SEKTA YA MADINI LAZIMA IWE NA MCHANGO MKUBWA KWENYE PATO LA TAIFA: MHE DOTTO BITEKO
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe
Dotto Mashaka Biteko akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na
wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini
Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisisitiza jambo
wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi
wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Stanislaus Nyongo akizungumza jambo
kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri mwenzake katika Wizara hiyo Mhe Dotto
Mashaka Biteko kuzungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na
wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini
Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akizungumza na
wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini
mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.
Na Mathias Canal, Dodoma
Sekta ya Madini inachangia kati ya
asilimia 3.5 mpaka 4 katika Pato la Taifa ukilinganisha na sekta zingine
ambazo zimejitutumua kwa kiasi kikubwa katika mchango mahususi wa pato
la Taifa nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe
Dotto Mashaka Biteko amebainisha kuwa kiasi cha kati ya asilimia 3.5
mpaka 4 ni kidogo sana ukilinganisha na umuhimu wa sekta hiyo nchini
hivyo Wizara ya Madini imekusudia kuongeza tija katika mchango wa pato
la Taifa kupitia sekta hiyo muhimu ya Madini.
Mhe Biteko amebainisha hayo Leo Januari
15, 2018 wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na
watumishi wa Wizara ya Madini ofisi Kuu Mjini Dodoma huku akiwataka
watumishi wote kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uzalendo mkubwa kwa
manufaa ya Taifa.
Alisema kuwa sekta ya Madini ni muhimu
nchini kutokana na rasilimali Madini ilizonazo hivyo watumishi wote
wanapaswa kufikiria namna ya kufanya kazi kwa tija ili kuwa na ongezeko
la mchango mkubwa katika pato la Taifa.
"Natamani nione kwenye taarifa ya robo
mwaka ya BOT ikisoma kwamba sekta ya madini inachangia angalau asilimia
10 ya Pato la Taifa kuliko ilivyo hivi sasa na hilo naamini linawezekana
kwa ushirikiano wa pamoja" Alisisitiza Mhe Biteko
Mhe Biteko alisema kuwa hakuna mtu
yeyote ambaye atatutumua mabega kwamba ni mkubwa katika Wizara badala
yake ukubwa wa cheo na umri utaonekana katika matokeo muhimu na makubwa
katika utendaji kazi.
"Mimi kuwa Naibu Waziri hapa So What...
kama sitofanya kazi yenye matokeo makubwa kutokana na imani niliyopewa
na Rais nitakuwa si lolote, hivyo kwa ushirikiano wenu pekee tutaweza
kutimiza utendaji uliotukuka na wenye manufaa makubwa" Alikaririwa Mhe
Biteko wakati akizungumza na watumishi wa Wizara ya Madini
Mhe Biteko alisema kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri
kwa manufaa makubwa ya watanzania wote hivyo watumishi mbalimbali wa
serikali, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuunga mkono
jitihada hizo pasina kurudisha nyuma makusudi na matakwa ya utekelezaji
wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwaka 2015-2020.
Asubuhi
siku ya Jumatatu Januari 8, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alimuapisha Mhe Dotto Mashaka
Biteko kuwa Naibu Waziri wa madini, Ikulu Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment