MILLION 200 KUTUMIKA KUBORESHA KITUO CHA AFYA MERERANI


2



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Genesta Mhagama(katikati) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(tatu kulia), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(tatu kushoto) pamoja na viongozi wengine baada ya uzinduzi wa namba maalumu ya kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Genesta Mhagama amemkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jaffo Tsh mil 200,000 kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha Afya Mererani ikiwa ni ahadi ya Rais Dr.John Magufuli aliyoitoa wakati wa ziara yake Mkoani hapo mwezi uliopita.
Ujenzi wa Kituo hicho ambao utaboresha huduma za mama na mtoto pia ni maalumu kwa ajili ya kusaidiazaidi katika kutoa huduma kwa watu walioathirika na virusi vya ukimwi katika Wilaya ya Simanjiro.
Ikiwa ni miongoni mwa Wilaya zilizoathirika zaidi na virus vya Ukimwi haswa katika eneo la mererani imeonekana inahitaji msaada wa haraka ili kudhibiti au kupunguza kabisa tatizo hilo katika jamii ya eneo hilo.
Fedha hizo zimetoka katika mfuko wa udhamini wa udhibiti wa Ukimwi ambao ulizinduliwa mwishoni mwa mwaka jana na kuanza kazi rasmi ya kukusanya fedha kutoka katika vyanzo vya ndani kusaidia katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Akipokea Hundi hiyo Waziri wa Tamisemi Mhe. Selemani Jaffo kabla ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Joel Bendera amesema umefika wakati ambapo jamii ya watanzania wanapaswa kuunga mkono jitihada hizi ili kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Wakati huo huo Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imezindua rasmi namba maalum ya kuchangia Mfuko huo wa udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.
Katika uzinduzi huo ambapo mgeni Rasmi alikua Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Mhe. Genesta Mhagama alitaja namba ya uchangiaji wa mfuko huo kuwa 0684909090 na kwamba kila mwananchi anahimizwa kuchangia Fedha ili fedha itakayopatikana isaidie watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
Katika hatua Nyingine Waziri Mhagama alimkabidhi hundi ya Tsh. Milioni 660 kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kwa ajili ya kununua dawa aina ya Contrimaxozole za watu wanaoishi na VVU.
Fedha zote hizi zimetoka katika Mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.

NIMEHATARISHA MAISHA YENU KUTOKANA NA UZALENDO WE DR JOHN POMBE MAGUFULI

maki (16)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia baada ya kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 20Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewatunuku vyeti wajumbe wa Kamati za Madini leo Ikulu jijini Dar es Salaam ikiwa ni shukrani kwa kazi ya kizalendo waliyoifanya.Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Magufuli amesema kuwa watu hao wamefanya kazi kubwa na ya kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya watanzania hivyo wanastahili pongezi.
“Ninashukuru sana kwa kweli mmetengeneza ukurasa wa pekee kwani kazi mliyoifanya ni ya kujitoa sadaka,”alisema Rais Magufuli.Ameongeza kuwa watanzania wengi wanaunga mkono juhudi hizi za kulinda raslimali za taifa licha ya kuwepo watu wachache wanaobeza jitihada hizo na kusema hao inabidi wapuuzwe.Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa wameonyesha uzalendo kwa taifa ambalo lina raslimali nyingi lakini lilikuwa halifaidiki nazo bali zilikuwa zikiwafaidisha watu wachache.Rais amesema kuwa katika suala la kutetea na kulinda raslimali za nchi hasa madini, hakuna hata mahakama ambayo ingeinyima Serikali ya Tanzania ushindi kwani unyonyaji uliokuwa ukifanyika ulikuwa wa wazi, hivyo ameipongeza Kamati ya majadiliano chini ya Mwenyekiti wake, Prof. Paramagamba Kabudi.Amewataka watanzania kuwa na moyo wa kizalendo kwa kujali na kulinda raslimali za nchi bila kuangalia manufaa yao binafsi.Ningekuwa na ubinafsi mii ningekeuwa tajiri sana kwani nimefanya kazi katika Wizara ya Ujenzi kwa miaka 16, hivyo ningetaka kujitajirisha ningeweza, lakini hivyo vyote vya nini,” aliuliza Rais Magufuli.Katika makubaliano kati ya Tanzania na Barrick Gold Company Limited, mgawanyo wa faida itokanayo na madini utakuwa 50 kwa 50, jambo ambalo halifanyiki katika nchi yoyote ya Kiafrika, aliongeza Rais Magufuli.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya majadiliano upande wa Tanzania, Prof. Paramagamba Kabudi amesema kuwa Rais Magufuli anapaswa kupongezwa kwa msimamo wake katika suala zima la usimamizi wa raslimali za nchi hasa madini.
Prof. Kabudi amenukuu magazeti ya Zambia jinsi yalivyompongeza Rais Magufuli kwa hatua hiyo. Amesema kuwa hakika nabii hakubaliki kwao, nje ya nchi wanampongeza Rais wakati baadhi ya watanzania wanabeza jitihada hizo.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amempongeza Rais magufuli kwa hatua anazozichukua katika kulinda raslimali za nchi na kuwataka wapinzani wenzie kumuuunga mkono.
“Mhe. Rais shikilia hapo hapo ili raslimali zetu ziweze kulindwa na kutunufaisha watanzania wote,”alisema Prof. Lipumba.
Baadhi ya waliotunukiwa vyeti hivyo ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Prof. Paramagamba Kabudi, Prof. Abdulkadir Mruma, Prof. Nehemiah Ossolo, James Dotto, Dkt. Yamungu Kayandabila, Prof. Lwoga, Andrew Massawe, Prof. Rwezaula Ikingula, Dr. Ambrose Joseph na Prof. Longinus Lutasitara.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mawaziri, Viongozi wa Dini, Viongozi wa vyama vya Siasa, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,Wanahabari, na wageni wengine ambao walionyesha kufurahishwa na hatua za Serikali ya Awamu ya Tano katika kulinda raslimali za nchi.

