HII HAPA KAULI YA KAMANDA MAMBOSASA JUU YA UVAAJI VIMINI DAR


Tokeo la picha la KAMANDA MAMBOSASA
Hatua hiyo inakuja baada ya gazeti la kila siku la Nipashe January 17 (leo) kutoka na kichwa cha habari; Polisi yakamata wavaa vimini, kunyoa viduku.
Akizungumza Dar es Salaam Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema taarifa hiyo haina ukweli wowote kwani mwandishi ameandika kitu ambacho hakukisema.
“Nilitaka nitoe ufafanuzi nikikanusha haya ambayo yameandikwa hayakusemwa na Jeshi la Polisi, anayasema mwenyewe mwandishi kwa interest yake na sana alichokuwa anatafuta ni umaarufu wa stori,” amesema.
“Ninamtaka sasa arudi kwa watanzania aombe radhi ili kuondosha usumbufu uliojitokeza, nimepigiwa simu kuanzia jana toka maeneo mbali mbali kwa jambo ambalo kimsingi halijafanywa na Jeshi la Polisi,” amesisitiza.

WCF YAWANOA WAAMUZI,WASULUHISHI NA MAKATIBU KUTOKA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZU(CMA)


 Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, (kushboto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, (wkawanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Shanes Nungu, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Morogoro leo Januari 17, 2018. Bw. Kalonga alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Eric Shitindi.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga,kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Eric Shitindi, akifungua mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba yake.

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), umejipanga vema kuendelea kutoa huduma bora kwa wadau, hususan katika kipindi hiki ambacho Mfuko unategemea ongezeko kubwa la waajiri na wafanyakazi, kutokana na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kujenga uchumi wa viwanda, ambao utaongeza ajira.
Hayo yamesemwa leo Januari 17, 2018 mjini Morogoro na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), ili kuongeza ujuzi kwenye utekelezaji wa majukumu ya Tume.

“Katika jambo hili la kujenga uchumi wa viwanda,  makampuni mengi yataanzishwa, kutakuwa na waajiri wengi, ongezeko la wafanyakazi, kwa hivyo unategemea kwamba hitajio la utoaji huduma za Mfuko kwa wadau  litaongezeka na Mfuko umekuja wakati muafaka na tupo kwa ajili ya kuwahudumia wale wote watakaopatwa na majanga mahala pa kazi lakini pia kuelimisha.” Alisema Bw. Mshomba.

Bw. Mshomba  alisema, kuanzia Julai, 2016 Mfuko ulianza kupokea madai ya Fidia yanayotokana na kuumia au kuugua mahali pa kazi.

“Jambo hili si rahisi kwa sababu ndio linaanza kwa hivyo tunahitaji ushirikiano wa karibu sana kutoka kwa wadau mbalimbali mkiwemo ninyi CMA, na katika hilo ushirikiano tu hautoshi Mfuko umekuwa ukitoa elimu ili kuwawezesha watu  wajue Mfuko umeanzishwa kwa sababu gani, kazi zake, lakini pia kujua taratibu za kudai fidia pale mfanyakazi anapopatwa na majanga ya kuumia au kuugua wakati akitekeleza wajibu wake wa kikazi.” Aliongeza Bw. Mshomba.

“Ndio maana leo hii tunao wataalamu wetu watakaotoa mada mbalimbali zikiwemo, Sheria za Fidia, Namna Fidia inavyolipwa lakini shughuli za Mfuko.” Alibainisha Mkurugenzi Mkuu Bw. Mshomba.

Aidha aliishukuru Tume kwa kuwashirikisha WCF ili kuwaelimisha wafanyakazi wake kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.

“Ni muhimu kwetu sisi kuwaelimisha wadau kuhusu shughulim zetu na ndio maana huwa tuko tayari wadau wetu wanapotualika ili kutoa elimu hiyo.” Alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa ……..kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Bw. Eric F. Shitindi amewahimiza washiriki wa kuzingatia elimu watakayoipata kwenye mafunzo hayo ili hatimaye watekeleze ipasavyo malengo ya serikali ya awamu ya nne ya kujenga uchumi wa kati ifikapo mwak 2025.

“Ni matarajio yetu kwamba Tume na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, mnao wajibu mkubwa sana katika kufanikisha azma hiyo ya serikali kama nyinyi mtatekeleza wajibu wenu.” Alisema.
Baadhi ya washiriki.
Baadhi ya washiriki.
Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Edrisa Mavura, akitoa hotuba yake.
Maafisa wa CMA wakiteta jambo.
Bw. Mshomba, (kulia), na Bw.Nungu, wakijadili jambo.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, akikaribishwa na Wakurugenzi wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kulia) na wa CMA, Bw.Shanes Nungu, alipofika kufungua mafunzo hayo
 Bw. Mshomba akijibu baadhi ya maswali ya washiriki kuhusu shughuli za Mfuko.
Baadhi ya washirtiki wakifuatilia mafunzo.
Kamishna wa Tume, Bi.Suzanne Ndomba, (kulia), akizungumza kwenye mafunzo hayo. Wengine ni Makamishna wenzake, kutoka kushoto, Bw.Kibwana Njaa, Bw.Jones Majura na Bw.Jaffary Ally Omar.
Picha ya pamoja.
Bw. Mashomba akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Sheria wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar.
Washiriki wakipitia vipeperushi vya WCF.

GAIRO:YATIMA WASAIDIWA VIFAA VYA SHULE


Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwaasa watoto yatima wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo. Kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walioambatana naye. Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha akitoa salamu kwa watoto yatima.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akigawa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Bethel kilichopo wilayani humo.
Watoto wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo wakiwa wamejipanga mstari kupokea zawadi.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye nguo ya njano), Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha (wa tatu toka kulia) pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Bethel wa Gairo.


Katika kujali makundi yenye changamoto za maisha hasa watoto wadogo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe amegawa sare za shule na madaftari kwa watoto yatima 150 kituo cha Bethel Wilayani Gairo kinachosimamiwa na Mchungaji Chacha.

Hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa ulifanyika mapema wiki hii, ambapo Mhe. Mchembe amesema kuwa huo ni utamaduni aliojiwekea kila mwanzo  wa mwaka wa kuwakumbuka watoto yatima na wale waishi katika mazingira magumu.

"Nawakumbusha wananchi kujenga utamaduni wa kusaidiana watu wasiojiweza ili muweze kupata baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, unajua unapokuwa nacho ukatoa kidogo unabarikiwa zaidi," alisema Mhe. Mchembe.

Mhe.  Mchembe aliwakumbusha watoto hao kuzingatia masomo kwani Serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Magufuli inatoa elimu bure hivyo hakuna mtoto wa masikini atakayeshindwa kusoma. 

Katika kukua kwao wamtangulize Mungu naye ataendelea kuwabariki na kuwatoa katika hali ya kuhisi unyonge wa kukosa wazazi.

Mwisho aliwaasa waalimu kuwa na moyo wa upendo kwa watoto yatima. Pia kuweka karibu hasa watoto wa kike kuwaepusha na mimba za utotoni.

ELIMU YATOLEWA KWA VIONGOZI WA DINI DHIDI YA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI


Mwenyekiti wa Mtandao wa kutokomeza Ndoa za Utotoni Bi. Valeria Msoka akisisitiza jambo katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini zote lengo likiwa ni kujadili nafasi yao katika kupinga ndoa za utotoni.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini mkutano mapema leo jijini Dar es salaam.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Hadi Mussa Salim akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini mbalimbali na kimila katika kujadili nafasi yao katika kupinga ndoa za utotoni.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Hadi Mussa Salim akichangia mada mbele ya wageni walioudhuria mkutano huo mapema leo jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi mtendaji wa RICPT ambaye pia ni muwakilishi wa dini ya kikristo Rev. Canon Thomas Godda akitoa ufafanuzi juu ya siku hiyo, na nini nafasi yao kama viongozi wa dini katika kupinga ndoa za utotoni na ushiriki wao katika kuleta mabadiliko ya sheria ya ndoa inayotumika hivi sasa.
Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bw. Godfrey Mpandikizi akitoa presentetion mbele ya wageni waliudhuria mkutano wa kujadili kushinikiza viongozi wa dini na wakimila kupambana ili kuweza kubadilishwa kwa sheria ya ndoa iliyopo hivi sasa.

  • Viongozi wa dini zote hapa nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuishinikiza serikali kukubali kubadilisha sheria ndoa ya mwaka 1971.

  • Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es salaam katika semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni(TECMN) iliyowakutanisha viongozi wa dini zote mbili pamoja na viongozi wa kimila kutoka mikoa mbalimbali.

  • Akiongea katika semina hiyo Bi. Valeria Msoka alisema kuwa viongozi wa dini ni watu walio karibu sana na jamii, hivyo wanazijua vizuri changamoto wanazokutana nazo wananchi ikiwemo ndoa za utotoni na wanatakiwa wasikae kimya kwani wao ndio msaada pekee kwa jamii yao.

  • Lakini pia viongozi wa dini ni watu wanaopewa nafasi nzuri na kuheshimiwa kwa kiasi kikubwa na serikali hivyo watumie muda huo kuiamba serikali kuwa sheria hii ya mwaka 1971 inayotoa ruhusa kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 haifai na inatakiwa kubadilishwa.

  • Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa lengo la kukutana na viongozi wa dini ni kujaribu kushauriana na kuona nini watakifanya kushinikiza kubadilishwa kwa sheria hiyo inayomnyima haki za zake za msingi mtoto wa kike.

  • Akiongea kwa niaba ya dini ya kiislamu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Al Hadi Mussa Salim alisema kuwa dini zetu zimekuja kwa lengo kuu la kuwasaidia wanadamu na hasa wanawake ambao walikuwa wakinyanyaswa na kunyimwa haki zao katika jamii hususani kwa upande wa ndoa.

  • Aidha Sheikh Mkuu wa Mkoa alisema kuwa cha muhimu tuungane kwa pamoja Waislamu, Wakristo, viongozi wa Kimila pamoja na serikali katika mitazamo na mwazo yetu ili tujue kuwa mtoto wa kike ni nani na haki zake ni zipi anazostahili kupata, kwa njia hiyo tunaweza kufanikiwa kulitokomeza tatizo hili la ndoa za utotoni.

  • Sheikh huyo aliendelea kusema kuwa tusipokuwa na sauti moja hatutaweza kama viongozi wa dini tukisema ndoa za utotoni zikome lakini serikali ikipinga atuwezi kuondoa tatizo hili, cha msingi ni kukubaliana makundi yote kuwa hatuzitaki ndoa za utotoni katika jamii yetu serikali ikubali viongozi wa kimila wakubali, wananchi wakubali na makundi yote yawe tayari kupambana vita hivi.

  • Kwa upande wake kiongozi aliwakilisha dini ya kikristo Rev. Canon Thomas Godda alisema kuwa zama zimebadilika kwani mwanzo sharia hii ilivyotungwa na ilipitishwa kwa urahisi kwa kuwa watu hawakuwa na uelewa, ila kwa sasa watu wameelimika na inapaswa kupingwa kwa nguvu zote swala hili.

  • Bw. Thomas aliendelea kusema kuwa ndoa inayokubalika hata katika vitabu vya dini ni ya watu wazima wote ambao umri wao ni kuanzia miaka 18 na kuendelea, hivyo basi wao kama viongozi wa dini watajaribu kufanya ushawishi kwa kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha swala hili linatokomezwa kabisa na sheria inabadilishwa.

SILAHA ZA KIVITA ZAKAMATWA SHINYANGA


Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK-47 iliyotupwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa wanataka kuvamia kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd kilichopo Nhelegani katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamis Januari 18,2018 Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema walikamata silaha hiyo usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano eneo la Tinde wakati majambazi hao wanafuatiliwa na polisi ndipo wakaamua kutupa bunduki hiyo.

“Silaha hii aina ya AK-47 yenye namba 18116428 ilikuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwa na risasi 25 ndani ya magazine yake na risasi zingine 8,zikiwa kwenye mfuko mdogo wa nailoni”,alieleza Kamanda Haule.

“Majambazi wawili pia walitelekeza pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC 856 BPF,mafuta ya cherehani ya kulainishia silaha,tochi mbili na koti zito”,aliongeza.

Alisema jeshi la polisi lilipata taarifa za majambazi hao kutaka kuvamia kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wa China tangu tarehe 6.01.2018 kisha kuanza kuwafuatilia na kubaini kuwa baadhi yao ni wakazi wa Kahama na Ushirombo ambapo amewataka kujisalimisha polisi.

Bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyokuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyotelekezwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Wachina mjini Shinyanga- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Silaha na vifaa vilivyotelekezwa na majambazi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha skafu iliyotumika kufunga bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Jielong
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha silaha aina ya AK-47 yenye namba 18116428 na mafuta ya kulainishia silaha yaliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Jielong
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule  akionesha risasi zilizotelekezwa na majambazi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule  akionesha  pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC 856 BPF iliyotelekezwa na majambazi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule  akionesha koti zito lililotelekezwa na majambazi
Jengo la ofisi za kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd kilichopo Nhelegani katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.
Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania),bwana Liu Buhua akilishukuru jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kuzuia uhalifu uliotaka kufanywa na majambazi
Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd ,bwana Liu Buhua akilishukuru na kulipongeza jeshi la polisi kuzuia uhalifu katika kiwanda hicho

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akiwa katika  kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd.

VYAMA VYA SIASA MAREKANI NJIA PANDA



  picha ya Bunge la Marekani.
Huku siku ya mwisho ikiwa imekaribia hapo Ijumaa usiku kabla ya kuwa na uwezekano wa kufungwa kwa shughuli za serikali ya Marekani wabunge wa vyama vya democrat na republican wako njia panda kukubaliana ili shughuli za serikali ziendelee bila ya kuweka hatarini mambo yalio na kipaumbele kwa vyama vyao.
Wademokrat wanataka muswaada wa kujitegemea ili serikali iweze kuendelea kufanya kazi wakati kwa upande wa chama cha republican wanataka muswaada uliounganishwa na usalama wa mipaka na mabadiliko ya uhamiaji.
Warepublikan waliwatumia wademokrat muswaada ambao hauna sera ya kuwalinda wahamiaji laki 7 wasio na vibali walioletwa nchini na wazazi wao wakiwa watoto wadogo lakini inawapa nafasi wademokrat hatua ya kipaumbele cha juu ya kurudisha tena bima ya afya kwa watoto kwa miaka sita. (CHIP).

KAULI YA TRUMP YAFANANISHWA NA UDIKTETA ASEMA SENETA

Seneta afananisha kauli ya Trump na udikteta


Seneta John McCain
Maseneta wawili wa chama cha Republikan Jumatano wamemshutumu Rais Donald Trump kwa kuendelea kuchukizwa na habari zinazokosoa uraisi wake, wakisema kufanya hivyo kunakandamiza misingi ya kidemokrasia katika jamii, uhuru na uwazi wa vyombo vya habari.
Katika maoni yalioandikwa katika gazeti la Washington Post, Seneta wa Republikan kutoka Arizona John McCain amesema kitendo cha Trump kujirudia katika madai ya “habari feki” zinapokuja habari ambazo Trump hazipendi hutumiwa na viongozi wa nchi nyingine kama ni sababu wakati wanavinyamazisha vyombo vya habari, “ambavyo ndio moja ya nguzo za demokrasia.”
Huko katika Bunge la Marekani, Seneta mwengine wa Arizona, Jeff Flake, ambaye amekuwa anamkosoa mara kwa mara Trump, amesema katika hotuba yake kwenye Baraza la Seneti kuwa kitendo cha Trump kukebehi vyombo vya habari ni sawa na kauli za siasa zinazotolewa na madikteta.
“Sio tu mwaka uliopita umeshuhudia rais wa Marekani akitumia lugha ya madikteta kuelezea vyombo huru vya habari, lakini inaokena hivi sasa, amegeuka kuwahamasisha madikteta na watawala wanaotumia mabavu kwa matamko yake. Hili ni jambo la makosa. Hatuko katika zama za habari feki kama anavyoeleza ((Rais wa Syria)) Bashar Assad. Sisi tuko, ukweli ulivyo, katika zama ambazoutashi wa kidikteta unajirudia tena kwa kuwashambulia watu huru na jamii huru kila mahali."

VIONGOZO WA AU WATETA KUHUSU KAULI YA TRUMP



Balozi Arikana Chihombori-Quao,
Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani, Arikana Chihombori-Quao, ameiambia VOA kuwa viongozi wa Afrika wamekasirishwa na tamko la udhalilishaji juu ya wahamiaji kutoka bara la Afrika na Haiti linalodaiwa kutolewa na Rais Donald Trump.
Amesema anategemea hatua zaidi rasmi na juhudi za kidiplomasia kupinga hilo, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa mabalozi wa Afrika kususia kuhudhuria hotuba ya rais ya hali ya taifa la Marekani kwenye Bunge la Marekani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Heather Nauert amesema Marekani ina uhusiano imara na Waafrika na Haiti, uhusiano imara zaidi kuliko maoni yoyote, ameripoti mwandishi wa VOA.
Wakati hisia hasi zikiendelea kutolewa nchini Marekani na nchi za nje kutokana na kauli ambayo vyanzo kadhaa vimesema kuwa rais alitoa tamko juu ya aina ya wahamiaji anaopendelea waingie nchini Marekani, rais aliulizwa na mwandishi iwapo anataka wahamiaji zaidi watoke kutoka Norway.
Trump alijibu: “Nataka watoke kote ulimwenguni.
Msemaji wa Ikulu ya White House Sarah Huckabee Sanders amekiri kuwa rais alitumia lugha kali wakati wa mkutano wake na wabunge juu ya suala la wahamiaji, na kusema kuwa ni sehemu ya wito wake.
“Nafikiri kuwa hiyo ni moja ya sababu watu wa Marekani wanampenda Trump, sababu mojawapo iliyopelekea kushinda uchaguzi na anaendelea kuwepo katika ofisi yake ya Oval ya ikulu ya White House. Hii ni kwa sababu yeye sio mtu anayetegemea kuandikiwa kila kitu. Yeye ni mtu ambaye anaeleza vitu vile vilivyo mara nyingi, na mara nyingine anatumia lugha kali sana,” amesema Sanders.
Matokeo ya kauli hiyo yenye utata anayodaiwa kuitoa Trump, Botswana, Ghana, Haiti, Namibia, Senegal na Umoja wa Afrika wamepeleka malalamiko yao rasmi ya kidiplomasia kupiga udhalilishaji huo.
Balozi wa Umoja wa Afrika nchini Marekani, Arikana Chihombori-Quao ameiambia VOA kuwa matamko hayo hasi juu ya Afrika na Uongozi wa Trump wa sera ya “Marekani Kwanza” ni kimbingamizi kwa uhusiano wa muda mrefu wa karibu kati ya Marekani na bara la Afrika.

TAFITI:NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI BADO HAZINA UHURU KAMILI



Reipoti ya Freedom House 2017.
Haki za kidemokrasia zimezidi kuonyesha kutoheshimiwa kaitka eneo la Afrika Mashariki ambapo Kenya, Tanzania na Rwanda zimeshuka viwango katika ripoti mpya juu ya hali ya uhuru duniani (global status of freedom).
Kenya
Uhuru Kenyatta akimaliza kukagua gwaride kabla ya kula kiapu kiwanjani Kasarani Nairobi.
Uhuru Kenyatta akimaliza kukagua gwaride kabla ya kula kiapu kiwanjani Kasarani Nairobi.
Utafiti uliofanywa na taasisi binafsi ya Freedom House lenye makazi yake Washington, ambalo sio la kisiasa wala serikali, linaeleza kasoro zilizojitokeza katika mchakato wa uchaguzi wa urais Kenya.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa uchaguzi ulikuwa na utata, ambao “marudio ya uchaguzi yalioamrishwa na mahakama yalifanyika bila ya kuwepo mageuzi ya msingi, matukio ya vurugu za kisiasa na kususiwa kwa uchaguzi huo na mgombea mkuu wa upinzani, Raila Odinga.
“Mambo haya yanatia dosari ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta, ambapo alidai kupata kura asilimia 98 ya kura zote pamoja na kuwepo mahudhurio ya chini ya wapiga kura,” ripoti hiyo imesema.
Taasisi hiyo imeipa Kenya asilimia 48 kati ya 100 --- ikionyesha demokrasia imeshuka kutoka asilimia 51 vile ilivyokuwa imeripotiwa mwaka 2017. Hali hiyo inaifanya Kenya kuwa kati ya nchi 58 zinazoelezwa kuwa “hazina uhuru kamili.”
Tanzania
Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Taasisi hiyo ya Freedom House pia imeripoti kushuka kwa haki za kidemokrasia nchini Tanzania, ambayo ilikuwa iko juu kidogo kuliko Kenya.
Tanzania, ambayo imepewa asilimia 52 katika ripoti hiyo mpya na asilimia 58 katika utafiti wa mwaka 2017, imewekwa katika kikundi cha nchi “zisizo na uhuru kamili.”
“Serikali ya Rais John Magufuli – ambaye alichukua madaraka mwaka 2015 kama ni mwanachama pekee wa chama tawala nchini – alianzisha ukandamizaji wa wapinzani, kuwafunga wanasiasa wa upinzani, akifunga vyombo vya habari na kuwakamata wananchi ambao wanatoa maoni yao ya kukosoa katika mitandao ya kijamii,” utafiti huo wa mwaka 2018 umeeleza.
Uganda
Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni
Uganda imeonyesha mabadiliko kwa kupanda daraja kutoka “kutokuwepo uhuru kabisa” kwenda “zisizo na uhuru kamili” japokuwa hivi sasa imepewa daraja la asilimia 37 ambayo bado iko chini kuliko Kenya na Tanzania.
Taasisi ya Freedom House inafanya tathmini yake ya uhuru nchini Uganda kwa kigezo cha “kuamka kwa sekta ya habari na utayari wa waandishi wa habari, mitandao ya jamii na wananchi kutoa maoni yao.”
Hata hivyo, ripoti hiyo imeongeza kuwa “hali ya kisiasa imeendelea kuwa kandamizi chini ya utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.
Rwanda
Rais Paul Kagame
Rais Paul Kagame
Rwanda imeorodheshwa kati ya nchi 49 ambazo “haziko huru.” Imepewa asilimia 23 – ambayo imeshuka kidogo kutoka asilimia 25 ambayo ilipata mwaka jana katika ripoti ya Freedom House. Utafiti mpya hautoi maelezo juu ya daraja waliopewa Rwanda.
Nchi nyingine
Burundi, Somalia na Sudan Kusini pia zimeelezwa kuwa “haziko huru” katika ripoti hiyo.
Sudan Kusini imepewa daraja ya pili kutoka chini—pointi mbili--- kati ya nchi 195 ambazo tafiti hiyo ilifanywa na Freedom House. Somalia inaunafuu kidogo, ambapo inanukta saba. Burundi, pia imegubikwa na migogoro ya ndani lakini sio kwa kiwango ambacho Somalia na Sudan Kusini imeathiriwa na migogoro hiyo, imepata daraja ya asilimia 19.