BILIONI MOJA YAWAPONZA POLISI SABA



1. E.4948 CPL Dani Isack Kasala
2. F.1331 CPL Matete Maiga Misana
3. G.1876 PC Japhet Emmanuel Lukiko
4. G.5080 PC Maingu Baithaman Sorrah
5. G.6885 PC Alex Elias Nkali
6. G.7244 PC Timoth Nzumbi Paul
7. H.4060 PC David Kadama Ngelela.

Aidha, kuhusu Afisa SSP: Moris Okinda ambaye alikuwa kiongozi wa askari hao walioomba na kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha, mamlaka yake ya kinidhamu tayari imemsimamisha kazi na tayari amefikishwa mahakamani pamoja na askari hao.
Pamoja na askari hao, pia wamefikishwa mahakamani watuhumiwa wengine wa nne waliokamatwa huko Kigongo feri Wilayani Misungwi wakitorosha madini hayo ya dhahabu kutoka Tanzania kwenda Nchi jirani ya Rwanda.

Watuhumiwa waliokamatwa wakitorosha madini hayo ya dhahabu ni;
1. Sajid Abadalah Hassan, miaka 28, mfanyabiashara wa dhahabu, mkazi wa Ilala Dar es Salaam na Mwanza mtaa wa pamba ‘A’.
2. Kisabo Kija  Mkinda , miaka 55, mfanyabiashara wa dhahabu, mkazi wa mwatulole –Geita
3.Emmanuel Ntemi, miaka 63, dereva, mkazi wa kijiji cha mwatulole –Geita
4. Hassan Sadiq Hassan, miaka 28, Mhindi, Raia wa Pakistani, mkazi wa Mwanza mtaa wa Pamba ‘A’, Mfanyakazi wa duka la kuuza vito.
Kufuatia sakata hili, Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na wanaendelea na uchunguzi wa kina ili tuweze kuwakamata watuhumiwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine katika sakata hili.

No comments: