CHAMA
cha ACT-Wazalendo kimeainisha mambo tisa ambayo Serikali ya awamu ya
tano imefanya vibaya katika miaka miwili ya uongozi wa Rais John
Magufuli.
Mwenyekiti
wa chama hicho, Yeremia Maganja, akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam amesema mambo hayo yamegawanywa katika mafungu
makuu matatu.
“Leo
tutatoa tathmini yetu ya miaka miwili ya utawala huu, tathmini hii ni
zao la utafiti husika uliofanyika nchi nzima. Tathmini yetu itaainisha
mambo 9 ambayo tunaamini hayakufanywa vizuri kabisa na Serikali,”
amesema Maganja.
“ACT
Wazalendo inao wajibu wa kujihusisha na masuala ya watu, tunatimiza
wajibu huo kwa tathmini hii ya kuangazia mambo haya risa ambayo ni
mapungufu ndani ya miaka miwili hii ya utawala huu,”ameongeza.
Amesema mambo hayo yamefanya vibaya kiasi cha kuleta athari nchini, kisiasa, kiutawala na kiuchumi.
Ametaja maeneo hayo kuwa ni ya, Haki za Msingi Usimamizi wa Uchumi na Uendeshaji wa Nchi.
Haki za Msingi
Maganja
amesema kumekuwepo na uminywaji wa uhuru wa Vyama vya Siasa Kufanya
mikutano ya hadhara, uhuru wa Vyombo vya habari, pamoja na Uhuru wa
Kujieleza, Kuminywa kwa haki ya wazanzibari kuchagua viongozi wao na
Kupuuzwa kwa matakwa ya Katiba Mpya.
Usimamizi wa Uchumi wa Nchi
Amesema
kumekuwepo kwa hali ya Kusinyaa kwa Uchumi wa Nchi, Kudhohofishwa kwa
Sekta Binafsi, Mazingira Mabaya ya Biashara Nchini, pamoja Kupaa kwa
Deni la Taif.
Mengine ni kutelekezwa kwa kilimo na utekelezaji wa miradi mikubwa bila kuzingatia maslahi ya umma.
Uendeshaji wa nchi
Mwenyekiti huyo amesema
katika kipengele hiki serikali hii imefanya vibaya kwa uvunjaji wa
misingi ya Sera ya Mambo ya Nje, unyanyasaji wa watumishi wa umma na
utawala unaovunja taasisi za kikatiba na kisheria kutoakana na kwamba
utawala huu umekuwa wa mtu mmoja.
No comments:
Post a Comment