news:sasa wamehamia kwa singida united sport pesa

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa imeendelea kuonesha dhamira
yake katika kuhakikisha Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu ujao
2017/2018 kunakuwa na ushindani wa kweli kutoka katika timu mbalimbli
kutokana na jitihada zake za kudhamini vilabu kadhaa. Baada ya kuingia
mkataba wa udhamini na Simba na Yanga katika kipindi cha miaka mitano
wenye thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 4, leo May 23 wametangaza kuingia
mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini na club ya Singida United ya Singida
wenye thamani ya Tsh milioni 250.

No comments: