umaarufu wa stori,” amesema.
“Ninamtaka
sasa arudi kwa watanzania aombe radhi ili kuondosha usumbufu
uliojitokeza, nimepigiwa simu kuanzia jana toka maeneo mbali mbali kwa
jambo ambalo kimsingi halijafanywa na Jeshi la Polisi,” amesisitiza.
No comments:
Post a Comment