simba wakanusa kumfukuza omog

Uongozi wa klabu ya Simba SC umekanusha taarifa za kumfukuza kazi kocha Joseph Omog, kama ilivyoripotiwa katika mitandao ya kijamii mapema hii leo. Kwa niaba ya uongozi wa klabu ya Simba, mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu hiyo ya Msimbazi Haji Manara amezungumza na Dar24 na kusema, Simba haijatoa taarifa yeyote kuhusiana na mabadiliko yanayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii. Manara amesema anaamini wanaotoa taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii hawaitakii mema klabu ya Simba, ambayo bado inamuamini kocha huyo kutoka nchini Cameroon. ‘Nimeshaeleza toka awali kuwa, hakuna mechi tano wala huo mpango wa kumwondoa kocha Omog au benchi zima la ufundi, klabu ya Simba haina mpango huo.

No comments: