Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola akiongea na washiriki wa mradi wa Uchumi wa Kijani ndani ya Hifadhi ya Hai (GEBR) wakati akifungua mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO iliyofanyika mjini Tanga. Lengo la mradi huo ilikuwa ni kupunguza umaskini, kuhifadhi bionuwai na maendeleo endelevu katika nchi za kushini mwa Jangwa la Sahara - Usambara ya Mashariki, Tanzania. P
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi ambaye alimwakilisha mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella akifungua rasmi na kumkaribisha mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO.
Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza wakati akifungua mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO iliyofanyika mjini Tanga. Meza kuu...
Mhifadhi wa Mazingira ya asili ya Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi.
Washiriki wa mradi huo wakiuliza maswali...
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola ameitaka jamii kujenga tabia ya kutunza mazingira katika maeneo yao kwa faida ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo. Katibu mkuu Profesa Kamuzola ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akifunga mafunzo ya mradi wa uchumi wa kijani chini ya jangwa la Sahara, yaliofanyika jijini Tanga. Alisema kuwa ni vyema wananchi wakajua umuhimu halisi wa kutunza mazingira na kuyatumia katika kujiongezea kipato. Mradi wa uchumi wa kijani chini ya Jangwa la Sahara ulikuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya ushirikiano wa kimtaifa KOICA chini ya Programu ya UNESCO. Kwa upande wake Katibu tawala wa mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi ameisisitiza jamii kupokea vizuri miradi wanayokuwa wakiletewa na wafadhili ili iwaongezee kipata na elimu zaidi katika utunzaji wa mazingira. "Wananchi ni vyema mkabadirika na kuacha kuishi bila kutambua kuwa mazingira ukiyatunza yanakuletea kipato cha juu kabisa, ukiangalia unaona unaweza kutengeneza mkaa kwa kutumia magunz ya mahindi baada ya kuwa umeshavuna hiyo ni faida tosha kabisa," alisema Mhandishi Zena Saidi. Naye Mhifadhi wa Mazingira ya asili ya Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi aliwashukuru sana wafadhili wa mradi huo kwa kuweza kutoa elimu kwa wananchi ... elimu ambayo imekuwa endelevu na kuwazalishia kipato cha hali ya juu. Bi. Mwanaidi alisema kuwa wananchi baaada ya kupewa elimu wameweza kujiendeleza katika miradi mbali mbali ikiwemo kutengeneza mkaa kwa kutumia majani ya mimea/magunzi, ufugaji wa vipepeo ambao wamekuwa wakiwazalisha kwa kutengeneza mapambo, kilimo cha uyoga, kilimo cha asali. Hifadhi ya mazingira ya amani inaendeleza ikolojia na baionowai ambazo ni hadimu duniani na zinapatikana katika milima ya usambara mashariki, na ina jumla ya vijiji 72.
No comments:
Post a Comment