Serikali ya Tanzania imesema inapitia upya usajili wa meli na
kuhakiki taarifa za meli zote zilizosajiliwa nchini humo ili kuondokana
na athari za meli zinazopeperusha bendera ya Tanzania zinazopatikana na
makosa katika maeneo mbalimbali duniani...
Makamu wa Rais Samia Suluhuu Hassan amezungumzia hatua ya uhakiki
wa meli hizo katika mkutano na waandishi wa habari, jijini Dar es
Salaam, alipokuwa akitoa taarifa kwa wananchi juu ya maazimio
yaliyofikiwa katika mkutano ulioshirikisha wataalamu kutoka Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano,kushughulikia meli
zinazopeperusha Bendera ya Tanzania,kufuatia hivi karibuni kukamatwa kwa
meli za Kaluba iliyokamatwa Jamhuri ya watu wa Dominica,ikiwa na
takribani tani 1,600 za dawa za kulevya na Andromeda iliyokamatwa
Ugiriki ikisafirisha zana zinazotumika kutengeneza silaha kinyume na
sheria za kimataifa kwenda Libya.
Serikali ya Tanzania imesema haihusiki na meli hizo zilizokamatwa
licha ya kwamba zimesajiliwa nchini kupitia taasisi ya Mamlaka ya
usafiri baharini Zanzibar, yenye mamlaka ya kusajili meli za ndani na
nje.
Wakati hayo yakiendelea jana wafanyabiashara wawili wakurugenzi wa
kampuni tofauti za meli walifikishwa katika mahakama ya Kisutu jijini
Dar es salaam wakituhukiwa kupeperusha bendera ya Tanznaia katika meli
ya kichina kinyume cha sheria Wafanyabiashara hao ni Issa Haji
mkurugenzi wa kampuni ya meli ya Lucky na Abdullah Issa Hanga wa kampuni
ya meli ya Saha.
No comments:
Post a Comment