DIAMOND AVUNJA RECORD NCHINI MOZAMBIQUE

superstar ambaye anaipeperusha bendera ya bongo vizuri.mwanamziki diamond platnum amefanya show ambayo inasemekana ni moja ya show za kihistoria kufanyika katika nchi ya mozambique.

HUYU HAPA SHABIKI WA MAJIMAJI ALIYEMROGA AJIBU NA TSHISHIMBI

Najua unaweza kushangaa kuhusiana na hili ila ndio kilichotokea.Mmoja wa mashabiki wa timu ya majiamaji anashutumiwa kuwaroga wachezaji wawili wa club ya yanga sports club wakati wa mchezo baina ya timu hizo mbili

Azam FC 1 vs 0 Kagera Sugar - Azam FC Wakaa Kileleni Kwa Muda

Wakati takwimu zikionyesha kuwa asilimia sabini na tano ya watanzania wanajishughulisha na shughuli za kilimo huku, wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za uendeshaji wa shughuli zao, waziri mkuu Kassim majaliwa amesema kwa sasa wameamua kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto hizo

WAKULIMA WA PAMBA, CHAI, KAHAWA,TUMBAKU, KOROSHO KUNUFAIKA, WAZIRI MKUU

Wakati takwimu zikionyesha kuwa asilimia sabini na tano ya watanzania wanajishughulisha na shughuli za kilimo huku, wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za uendeshaji wa shughuli zao, waziri mkuu Kassim majaliwa amesema kwa sasa wameamua kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto hizo

POLISI WAMWITA OMMY DIMPOZ POLISI CENTRAL

Kama ulikuwa hujui hii hapa mpya kwenye trends za youtube ambayo inamuhusisha mwanamziki mkubwa kwenye level za buradani nchini mwanamziki ommy dimpoz ambaye aliitwa na mapoli wa central jijini Dar-es-salaam kwa ajili ya mahojiano

hili hapa povu la jackline wolper kwa x wake(harmonize)

POVU alilolitoa superstar anayetikisa kiwanda cha Bongo Muvi, Jacqueline Wolper kwa X- wake, kupitia ukurasa wake wa Instagram, ni povu ‘zito’, kiasi kwamba hata kama ni nguo chafu kiasi gani lazima zitatakata kwani amemuita ni muimba Taarab.

Kwa mujibu wa mashabiki, hasira za mkizi zilimkamata Wolper baada ya X- wake huyo kuwa anamfuatilia mara kwa mara kwenye 18 zake, kiasi cha kumsababishia mpenzi wake wa sasa anayejulikana kwa jina la Brown, kupaniki na kuhisi labda huenda, wawili hao bado wana uhusiano wa siri.
Baada ya posti hiyo ya Wolper, mashabiki wakashusha komenti kibao. Wengine walimpongeza kwa kutoa kichambo hicho, wapo waliomkosoa na kumwambia kwa nini hizo siri hakuzisema kipindi walipokuwa pamoja, na wengine waliishia kusema kwamba mapenzi ya mastaa wa Kibongo ni ‘kizunguzungu’.

GWAJIMA ATAJA WOTE WALIOTAKA KUMUUA LISSU (Kimenukaaaa!!)

inawezekana ulikuwa umepitwa na taarifa hii.ila kama unavyojua kwanguleo blog inalusogezea taarifa hizi ili na wewe uwe karibu na nchi yako.leo hii kilichojiri mtandaoni hasa youtube ni hii ya mchungaji gwajima ambaye anasema anawajua wote waliofanya shambulia lililotokea kwa mbunge wa singida mashariki ambaye pia ni rais wa tpl mheshimiwa Tundu lissu

'Zitto utanifanya nini? ninaweza kukuzuia usiongee hadi mwisho wa Ubunge...

September 13, 2017 Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza tena kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge kumhoji Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe baada ya kuendelea kutoa maneno ya kulidhalilisha Bunge licha ya jana Spika kuagiza kuhojiwa kwa kauli hizohizo.


Leo Spika amefunguka zaidi Bungeni kuhusu Zitto Kabwe na kumwambia ana uwezo wa kumzuia asiongee hadi mwisho wake wa Ubunge.

BREAKING: Mahakama ya Kisutu imemuachia huru Yusuf Manji

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuachia huru Mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati akionyesha kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya Manji na wenzake.

Spika wa Bunge Amuonya vikali tena ZITTO KABWE, anaweza Kumpiga Marufuku...

Spika wa Bunge Amuonya vikali tena ZITTO KABWE, anaweza Kumpiga Marufuku ya Kuongea Bungeni.

Spika wa Bunge Amuonya vikali tena ZITTO KABWE, anaweza Kumpiga Marufuku...

Spika wa Bunge Amuonya vikali tena ZITTO KABWE, anaweza Kumpiga Marufuku ya Kuongea Bungeni.

Mkwara wa Lipumba wapagawisha wabunge wa CCM | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

Mkwara wa Lipumba wapagawisha wabunge wa CCM | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

Upelelezi wa kesi ya Halima Mdee wa kumtolea lugha ya matusi Magufuli u...

Leo September 12 2017 upelelezi wa kesi ya kumtolea lugha ya matusi Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe Halima Mdee umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

LOWASSA ATOA SIRI, TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

TUNDU lisu Atamka maneno (12 tu) makali baada ya kufungua macho hospita...

Chadema: Tundu Lissu Apumulia Mipira, Lakini Jasiri, Tuendelee Kumuombea

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezungumzia maendeleo ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyejeruhiwa vibaya hivi karibuni baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema, amesema hali ya Lissu imekuwa ikibadilika mara kwa mara na inaonesha alipigwa zaidi ya risasi tano za kivita kwenye mwili wake, zilizomjeruhi vibaya sana. Viongozi hao wa Kamati Kuu ya Chadema wamesema mbele ya mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi yao iliyoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwamba hawana imani na jeshi la polisi na serikali katika kuwatafuta na kuwabaini waliokula njama za kumshambulia mbunge huyo

KANISA KATOLIKI LATOA TAMKO KULAANI VURUGU NA MAUAJI



SeeBait
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. 

Dar es Salaam. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limelaani shambulizi la hivi karibuni lililotekelezwa na watu wasiojulikana dhidi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mbunge huyo aliyejeruhiwa Septemba 7 kwa kupigwa risasi tano mjini Dodoma, hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Nairobi nchini Kenya.

Baraza pia limeungana na Watanzania kulaani kwa nguvu zote matendo yote ya vurugu, mauaji na uvunjifu wa amani nchini.

Tamko la baraza hilo lililosainiwa na Makamu wa Rais wa TEC, Askofu Beatus Kinyaiya limetolewa baada ya kikao cha kawaida cha baraza kilichofanyika kwa siku mbili Septemba 9 na 10 jijini Dar es Salaam.

“Katika Taifa letu sasa tunashuhudia matendo ya mauaji ya watu wasio na hatia kama ilivyokuwa kule Mkuranga, Rufiji na Kibiti, utekwaji wa watu na kuteswa, utekaji wa watoto, ulipuaji wa ofisi za watu na hivi karibuni shambulio la mbunge Lissu,” limesema baraza katika tamko hilo.

Imeelezwa vurugu na mashambulizi ya aina yoyote ile yanalifedhehesha Taifa kwa kuwa matendo hayo ni dhambi, uhalifu na si utamaduni wa Mtanzania, hivyo vyombo vinavyohusika havina budi kuyakomesha mara moja.

BUNGE LAAHIDI KUMPA USHIRIKIANO JAJI MKUU TANZANIA



SeeBait

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai atahakikisha yeye na wabunge wanampa ushirikiano Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma aliyeapishwa leo baada ya kuteuliwa siku ya jana Septemba 10 mwaka huu.


Ndugai ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatoa salamu za wabunge katika ghafla hiyo ya uapisho iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa bila ya kumsahau Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.


"Sisi kama bunge tunawahakikishia ushirikiano mkubwa sana kwa kuhakikisha kazi za Mahakama zinaendelea kama zilivyo kikatiba na tutaheshimu sana. Yale maneno na makombora moja moja ya bungeni ni vitu vya kawaida, ndiyo utamaduni wa bunge",amesema Ndugai.


Aidha, Ndugai amesema Mahakama inamchango mkubwa kwa wananchi pamoja na taifa kwa ujumla kwa kuwa hicho ndicho chombo pekee kinachoweza kumtetea mnyonge kuweza kupata haki yake kutoka kwa waporaji.


"Kuwepo kwa Mahakama ndiyo usalama wetu, amani, kheri na matumaini ya mnyonge katika sheria na maamuzi ya Mahakama. Kwa hiyo tunakutakia kila la kheri katika kazi yako, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu na tutakusaidia na kuomba msaada wako",amesisitiza Ndugai.


Kwa upande mwingine, Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma ameahidi kufanya kazi katika maadili ya kisheria pamoja na kurudisha imani ya wananchi kuhusiana na kupata misaada ya kisheria inayotolewa katika Mahakama mbalimbali ndani ya Tanzania

LOWASSA AMTEMBELEA TUNDU LISSU HOSPITALIYA ADHA KHAN NCHINI KENYA



SeeBait

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa yupo Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.


Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema alijeruhiwa kwa risasi tano Alhamisi Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini Dodoma akitokea bungeni.


Katika akaunti yake ya Twitter, Lowassa ame-tweet akisema, “Earlier today i paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of TLS and dear friend @tundulissutz He is recovering well. It is Sad times for Tanzania. Let us all keep praying.”


Kwa tafsiri isiyo rasmi amesema “Mapema leo nilitembelea Hospitali ya Nairobi kumwona mbunge, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na rafiki kipenzi Tundu Lissu. Anaendelea vizuri. Ni kipindi cha masikitiko kwa Tanzania. Kwa pamoja tuendelee kuomba.”


Katika tweet hiyo, Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ameweka picha akiwa pamoja na Alicia ambaye ni mke wa Lissu; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na dereva wa Lissu Simon Mohamed Bakari.



Earlier today i paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of TLS and dear friend @tundulissutz
He is recovering well. 1/2

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 06,2017


Magazetini leo Jumapili Agosti 06, 2017