DAKTARI ABAINI KANUMBA ALIKUWA NA UVIMBE KICHWANI



Daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa ya binadamu na vifo vyenye kutia shaka, Innocent Mosha kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ameieleza Mahakama Kuu alichobaini baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wa msanii wa fani ya uigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba.

Dk Mosha ambaye ni shahidi wa nne wa upande wa mashtaka katika kesi ya kuua bila ya kukusudia inayomkabili msanii wa fani hiyo, Elizabeth Michael maarufu Lulu amesema walipofungua fuvu walibaini ubongo wa Kanumba ulikuwa umevimba.

Lulu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Katika ushahidi wake leo Jumatatu Oktoba 23,2017, Dk Mosha akiongozwa na Wakili wa Serikali, Faraja George mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Samu Rumanyika ameeleza akiwa kazini alipewa maagizo kuwa anatakiwa kuufanyia uchunguzi mwili uliokuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili.

Shahidi huyo amesema katika uchunguzi wa mwili wa Kanumba alibaini kuwepo uvimbe sehemu ya nyuma kwenye ubongo na walipofungua fuvu walibaini ubongo ulikuwa umevimba.

Dk Mosha alipoulizwa na wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala juu ya sampuli walizopeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu hali ya kilevi katika mwili wa Kanumba, amesema hakuwahi kufahamu matokeo ya uchunguzi.

Pia, amesema hafahamu kama Kanumba alijigonga ukutani kwa kuwa hakuwepo eneo la tukio.

HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA SARATANI PAMOJA NA MATIBABU YA AWALI SASA BURE KWENYE HOSPTALI ZA SERIKALI

Huduma za Uchunguzi wa Saratani kutolewa bila malipo

Waganga wa vituo vyote vya Serikali hapa nchini wametakiwa kuhakikisha huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti zinatolewa bila malipo yeyote sambamba na matibabu ya awali.
Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kuamua kuboresha huduma hizo kwa kununua mashine 100 za tiba mgando,mashine 9 za upasuaji mdogo ambazo zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake pamoja na mitungi 173 ya gesi ya carbon dioxide zitakazowezesha mashine hizo kufanya kazi.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,wazee na Watoto Ummy Mwalim amebainisha hayo jijini Dar es salaam ambapo amevitaka vituo vya umma nchini kuhakikisha vinatenga siku maalum katika kila mwezi ili kuweza kuwahamasisha wanawake waweze kujitokeza kupata huduma hizo.

"natoa rai kwa wananchi hasa wanawake wenzangu kuhudhuria vituoni ili kuweza kupata huduma za uchunguzi mapema"alisema Ummy.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje,Serikali ya awamu ya tano imeamua kuboresha huduma za afya hususani upande wa saratani ili kuweza kuhakikisha wagonjwa hao wanatibiwa hapa nchini.

Ifahamike kuwa takribani wagonjwa wapya elfu 50 kila mwaka wanagundulika kuwa na saratani ,na idadi hii inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI ATEMBELEA KITUO CHA UZALISHAJI UMEME KIGAMBONI



 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (wapili kulia), akifurahia jambo na wahandisi na mafundi wa TANESCO alipotembela  mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2017.
 Naibu Waziri, Mgalu, (katikati), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANSECO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), na Naibu Mkurugenzi Mtendjai wa TANESCO, (anayeshughulikia usafirishaji umeme), Mhandisi, Kahitwa Bishaija, (kushoto), wakiwasili kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kigamboni jijini Dar es Salaam Oktoba 20, 2017.
 Wahandisi wa TNESCO wakimalizia kazi ya kufunga mitambo kwenye kituo cha Kigamboni.
NAIBU Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, ameendelea na ziara yake ya kujifunza kwa kukagua miradi mingine miwili mmoja wa ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme Kimbiji na kingine cha kupoza umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2017.
Alhamisi Oktoba 19, 2017, Mhe. Mgalu alifanya ziara kama hiyo kwa kutembelea vituo viwili vya kupoza umeme vya Mbagala na Kurasini wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiwa KIgamboni, Mheshimiwa Naibu waziri ambaye alifuatana na Katibu Tawala wa Wilaya mpya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na viongozi wengine wa juu wa Shirika hilo, alianza kwa kukagua kituo cha Kigamboni ambapo aliwakuta mafundi wa TANESCO wakimalizia kufunga mitambo kwenye kituo hicho.
Aidha Naibu waziri alimalizia ziara yake kwa kutembelea eneo la ujenzi wa kituo kipya cha Kimbiji ambapo kazi ya kusafisha eneo la ujenzi nayo imekamilika na kinachosubiriwa ni kuwasili kwa vifaa ili ujenzi uanze.
Mheshimiwa Mgalu alisema kutokana na ongezeko kubwa la watumiaji wa umeme, vituo hivyo vitasaidia sana kuboresha huduma ya upatikanaji umeme hususan katika kipindi hiki ambacho serikali ya awamu ya tano imejielekeza kujenga uchumi wa viwanda na hitajio kubwa katika utekelezaji wa mpango huo ni upatikanaji wa umeme wa uhakika.
“Niwashukuru tu kwa ksuema, ziara yangu hii ni ya kwanza kwenye eneo hiki tangu niteuliwe na nimeona nije ili nijionee jitihada hizi za kuboresha hali ya umeme wilayani Kigamboni ambapo kuna uhitaji mkubwa wa umeme ,kutokana na ongezeko kubwa la watu.” Alisema.
Akieleza zaidi Mheshimiwa Mgalu alihimiza Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ambalo kwa niaba ya serikali ndilo linatekeleza mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi ili hatimaye wananchi wapate huduma ya umeme katika hali bora zaidi.
Aidha Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, Aliishukuru serikali kwa kuleta mradi huo katika wilaya hiyo na kusema serikali wilayani Kigamboni itatoa kila aina ya msada ili kuhakikisha mradi huo mkubwa unakamilika.
“Hii ni wilaya mpya ni jambo la kushukuru kuwa katika kipindi kifupi wilaya inaletewa mradi mpya wa kuboresha umeme kwa kweli wananchi wana matarajio makubwa na mradi huu na sisi tumefarijika sana.” Alisema Katibu Tawala wa wilaya ya Kigamboni.


 Naibu waziri akipatiwa maelezo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, Mhandisi Kahitwa Bishaija, (wapili kushoto). Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Naibu waziri akipatiwa maelezo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, Mhandisi Kahitwa Bishaija, (wapili kushoto). Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (kushoto), akifurahia jambo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, wakati wakitoka ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo kuanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa vituo vya umeme vya Kigamboni na Kimbiji.
 Meneja Mwandamizi wa TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (kulia), akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa Nihstai, Mhe. Subira Mgalu, (wakwanza kushoto) kwenye eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme cha Kimbiji, wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, Oktoba 20, 2017.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula, (kulia), akimuonyesha mchoro wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kigamboni, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (katikati), na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Bi. Rachel Mhando, wakati Mhe. Mgalu alipotembekea kituo hicho leo.

MAKONDA AKABITHI GARI ZENYE MWONEKANO MPYA KWA AJILI YA DORIA ZA MKOA WA DAR-ES-SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Magari ya kisasa 18 kati ya 26 yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa Mabovu  kwa ajili ya kufufuliwa upya.

Magari hayo yalipelekwa Kilimanjaro kutokana na ubovu lakini  sasa yanarejea Dar es Salaam yakiwa Mazima na muonekano mpya kama wa Magari ya umoja wa mataifa (UN) ambapo yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari 11 wakiwa wamekaa na silaha zao.
Akikabidhi Magari hayo kwa Jeshi la Polisi RC Makonda amesema yataenda kuhudumia wananchi kwa kuimarisha Ulinzi na Usalama jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kilichomgusa kuboresha Jeshi la Polisi ni Baada ya kuona Askari wakifanya kazi katika mazingira magumu na wakati mwingine kuvamiwa na majambazi kisha kuuawa na kuporwa Silaha.
Aidha  RC Makonda ameishukuru kampuni ya Rajinder Motors Ltd (RSA) kwa kumuahidi kutengeneza Magari 56 ya Polisi Dar es Salaam bila kutumia fedha za serikali (Bure).
RC Makonda ametumia Makabidhiano hayo kutuma salamu kwa Majambazi, Vibaka na wale wenye nia ya kuvuruga Amani na Usalama kuwa kiama chao kimefika.
Amesema alipotangaza mpango wa kufufua Magari yaliyokufa wapo waliombeza lakini sasa wanajionea Magari yakiwa Mapya.
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar ea Salaam Lazaro Mambosasa na viongozi wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo wamempongeza  RC Makonda kwa ubunifu mkubwa alionao.