Picha : YALIYOJIRI KWENYE SHEREHE YA HARUSI YA SHILOLE
Msanii
wa Muziki wa Bongo Fleva na Mjasiriamali, Shilole ‘Shishi Baby” jana
amefanya sherehe ya harusi yake aliyofunga na mumewe Uchebe katika
ukumbi ulioko Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
Sherehe hiyo ilipambwa na burudani mbalimbali na ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa filamu na muziki wa Bongo Fleva.
Wasanii
mbalimbali waliohudhuria katika sherehe hizo walijaribu kumfurahisha
bibi harusi pamoja na mumewe kwa staili tofauti tofauti huku
zikiambatana na zawadi kem kem.
Rais
wa WCB, Diamond Platnumz alitoa kali ya mwaka katika sherehe ya harusi
ya Shilole na Uchebe baada ya kumtaka bibi harusi huyo kuchagua zawadi
ambayo anaitaka kutoka kwake. Baada ya Diamond kusema hivyo, Shishi
alimuomba Diamondi kumsaidia kuitangaza biashara yake mpya ya Shishi
Chili, ambapo Diamond alikubali ombi hilo.
Naye
msanii ambaye yuko chini ya lebo ya WCB, Harmonise hakuacha kuonyesha
makali yake baada ya kumtaka Shilole atafute gari aina ya Toyota Noah,
yenye thamani ya shilingi za kitanzania, milioni 9 ambayo yeye
(Harmonise) atailipia na itatumika katika kurahisisha biashara za
Shishi.
Kwa
upande wao Jux na Vanessa nao hawakubaki nyuma, ambapo Jux aliahidi
kumlipiaa ada ya mwaka mzima mtoto wa Shilole katika shule anayosoma,
huku mpenzi wake Vanessa akijitolea kuwalipia Hoteli ya Nyota tano ya
kilimanjaro, Shilole na mumewe Uchebe.
Msanii
Shilole ambaye pia ni muigizaji wa filamu hapa nchini, amejikita kwenye
ujasiriamali ambapo kwa sasa anamiliki mghahawa pamoja na bidhaa ya
‘shishi chili’.
No comments:
Post a Comment