MABALOZI WA ZAMANI WALALAMIA.................



Wahamiaji wa Afrika na Haiti waliokuwa na azma ya kuomba hifadhi nchini Marekani, wakiwa Mexicali, Mexico, Oktoba. 5, 2016.
"Wahamiaji wanaokuja Marekani kutoka Afrika, ni watu wenye mafanikio makubwa.Ninataka kusema kutoka ndani ya moyo wangu, sisi ni sehemu yenu,sisi ni sehemu ya jumuiya ya ulimengu. Hatua cha ziada isipokuwa heshima kwenu," balozi wa Marekani nchini Zimbabwe.
Mabalozi 48 wa Marekani waliokuwa wakihudumu katika nchini mbali mbali barani Afrika wamepeleka barua White House, kuelezea ‘wasi wasi mkubwa’ juu matamshi yaliripotiwa kutolewa na rais Donald Trump akitumia lugha mbaya kuyaita mataifa ya Afrika.
“Sisi mabalozi wa zamani wa Marekani katika nchi 48 za Afrika, tunaandika kuelezea wasi wasi wetu mkubwa sana kuhusiana na ripoti juu ya matamshi yako ya karibuni kuhusu nchi za kiafrika na kuthibitisha umuhimu wa washirika wetu na mataifa takriban 50 ya Afrika,” barua hiyo imesema. “Kama mabalozi wa Marekani wa nje ya nchi tumeona Afrika yenye mambo mengi na utamaduni tajiri sasa, yenye ustahmilivu, na ukarimu mkubwa na huruma.”
Barua iliwapongeza wajasiriamali, wasanii, wanaharakati, wana mazingira, na wasomi barani humo, wakati wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza uhusiano mzuri kati ya Marekani na mataifa 54 ya Afrika.
“Tuna matumaini kwamba utatathmini maoni yako kwa Afrika na raia wake, na kutambua umuhimu wa michango ya waafrika na wamarekani weusi ambayo wameitoa na kuendelea kuitoa kwa nchi yetu, historia yetu, na kuendeleza uhusiano wa kudmu ambao siku zote utaiunganisha Afrika na Marekani,” imesema barua.
Jumatano, katika hali ya kupinga matamshi ya Trump yaliyoripotiwa, balozi wa Marekani kwa Zimbabwe, Harry Thomas Jr. amesema kwamba nchi yake imewakaribisha waafrika wote wahamiaji na wageni.
“Ningependa kusema kwa niaba ya ubalozi wetu, serikali yangu, watu wa Marekani, tuna heshima kubwa kwa Zimbabwe, kwa bara la Afrika, watu wake, utamaduni wake, mila zake,” amesema akimuelezea rais Emmerson Mnangagwa na waliohudhuria sherehe za kupokea msaada wa afya mjini Harare.
“Wahamiaji wanaokuja Marekani kutoka Afrika, hasa Zimbabawe ni watu wenye mafanikio makubwa. Ninataka kusema kutoka ndani ya moyo wangu, sisi ni sehemu yenu, sisi ni sehemu ya jumuiya ya ulimwengu. Hatuna chochote zaidi ya heshima kwenu na tunawakaribisha kwetu kama wageni au wakazi, amesema.

No comments: