Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akigawa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Bethel kilichopo wilayani humo.
Watoto wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo wakiwa wamejipanga mstari kupokea zawadi.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel
Mchembe (mwenye nguo ya njano), Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo
Gairo, Mhe. Andrea Sendeha (wa tatu toka kulia) pamoja na kamati ya
ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa
kituo cha Bethel wa Gairo.
Katika kujali makundi yenye changamoto
za maisha hasa watoto wadogo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi
Mchembe amegawa sare za shule na madaftari kwa watoto yatima 150 kituo
cha Bethel Wilayani Gairo kinachosimamiwa na Mchungaji Chacha.
Hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa
ulifanyika mapema wiki hii, ambapo Mhe. Mchembe amesema kuwa huo ni
utamaduni aliojiwekea kila mwanzo wa mwaka wa kuwakumbuka watoto yatima
na wale waishi katika mazingira magumu.
"Nawakumbusha wananchi kujenga utamaduni
wa kusaidiana watu wasiojiweza ili muweze kupata baraka kutoka kwa
mwenyezi Mungu, unajua unapokuwa nacho ukatoa kidogo unabarikiwa zaidi,"
alisema Mhe. Mchembe.
Mhe. Mchembe aliwakumbusha watoto hao
kuzingatia masomo kwani Serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Magufuli
inatoa elimu bure hivyo hakuna mtoto wa masikini atakayeshindwa kusoma.
Katika kukua kwao wamtangulize Mungu naye ataendelea kuwabariki na kuwatoa katika hali ya kuhisi unyonge wa kukosa wazazi.
Mwisho aliwaasa waalimu kuwa na moyo wa
upendo kwa watoto yatima. Pia kuweka karibu hasa watoto wa kike
kuwaepusha na mimba za utotoni.