Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umeitisha maandamano leo Jumanne nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi, ikiwa ni hatua ya kushinikiza kujiuzuru kwa baadhi ya maafisa wa juu wa tume hiyo walioshiriki kuandaa uchaguzi mkuu wa August 8 mwaka huu uliobatilishwa na mahakama ya juu nchini.
Tayari rais Uhuru kenyata ametoa onyo kwa wapinzani ambapo amesema kuwa watakumbana na mkono wa sheria iwapo maandamano yao yataingilia shughuli za kiuchumi zaraia wa nchi hiyo.
”Endeleeni na maandamano yenu, mkigusa mboga za mama wanaouza barabarani, tuko na nyinyi. Mkigusa maduka ya watu tuko na nyinyi. Lakini kama hamna lingine lolote la kufanya isipokuwa kutembea – tembeeni. Mimi nawaambia hata mukinitukana mpaka asubuhi, haitabadilisha dunia”, alisema Kenyata.