AGUERO AREJEA UWANJANI

Image result for photo of sergio aguero

Sergio Aguero amefungia Manchester City mabao 176 - amepungukiwa na moja tu kufunga rekodi.
Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amerejea mazoezini siku 11 baada yake kuvunjika ubavu katika ajali ya barabarani mjini Amsterdam.
Aguero, 29, alikuwa ametarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki kadha
Hata hivyo, alirejea kufanya mazoezi mepesi Jumanne.
City wamesema mchezaji huyo wa Argentina ataendelea "kuimarisha hali yake ya mwili siku zijazo akilenga kurejea kikosini".
Aguero anahitaji bao moja pekee kufikia rekodi ya ufungaji mabao City ya Eric Brook ambayo ni mabao 177.
City wanaongoza Ligi ya Premia kwa wingi wa mabao, mbele ya Manchester United, na watakutana na Stoke siku ya Jumamosi.
Aguero alijeruhiwa akiwa kwenye teksi akisafiri baada ya kuhudhuria tamasha ya muziki. Teksi hiyo iligonga boriti ya taa barabarani.
Alikuwa ameenda Amsterdam kumuona nyota wa muziki kutoka Colombia Maluma akitumbuiza.

No comments: