MVUA KUBWA YANYESHA NA KUEZUA MAPAA YA NYUMBA KIGOMA



MTU mmoja amekufa na nyumba mbili zimeezuliwa mapaa yake na kuanguka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha ikiwa ni msimu wa mvua za vuli ambao umeanza mkoani Kigoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno alisema hayo mjini Kigoma na kumtaja aliyekumbwa na mkasa huo ni Jumanne Masudi (54) ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyarubanda, Tarafa ya Kalinzi Kigoma Vijijini na kwamba alikumbwa na mauti saa 10:30 jioni juzi akiwa nyumbani kwake.
Kamanda Otieno alisema wakati mvua ikinyesha, Masudi alikuwa nyumbani kwake na kwamba mvua hiyo iliyoambatana na upepo, iliezua paa la nyumba aliyokuwemo na kusababisha ukuta kuanguka, ambao ulimuangukia kichwani na kusababisha kifo chake.
Maafa hayo yamekuja siku moja baada ya juzi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Agnes Kijazi kuzungumzia mwelekeo wa mvua za msimu, akisema kutakuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi yanayopata msimu moja wa mvua kwa mwaka, na kwamba mvua kubwa inatarajiwa Januari mwakani.
"Msimu huu ni mahsusi katika maeneo ya magharibi mwa nchi, Kanda ya kati, nyanda za juu Kusini Magharibi, Kusini mwa nchi, maeneo ya Kusini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na Ukanda wa Pwani ya Kusini. Mvua inatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya Novemba na kuisha wiki ya nne ya Aprili, 2018,” alieleza Dk Kijazi.
Katika tukio lingine, Kamanda Otieno alisema dereva wa pikipiki ya abiria maarufu bodaboda, William Nashon (22) ameuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na mtu asiyefahamika aliyekuwa abiria wake, aliyemtoa eneo la Ujenzi manispaa ya Kigoma Ujiji na kumpeleka eneo la Burega.
Otieno alisema Nashon alikufa akiwa anakaribia Hospitali ya Mkoa ya Kigoma ya Maweni, akifanya jitihada za kuokoa maisha yake na kwamba alianguka baada ya kupoteza damu nyingi kutokana na jeraha alilolipata na hivyo kufariki dunia. Hata hivyo, licha ya mauaji hayo muuaji hakuchukua kitu chochote kutoka kwa mtu huyo na polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu kadhia hiyo.

BANK YA WATU WA ZANZIBAR YAKABITHI HUNDI KUSAIDIA UJENZI WA SHULE NA NUMBA ZA WALIMU MKOANI



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayuob Mohammed Mahmoud na Mkurugenzi Masoko wa PBZ Said Ali Mwinyigogo.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini kwa ajili ya kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu wa Mkoa wa Dar es Salaamkulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paulo Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marine Thomas  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonda akizungumza na kutowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo kufanikisha ujenzi wa Ofisi za Walimu wea Shule za Dar es Salaam,kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidhi.


NAIBU WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA BOHARI YA DAWA(MSD



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile, akizungumza na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), alipofanya ziara ya siku moja kutembelea ofisi hizo jijini Dar es Salaam leo.



 Mkurugenzi  Mkuu   wa   MSD,  Bwana   Laurean   Rugambwa  Bwanakunu (kulia), akitoa maelezo kwa Mhe. Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulileleo ametembelea Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pamoja na mambo mengine amepata taarifa yautendaji ya MSD kuhusu usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na kusemakuwa bajeti ya dawa inayotolewa na serikali iendane na hali halisi ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye hospitali na vituo vya afya nchini.Naibu waziri huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kuitembelea MSD tangu ateuliwe kwenyenafasi   hiyo, amesema   hatua   ya   serikali   kuongeza   bajeti   ya   dawa   kuanzia   mwaka   wa   fedha uliopita na mwaka huu ina lengo la kupunguza gharama ya dawa na kuhakikisha upatikanaji wadawa muhimu kwenye vituo vyote vya Afya vya umma ili kumpunguzia mwananchi gharama zamatibabu.Kwa upande mwingine Mhe. Ndugulile amewataka watendaji wa MSD kuwa na utaratibu wakuwatembelea wateja wao ili kuboresha huduma zaidi baada ya kusikiliza maoni, malalamiko n ahata   ushauri   wao.   Sambambana   hilo   amewaagiza     MSD   kitengo   cha   huduma   kwa   watejakutembelea   wateja   wao   na   kuhakikisha   kitengo   cha   Manununuzi   Maalumu   (SpecialProcurement) kinaongeza kasi kwenye manunuzi.Naye  Mkurugenzi  Mkuu   wa   MSD,  Bwana   Laurean   Rugambwa  Bwanakunu   ameeleza   kuwakutokana na hatua ya MSD kuagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, bei ya dawana vifaa tiba imekuwa nafuu kwa watumiaji na kueleza kuwa mpaka sasa tayari MSD imetoamikataba kwa wazalishaji 104, ambapo 11 kati yao ni kutoka ndani ya nchi. Mikataba hiyo nikwa ajili ya dawa na vifaa tiba takribani  700.Aidha, ameeleza kuwa kiutaratibu MSD hupeleka dawa moja kwa moja vituoni mara nne kwamwaka, yaani kila baada ya miezi mitatu, mpango wa MSD sasa hivi ni kufikisha dawa hizo kilabaada ya miezi miwili kwa mwaka mzima. Amesema hatua hiyo ya kupeleka dawa moja kwamoja vituoni itapelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa nyakati zote vituoni, hasa maeneoya vijijini. 
Naibu  Waziri  huyo ameipongeza  MSD   kwa   koboresha   utendaji   wake,   hasa  katika   hatua   yakupunguza   muda   wa   taratibu   za   ununuzi kutoka   miezi   tisa   hadi   miezi sita   kwa  ajili   yakukamilisha   mchakato   mzima   wa   manunuzi,   kwa   kufuata   sheria   na   taratibu   za   ununuzi   wa Umma.   Katika ziara   hiyo, Mhe.   Ndugulile   amepewa   taarifa   ya   kitengo   cha   ufuatiliaji   wamwenendo wa kazi za kila siku za MSD, kijulikancho kama Strategic management office (SMO)ambacho kiko chini ya ofisi ya Mkurugenzi Mkuu. 
Amewapogenza watendaji wote wa MSDkwa mabadiliko wanayofanya hasa kwa wateja wao na watanzania kwa ujumla.Naibu Waziri huyo amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD)tangu mwezi Septemba, 2012 hadi mwezi Julai, 2016.

KAULI YA LULU JUU YA KESI YAKE DHIDI YA KANUMBA AMBAYO INASOMWA KESHO

ALICHOKISEMA LULU KUHUSU KESI YAKE YA KANUMBA AMBAYO INASOMWA TENA KESHO


Image result for lulu michael
Ikiwa imebakia siku moja kuanza kusikilizwa tena kwa kesi ya mauaji ambayo inamkabili, msanii Elizabeth Michael (Lulu) amesema yupo tayari kukabiliana na kesi hiyo, ambayo alijua ipo siku itarudi tena.
Lulu ameyasema hayo leo alipokuwa  kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa alikuwa na taarifa ya kesi hiyo kabla watu hawajaipata kwenye mitandao, na utaratibu wa kisheria ulifuatwa.

“Unajua watu hawajui sheria, kesi haikuwahi kuisha ni pocedure ya kawaida ya mahakama imefuatwa na ni muda wake umefika sasa , siyo kama imeibuka tu, na kwasababu mimi ndiye muhusika nimepata taarifa kwa njia ya kisheria siyo kama nyie kwenye mitandao, na pengine niliipata kabla yenu”, amesema Lulu.

Lulu ameendelea kusema kwamba kuwepo kwa kesi hiyo kunamuathiri kwa kiasi kikubwa kwenye kazi zake na maisha yake kiujumla.

Kesi inayomkabili muigizaji huyo wa bongo movie inatarajia kusikilizwa tena kesho Oktoba 19, 2017 baada ya kuwa nje kwa dhamana kwa muda mrefu.

Elizabeth Michael (Lulu) anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo bila kukusudia cha  aliyewahi kuwa muigizaji  wa filamu nchini, Steven Kanumba, mnamo  April 7,  2012 .

WAZIRI KIGWANGARA ATEMBELEA MELI YA MFALME WA OMANI

Waziri wa Maliasili Dkt. Kigwangalla atembelea meli ya Mfalme wa Oman *Afanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Utalii wa Oman Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema Tanzania na Nchi ya Oman wamefanya mazungumzo ya pamoja ya namna ya kukuza sekta ya Utalii baina ya nchi hizo mbili ambapo watashirikiana katika muingiliano wa Watalii watakaokuwa wakitokea moja kwa moja Oman na kuja Tanzania. “Tumeweza kuzungumzia ushirikiano wa sekta ya Utalii. Hii ni pamoja na kuanzisha soko la pamoja kati ya Oman na Tanzania. Watalii wanaokwenda Oman wanaotaka kuja nchi za Afrika basi waunganishwe moja kwa moja kutoka Oman na kuja Tanzania kwani wenzetu wana watalii wengi kuliko sisi. Hivyo ujio wao hapa nchini ni faida kubwa kabisa na tumejifunza mengi katika sekta hii. Pia tumeweza kujifunza namna wenzetu wanavyoitangaza nchi yao na sisi tutatumia uzoefu huo kuboresha sekta hii ya Utalii kama dhamana tuliyopewa” alieleza Dk. Kigwangalla. Awali Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika mapema jana Jijini Dar e Salaam ikiwa katika msafara wa kitaifa kati ya Serikali ya Oman na Tanzania. Aidha, katika tukio hilo Mh. Waziri DK. Kigwangalla aliweza kuungana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu Hassan katika chakula cha mchana ndani ya Meli hiyo ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’. Meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ ipo nchini hadi Oktoba 21.2017. ambapo ipo nchini kusambaza ujumbe wa ‘Amani na upendo’ duniani ambapo ikitoka Tanzania inatarajia kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo hayo.Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi wakati Dk. Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman iliyopo nchini.
Moja ya alama za kuvutia za Taifa la Oman
Moja ya usafiri unatumika katika nyanja za Utalii nchini Oman
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi wakati Dk. Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman iliyopo nchini.
Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi akitoa maelezo kwa Waziri wa Maliasili Dk. Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman iliyopo nchini.
Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kumaliza kwa tukio la chakula cha mchana ndani ya meli ya Mfalme wa Oman, mapema leo Jijini Dar e Salaam.
Waziri Maliasili na Utalii DK. Kigwangalla akizungumza katika tukio hilomara baada ya chakula cha mchana ndani ya Meli ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’.
Waziri Maliasili na Utalii DK. Kigwangalla akizungumza katika tukio hilomara baada ya chakula cha mchana ndani ya Meli ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’. Chini meli hiyo.

tgnp mtandao yafungua rasmi mafunzo ya sikutatu kwa wanawake wanaofanya biashara mipakani


TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia GTI na AWDF wameandaa mafunzo ya siku tatu kwa wafanya biashara wanawake wa mipakani lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanawake hawa wa kuingiza maswala ya jinsia katika biashara zao.
Mafunzo hayo yamewaleta pamoja zaidi ya washiriki 35 wakiwemo Maafisa wa serikali kutoka mipaka tofauti tofauti, Asasi za kiraia ili kuwajengea uwezo wa kuzifahamu haki zao na kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wafanya biashara wanawake wa mipakani katika biashara zao.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtadao Bi. Lilian Liundi alisema kuwa wameamua kuwapa wafanyabiashara wa mipakani elimu hiyo ili waweze kufahamu kanuni mbalimbali za Afrika Mashariki na namna ya kuboresha huduma zao ili kuweza kuyafikia masoko kwa urahisi kuanzia ngazi ya kikanda na kufikia kimataifa.

Aliongezea kwa kusema kuwa utafiti uliofanywa na Kituo cha Sera za Biashara Afrika unaonyesha kuwa biashara  imatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 60 ya wanawake, na katika biashara zifanyikazo katika nchi za jangwa la Sahara, ambapo asilimia kati ya 70 na 80 ya wanawake wamejikita zaidi katika biashara isiyo rasmi na utafiti wa UN Woman unaonyesha zaidi ya asilimia 74 ya wafanyabiashara za mipakani katika nchi za maziwa makuu ni wanawake.

Mkurugenzi huyo aliendelea kwa kusema kuwa wanawake wanaofanya biashara mipakani wanakumbana na changamoto nyingi ikiwemo usawa katika mgawanyo wa kipato na maamuzi juu ya rasilimali katika kufikia zana za uzalishaji kama vile mitaji, ardhi na teknolojia sahihi na taarifa pamoja na elimu ya mafunzo, vilevile ukatili wa kijinsia ikiwemo rushwa ya ngono na nyingine nyingi.
Lakini pia pamoja na nchi zetu kuridhia mikataba mbalimbali ya kitaifa, kimataifa na ya kikanda ya kuendeleza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kama mkataba wa Umoja wa kimataifa wa mwaka 1979, mpango mkakati wa Beijing wa mwaka 1995, Itifaki ya Maputo ya mwaka 1997 na mkataba wa jinsia na maendeleo wa ukanda wa SADC 1998.

Aidha bi. Lilian liundi alisema licha ya juhudi hizo zote lakini bado hakuna muungano kati ya biashara na sera za jinsia kwani mikataba muhimu ya biashara bado inaupofu mkubwa wa kijinsia, kwa kiasi cha kushindwa kuzingatia mahitaji muhimu ya wanawake, lakini pia utekelezaji hafifu wa mikataba na kutokuwepo kwa taarifa mbalimbali za fursa za biashara hii imewaongezea vikwazo wanawake wanaofanya biashara isiyo rasmi katika mipaka na kwa wajasiliamali wadogo kwa ujumla kuweza kukuza biashara zao.

Lakini pia serikali za nchi za afrika mashariki zilitakiwa kukaa chini na kuunda sera na mipango itakayowasaidia wafanyabiashara hawa wadogo wa mipakani kwa kuwaondolea kodi kandamizi ili na wao waje kuwa wafanyabiashara wakubwa kwa kuwawekea mikakati madubuti, kwani wafanya biashara hawa wakiwezeshwa wanaweza kuwa wakubwa na kuchangia vizuri pato la taifa.
Na mwisho alimalizia kwa kusema kuwa changamoto hizi zinahitaji sera kufanyiwa maboresho ili kuunga mkono juhudi za wanawake na kuwapa ujasiri wanawake wa kuimarisha  biashara zao, lakini pia maboresho hayo yanatakiwa kulenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika biashara za mipakani kwa kuboresha na kurahisisha mchakato wa kufanya biashara mipakani.

Inatambulika kuwa wanawake hurudisha asilimia kubwa ya pato lao kwa familia na jamii zao, hivyo juhudi za makusudi zinahitajika katika kuwainua kiuchumi wanawake hawa na kwa nchi kama za afrika mashariki zinahitajika kuhakikisha kuwa wanawake wanapata haki na fursa sawa kama wanaume ili kupunguza pengo la kijinsia, wanawake wanatakiwa kutoa michango yao katika maendeleo ya jamii zao.