MPYA:TCU YATOA MAAGIZO MAZITO KWA WANAFUNZI WANAOTEGEMEA KUOMBA VYUO VIKUU MWAKA HUU 2017/2018


Hapo jana Tume ya vyuo Vikuu Tanzania TCU iliitisha vyombo vya habari na kuamua kuzungumzia swala zima la udahili kwa wanafunzi wa kidato cha sita mwaka huu 2017/2018.

Kaimu katibu Mkuu Nacte alisema Tume imetekeleza agizo  la kuawataka wanafunzi waombe vyuo wanavyotaka wenyewe ambapo hapo nyuma ilibainika kuwamba TCU walikuwa wakiwapangia wanafunzi vyuo.

Jumla ya wanafunzi  70,550 wamepata daraja la kwanza hadi la nne,kati ya hao ,Amema kwamba mwaka huu zaidi ya 50.7% ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka huu wanatarjiwa kujiunga na elimu ya juu 2017/2018.

Kwa mwaka wa masomo 2017/2018,udahili wa wanafunzi rasimi utaanza tarehe 22 july 2017 kwenye vyuo vyote hapa nchini na maombi yatatumwa moja kwa moja chuoni na sio TCU tena.

TCU IMETOA MAAGIZO YAFUATAYO KWA WANAFUNZI  WANAOTARAJIA KUOMBA

1. WAOMBAJI WATUME MAOMBI MOJA KWA MOJA KWENYE CHUO HUSIKA,VYUO VINA TAARIFA HIYO TAYARI.

2.WAOMBE KUSOMA KTIKA PROGRAMME NA VYUO AMBAVYO VIMEIDHINISHWA NA TCU NA NACTE,ORODHA IPO KWENYE WEBSITE YA TUME TAYARI.

3.WAOMBAJI WANASHAURIWA WAOMBE WENYEWE USIMTUME MTU,KUEPUSHA USUMBUFU BAADAE.

4.ENDSAPO UTACHAGULIWA CHUO ZAIDI YA KIMOJA,UTAPEWA TAARIFA NA UTATAKIWA KUCHAGUA CHUO KIMOJA TU.

5.MNASHAURIWA KUSOMA KWA MAKINI SIFA ZILIZOTANGAZWA 2017/2018.

6.TCU HAITATOZA ADA YOYOTE WAKATI WA UOMBAJI WA VYUO VIKUU,ILA KUTAKUWA NA ADA KATIKA CHUO UNACHOTAKA KUOMBA.

7.MNASHAURIWA NA KUSISITIZWA KUOMBA PROGRAMMES TU ZILIZOIDHINISHWA NA TCU NA NACTE.

8.VYUO VIKUU VINAKUMBUSHWA KUAINISHA ADA YA KILA PROGRAMME WAKATI ZIKITANGAZA KOZI ZAKE.

9.VYUO VINAKUMBUSHWA KUDAHILI WANAFUNZI WENYE SIFA STAHIKI KAMA ZILIVYOAINISHWA NA KUPITISHWA NA TCU AU NACTE.

No comments: