ANANIZUSHIA KUGOMBEA HAWAJIAMINI-RC GAMBO

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa hana mpango wa kugombea ubunge Arusha Mjini ila anachofanya sasa ni kutekeleza ahadi za Rais Dkt. John Magufuli za kutatua kero za wananchi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi habari, ambapo amesema kuwa taarifa zinazosambazwa kuwa atagombea ubunge jimbo la Arusha mjini ni za wanasiasa wasiojiamini na wameshindwa kutatua kero za wananchi.
Amesema kuwa baadhi wabunge hawaonekani majimboni na kuwaachia viongozi wa Serikali kufanya kazi zilizopaswa kufanywa na wabunge hao hivyo kuwa na hofu kubwa kuwa wanaweza kupokonywa nafasi zao.
“Kazi ambazo nafanya kwa kushirikiana na wasaidizi wangu wakuu wa wilaya ni kutatua kero na tumeachana na mambo ya kisiasa, sisi tunachapa kazi, huu ni muda wa kazi hatufanyi siasa,”amesema Gambo

wanafunzi watano wapigwa risasi kenya

HABA

wanafunzi watano na mlinzi wa shule wameuawa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi mwenzao, huku wengine 17 wakijeruhiwa katika shule ya sekondari ya Lokichogio iliyopo kaunti ya Turkana, nchini Kenya
Mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina la Abraham mwenye asili ya Sudan Kusini alikwenda shuleni akiwa na wenzake, na kuanza kuwamiminia risasi wanafunzi ambao walikuwepo kwenye shule hiyo, kwa kinachoaminika kuwa ni kulipiza kisasi baada ya kusimamishwa sule kwa utovu wa nidhamu.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanafunzi huyo alifanikiwa kuingia shuleni hapo baada ya kumuua mlinzi na kisha kuingia bwenini, na kufanya shambulio lililopelekea vifo hivyo na kujeruhi wengine.

Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua

Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua
Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation. Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo. 
Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.
Iwapo mtoto wako mchanga au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari. Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:
1. Jaribu kumpa mtoto wako maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema. 
2. Iwapo maji hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. 
3. Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele au fiber. Iwapo mwanao ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple na pea lililopondwa pondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au kufunga choo. 
4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.
5. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumia mafuta ya madini (mineral oil) au dawa za kulainisha choo na za kuharishwa katika kutibu tatizo hilo la kukosa choo la mtoto.
6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirschsprung ugonjwa wa kumee neva katika utumbo, au Cystic Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.
7. Kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng’ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya ng’ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng’ombe. 
8. Mwogeshe au mweke mwanao katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa majini na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata chook wa urahisi. 
N.B Ukosefu wa choo kwa watu wazima baadhi ya wakati huandamana na magonjwa kama vile Arthritis, Appendicitis, Cataract, saratani, shinikizo la damu, Rheumatism na kadhalika lakini kwa watoto huenda tatizo hilo likawa halisababishwi na maradhi hayo.
Utafiti unaonyesha kuwa hakuna uhusiano wowote kuhusu kukosa choo mtoto na kupewa nyongeza ya chuma au Iron Supplement. Hivyo usimkatishe kumpa mwanao chuma iwapo anakosa choo. Kwani chum ni muhimu sana katika kuzuia upungufu wa damu mwilini kwa mtoto wako mdogo.

MAGOLI: Simba SC 1 - Mtibwa Sugar 1

katika hai isiyo ya kawaida huku mtibwa wakiwa wameshajiaminisha kuwa wameshachukua point tatu mchezaji emmanuel okwi awarudisha nyumba wakata miwa hao wa mtibwa baada ya kurudisha goal katika dakika za mwisho za mchezo

IJUE TOFAUTI YA MWANAMKE NA MWANAUME KWENYE MAHUSIANO

Majirani wa Hamisa Mobetto wasimulia jinsi Diamond alivyokua akiingia us...

Dah asikudanganye mtu hasa kwenye swala la kulamba asali kama msemo wa bandu bandu humaliza gogogo ndio ilivyokuwa kwa diamond ambaaye alikuwa anatoroka kwa boss lady kwenda kula asali aliyobakisha kwa hamisa mobbeto huku majirani waishindwa kulala kushuhudia staa huyo akija kwa mobbeto night kali ili asijulikanane na mapaparazi.tembelea kwangu leo blog yangu na pia tembelea page yangu ya faceebook na click follow button ili uwe wakwanza kupata taarifa mara zinapotokea

Cheki Jux Akimpigia Magoti Vanessa Mdee Jukwaani, Waimba Pamoja Tigo Fi...

Moja kati ya vitu vya ajabu sana kufanywa na mastaa hasa wa kibongo ni kumnyenyeka x wako, ila jamaa ambaye ni mkali wa nyimbo ya utaniua jux ameonyesha kuwa halijali hiloo na hii ni baada ya kumpigia magoti aliyekuwa e wake vannesa mdee tena jukwaaani.kama inavyojulikana kuwa jux na v money kwa sasa sio wale tuliokuwa tunawajua tena baada ya kuachana na kilaa mtu kujua hamsini zake.kwa taarifa zaidi please nikuombe usubscibe kwenye blog yangu na pia tembelea kwenye page zangu za facebook na tweet

DALADALA YAZAMA ZIWA VICTORIA

IDRIS SULTAN BATA LAKARIBIA BAADA YA KUALIKWA KUIGIZA KWENYE FILAMU YENYE BAJETI YA BILLION 38

  •   Itashutiwa katika miji ya Berlin, London, Paris, Cape Town na Acapulco, Mexico

Mastaa wakubwa duniani kama Eric Dane wa Lastship ,Gerard Depardieu wa Life of Pie,  Thomas Kretschmann wa Avengers Pearl Thusi  wa  Quantico…kushiriki

NYOTA ya aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Mtanzania Idris Sultan, inaendelea kung’ara  baada ya ‘kupata shavu’ la kushiriki filamu yenye bajeti ya dola za Kimarekani milioni 17 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 38.

Idris pamoja na Mtanzania mwingine Ernest Napoleon, wataungana na mastaa wakubwa  duniani kama Eric Dame, mwigizaji Mmarekani, Gerard Depardieu wa Ufaransa, Thomas Kretschmann wa Ujerumani na wengine wengi kucheza filamu hiyo ya ujambazi wa kimataifa.

Filamu hiyo itakayojulikana kwa jina la ‘The Blue Mauritius’, inahusu majambazi watano wa kimataifa ambao wanasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika ya Kusini, kwa ajili ya kuiba vitu mbali mbali vyenye thamani kubwa duniani.

Idris na mwenzake Ernest Napoleon, watasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika kusini mapema mwakani kwa ajili ya filamu hii  kubwa kuwahi kuwahusisha Watanzania.

“D Street inayo furaha kubwa kugeukia vipaji vya waigizaji wa Kiafrika kwa kuwaunganisha na waigizaji wa kimataifa kama itakavyokuwa kwa ‘The Blue Mauritius’,” anasema Dexter Davis, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya D Street Media Group ya Marekani, inayoanda filamu hiyo

Kwa mujibu wa Davis, filamu hiyo itasambazwa siyo tu Marekani, bali pia katika majumba makubwa ya sinema dunia nzima.

“Ernest na Idris watang’ara, tunasubiri kwa hamu kuwaona tena kwenye skrini kubwa wakifanya makubwa,” anasema Davis
Mapema mwaka huu, wawili hao walicheza filamu iliyojulikana kama ‘Kiumeni’ ambayo pia Ernest alikuwa ni mzalishaji na kushirikiana na Daniel Manege kuiandika. Filamu hiyo ilishinda katika Tamasha la Timataifa la Filamu la Zanzibar ambalo Idris na washiriki wenzake walihudhuria
 “Ninayo furaha kubwa kufanya kazi na Idris katika filamu kubwa kama hii ya The Blue Mauritius. Ni mwaka wa pekee kwa mimi kufanikiwa kufanya kazi na D Street. D Street inabadilisha upepo kwa Afrika inapokuja kwenye suala la kutengeneza filamu,” anasema Ernest 
Kwa upande wake Idris anasema, “Nilikutana Dexter Davis kwenye Maonyesho ya Filamu ya Kimataifa ya Zanzibar mwezi Julai na nilifurahishwa na namna ambavyo amevutiwa na vipaji kutoka Afrika. Alivutiwa kufanya kazi na mimi baada ya kuona ushiriki wangu katika filamu ya ‘Ballin; On the Other side of the World’ na miezi miwili baadaye nilishiriki Katina filamu moja ya Kimarekani. Filamu hizi mbili zimenifanya niweze kufanya kazi nchini Marekani jambo ambalo nilitamani sana,” 
Filamu hiyo inatarajia kuanza kuzalishwa mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka ujao (2018).

MBOWE ATOA IDADI YA OPERATION ALIZOFANYIWA MHE:LISSU MPAKA SASA

Image result for tundu lissu 2017

ACT WAZALENDO WAPINGA UCHAGUZI ULIOFANYWA NA RAIS KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI

Jana, Oktoba 7, 2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya teuzi mbalimbali ikiwemo uteuzi wa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
ACT Wazalendo tunasikitika kusema Kwamba kama ilivyo desturi, Rais ameamua kuyaweka pembeni matakwa ya Sheria yanayoongoza mchakato wa uteuzi wa Katibu wa Bunge na kuamua kujichagulia apendavyo.

Kutokana na unyeti wa nafasi ya Katibu wa Bunge, na kwa minajili ya kuweka ‘check and balance’ pamoja na kulinda uhuru wa Bunge, kwenye mchakato wa uteuzi wa nafasi husika, sheria imeweka utaratibu wa kufuatwa kwenye uteuzi wa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo basi, mbali na Rais kuwa na mamlaka ya kumteua Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anapaswa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Sheria ya Utawala wa Bunge – The National Assembly (Admintration Act), 2015. Kwa mujibu wa Kifungu cha 7(3) cha Sheria hiyo, Rais atateua jina moja kutoka miongoni mwa majina matatu yaliyopendekezwa na Tume ya Huduma za Bunge. 

Jambo hili sio la hiyari. Ni sharti la lazima la sheria ambalo Rais analazimika kulifuata. Ndio maana kifungu husika kinasema “The Commision shall recommend three names” (Tume ni LAZIMA ipendekeze majina matatu). 
Wajumbe wa Tume ya Huduma za Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 12(2) cha Sheria ya Utawala wa Bunge ni wafuatao:
1. Ndg. Job Ndugai, Spika wa Bunge

2. Ndg. Tulia Akson, Naibu Spika wa Bunge
3. Ndugu Jenister Mhagama – Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Bunge
4. Ndg. Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni
5. Ndg. Magdalena Sakaya – Kamishna wa Bunge (CUF)
6. Ndg. Peter Msigwa – Kamishna wa Bunge (Chadema)
7. Ndg. Salim Hassan Abdullah Turky – (Kamishna wa Bunge – CCM)
8. Ndg. George Masaju
9. Ndg. Mary Chatanda (Kamishna wa Bunge – CCM)
10. Ndg. Kangi Lugola-(Kamishna wa Bunge-CCM)
11. Ndg. Mussa Hassan Zungu-(Kamishna wa Bunge-CCM)
Kwa taarifa tulizonazo, hakuna kikao chochote cha Tume ya Bunge kilichoketi na kupendekeza majina kwa Rais kwa ajili ya uteuzi wa Katibu wa Bunge. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wote wa Tume ya Huduma za Bunge waliohojiwa na vyombo vya habari wamethibitisha pia kutofanyika kwa kikao hicho.
Hitimisho:
1. ACT Wazalendo tunaona kuwa uteuzi huu si tu ni mwendelezo wa Rais kufanya maamuzi bila kuzingatia sheria za nchi bali ni ushahidi mwingine wa wazi wa kudharau mhimili wa Bunge.
2. Ni matumaini yetu kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano na watu wote wanaopenda uhuru na uimara wa Bunge watasimama imara kuupinga uteuzi huu ambao ni kinyume na sheria.
3. Kama Rais hatatengua uteuzi huu na kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria za nchi, ACT Wazalendo kitalifikisha suala hili Mahakamani ili kupata ufafanuzi wa mahakama.
4. Ni wakati muafaka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuishauri serikali kwenye masuala ya kisheria kuwajibika. ACT Wazalendo tunaamini suala hili na vitendo vingine vya huko nyuma vimetokea kwa sababu ya moja ya sababu mbili. Inawezekana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa woga au uzembe, hamshauri Rais ipasavyo au Rais hafuati ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika yote mawili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kama anataka kulinda heshima yake binafsi na ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hana budi KUJIUZULU.
Ado Shaibu

Katibu, Itikadi, Mawasiliano na Uenezi 
ACT Wazalendo 
Oktoba 8, 2017
Dar es salaam

CHIBU(PLATNUM) APELEKWA MAHAMANI NA MOBETO

Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.Image result for DIAMOND & AMISA

Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mobeto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.

Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.

Wakili Zulu amesems leo Alhamisi amesema mteja wao Hamisa Mobeto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.

“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto  (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema.

Zulu amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu.