TUTARAJIE MAANDAMANO YA AMANI KUDAI KATIBAMPYA


Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Katiba nchini, (JUKATA) Hebron Mwakagenda  akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu  maandamano ya kudai katiba mpya.

Wakati Sintofahamu kuhusu katiba Mpya nchini Tanzania ikiendelea kuzidi huku Utawala wa awamu ya Tano ukiwa Kimya kuhusu swala hilo,Harakati zilizoanzishwa majuma kadhaa yaliyopita hatimaye yameanza kuzua mambo baada ya Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA kutangaza maandamano makubwa kudai kurejeshwa mchakato wa Katiba mpya.

Mchakato wa Katiba nchini ulisimama kupisha uchaguzi mkuu mwaka 2015 na Tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya Tano kumekuwa kimya huku wanaharakati wakinongona chinichini kuhusu hatma ya mchakato huo ambao unatajwa kuligharimu taifa pesa nyingi kipindi cha ukusanywaji wa maoni yake.

Wakati hayo yakitokea Leo Jukwaa la Katiba Tanzania limetangaza Rasmi azma yake ya kufanya maandamano ya nchi nzima kuishinikiza serikali Kurejesha mchakato wa Katiba mpya.

Akitangaza Maandamano hayo Leo jijini Dar es salaam wakati Wa mkutano na waandishi Wa Habari,Mkurugenzi Mtendaji Wa (JUKATA),Hebron Mwakagenda amesema baada ya mkutano Mkuu Jukwaa hilo uliofanyika mkoani Dodoma mwisho Wa wiki iliyopita wamezimia kifanya maandamano nchi mzima yenye lengo la kudai katiba mpya.

 "Tumeazimia kufanya maandamano katika ngazi ya  kitaifa yatafanyika Jijini Dar es Salaam,yakianzia ofisi za JUKUTA  hapa Mwenge Tarehe 31 mwezi huu wa kumi Saa nne asubuhi na yatahitimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja" amesema Mwakagenda.

Mwakagenda amesema Jukwaa la hilo ni teyari limeshaliandikia barua Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam kutoa taarifa juu ya kusudia kufanya maandamano hayo 

"Maandamano haya  ni ya amani ili kurudisha hamasa ya wananchi kuendelea kushiriki kwenye michakato ya kidemokrasia  hapa nchini"

"Kwa upekee na heshima kubwa sana JUKATA pia tumemwandikia barua Rais Magufuli kumwomba ayapokee maandamano yetu ya amani katika viwanja vya Mnazi Mmoja" Amongeza Kusema Mwakagenda.

Hata hivyo,Mwakagenda amesema kuwa maandamano hayo kwa upande Wa Mikoa  mingine nje ya Dar Maandamano ambapo yatafanyika kila wilaya.

Pamoja na hayo JUKATA wamesema wanaamini watapata ushiriano Wa kutosha Wa Jeshi la Polisi ili maandamano hayo yafanyike kwa amani.

No comments: