Chama kinachotawala nchini Liberia, Unity party, kimemfukuza rais
anayeondoka wa nchi hiyo, Ellen Johnson Sirleaf, kutoka kwa uanachama
Chama hicho kilipiga kura ya kumwondoa siku ya Jumamposi na hatua
hiyo ilichukuliwa baada ya tuhuma kwamba hakumuunga mkono makamu wake wa
rais Joseph Boakai kama mgombea urais kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka
jana.
Boakai, ambaye alikuwa makamu wa rais kwa miaka 12, alishindwa na nyota wa zamani wa soka, George Waeh.
Johnson Sirleaf, ambaye ni mshindi wa tuzo la amani la Nobel, hangegombea tena urais kwa sababu haruhusiwi na katiba ya Liberia kufanya hivyo.
Wakosoaji wa Boakai walimshutumu kwa kile walichokiita "kutofanya mengi ya kuimarisha taifa" akiwa makamu wa rais.
Iwapo kila kitu kitaenda shwari, Liberia itashuhudia ubadilishanaji mamlaka kwa njia ya kidemokrasia kwa mara ya kwanza katika kipindi cha Zaidi ya miaka 70.

No comments:
Post a Comment