WAZIRI MHAGAMA ATINGA KIWANDA CHA VIATU.............ATOA AGIZO KWA VITENDAJI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amewataka watendaji wa kiwanda cha Viatu na bidhaa za ngozi cha Karanga Wilaya ya Moshi kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuendana na Soko lililopo nchini.
Ametoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki ili kukagua shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho na kujiridhisha na ubora wa bidhaa zinazozalishwa.

“Niwatake watendaji kuweka mikakati madhubuti ya kuendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa kuzingatia viwango vinavyotatiwa”, Mhagama
Aidha Waziri aliwaasa watendaji wa kiwanda hicho kuendelea kutatua changamoto zinazowazunguka za kimfumo kwa kuzingatia sheria na taratibu za uendeshaji wa kiwanda hicho ili kuendana na ukuaji wa teknolojia na ushindani ulipo.

“Nisingependa kuona kiwanda kinakwama kuzalisha bidhaa zenye ubora, hivyo ni vyema kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji wa kiwanda katika ufanisi wa hali ya juu”,alisisitiza mhagama.
Kiwanda cha viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi kilizinduliwa rasmi Juni 3, 1977 na Rais wa awamu ya kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere.Awali kilikuwa na ubia na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF ambapo baada ya mabadiliko ya kuunganishwa kwa mifuko hiyo , kwa sasa kina ubia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF.

No comments: