MKUTANO WA SIKU TANO WA MAJAJI NA MAHAKIMU WA JUMUIA YA MADOLA WAFUNGULIWA NA MAKAMO WA RAIS


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa  Majaji  na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Chama cha Majaji na Mahakimu wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA). 

Makamu wa Rais alisema” jitihada zenu katika kuendeleza na kuimarisha viwango na uhuru wa mahakama na vilevile kuendeleza utawala wa sheria vimeendelea kuimarika na kuifanya jumuiya yenu kuwa imara zaidi”.

Kwa miaka mingi mmeendelea kuchochea na kuimarisha uhuru wa mahakama huku mkijitahidi kuendeleza utawala wa sheria katika nchi za jumuiya ya madola, alisema Makamu wa Rais.

Aidha, mkutano huo uliohudhuriwa na Majaji Wakuu wa Mahakama, majaji na mahakimu, Makamu wa Rais aliuasa mhimili wa Mahakama kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano ya kuondoa umaskini na rushwa ili kufikia maendeleo ya kweli. 

“Naamini kwamba nia ya kujenga mahakama yenye ufanisi, uwajibikaji na jumuishi haitafikiwa kama mahakama ya Tanzania itajitenga na jitihada za serikali za kuondoa umaskini na rushwa”, alisisitiza Makamu wa Rais.

Pia Makamu wa Rais alisisitiza kuwa rushwa huondoa uhuru wa mahakama na hivyo kupoteza utawala wa sheria.  Aliwataka washiriki wa mkutano huo kupambana na rushwa katika mahakama ili kuhakikisha haki na maendeleo vinapatikana.

Mwisho Makamu wa Rais aliwahakikishia washiriki wa mkutano huo kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kuheshimu na kuimarisha uhuru wa Mahakama kwa  kuhakikisha inaendelea kupambana na kuondoa vitendo vya rushwa.  
 
Imetolewa na :-
Ofisi ya Makamu wa Rais

NIMEMALIA ZIARA YANGU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 25 Septemba, 2017 amemaliza ziara yake ya siku 6 katika Mkoa wa Arusha.

Akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mhe. Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi wa Sangsi nje kidogo ya Jiji la Arusha na wananchi wa Pacha ya Kia Mkoani Kilimanjaro na kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kutatua kero za wananchi na kuwahudumia bila kuwabagua kwa misingi ya itikadi za kisiasa, dini na ukabila.

Mhe. Rais Magufuli amesema katika kutimiza azma hiyo Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya Usa River  – Arusha inayojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 139, mradi wa maji wa Arusha utakaogharimu Shilingi Bilioni 42, mradi wa kusambaza umeme katika vijiji zaidi ya 200 na mingine mingi inayotekelezwa katika maeneo hayo.

“Nina uhakika nyinyi wakazi wa Arusha mnaona Arusha inavyobadilika, kabla ya kujengwa barabara hii kulikuwa kunatokea ajali nyingi, na kuna watu walikufa pale kwenye daraja, inawezekana wengine wameanza kusahau, wanaozaliwa sasa hivi wanaweza kuona haya sio chochote lakini hii ni ishara ya kupanda kwa uchumi wetu, uchumi unapopanda na miundominu inakuwa mizuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero mbalimbali za wananchi wakiwemo wafanyakazi ambao wamelalamikia kuhamishwa vituo vya kazi bila kulipwa stahiki zao na amerejea agizo lake la kupiga marufuku mfanyakazi yeyote kuhamishwa kituo cha kazi pasipo kulipwa stahiki zake.

Kuhusu kero za wananchi wa pacha ya Kia waliolalamikia tatizo la uhaba wa maji, kunyang’anywa maeneo ya biashara na waliokuwa walinzi wa uwanja wa ndege kudai haki zao Mhe. Rais Magufuli ameziagiza mamlaka husika kushughulikia matatizo hayo.

Mhe. Rais Magufuli amerejea Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Arusha
25 Septemba, 2017

STOP TUZO ZA MZIKI NA MSHINDANO YA MITINDO ASEMA WAZIRI MWAKYEMBE

Mwakyembe apiga marufuku tuzo za muziki na mashindano ya Miss Tanzania

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amepiga marufuku mashindano ya Miss Tanzania na tuzo za muziki kutokana na ubabaishaji wa waandaaji wa mashindano ya tasnia hizo.

Mwakyembe amesema mashindano ya Miss Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji kwenye utoaji wa tuzo na kumekuwa na tabia ya kuchelewa kuwapa washindi zawadi wanazoahidiwa jambo linaloleta usumbufu.

Waziri huyo ameongeza kuwa watakaotaka kuandaa mashindano hayo ni lazima zawadi wanazoahidi kuwapa washindi zipekwe ofisini kwake.

”Kwa sasa tunanakaa chini na wadau wa burudani juu ya mashindano hayo ila tunataka tuzo ziwe na (guaranteed sustainability) muendelezo wa uhakika na sio kufanyika kwa kubahatisha”, alisema Mwakyembe.

Kwa mara ya mwisho mashindano ya za Miss Tanzania yalifanyika mwaka 2016 ambapo ilichukua takribani miezi 6 kwa Kamati ya shindano la Urembo la Miss Tanzania kumpatia mshindi zawadi yake.

Kwenye tuzo za muziki waziri Mwakyembe amesema tuzo hizo zinahitaji marekebisho kwani zilikuwa zikitegemea watu wachache kiasi kwamba wakinuna basi hakuna tuzo.

IJUE SABABU YA KOCHA WA NJOMBE MJI KUONDOKA




Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Njombe Mji, Hassan Banyai amefunguka kueleza sababu zilizo mpelekeakuchgukua uamuzi wa kuachana na timu hiyo.
Banyai amesema sababu kubwa iliyopelekea yeye kuondoka ni kutishiwa maisha na watu waliokuwa wanamuambia aawaachie timu yao.
Hata hivyo, Banyani aliongeza kuwa katika timu ya Njombe Mji hakukuwa na utaratibu mzuri hasa wa kuheshimu taaluma pamoja na viongozi mbali mbali wa timu hiyo na badala yake kila mtu alikuwa anaingilia majukumu ya mwenzake suala ambalo kocha huyo hakulipenda..

NANI MCHEZAJI BORA MWAKA HUU.JE NI MESSI,RONALDO AU NEYMAR JR

NI YULE YULE MORATA WA REAL MADRID HATMAYE AFUNGA HATI TRICK YAKE YA KWANZA CHELSEA

SPOR



Alvaro Morata alifunga mabao matatu katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa hapo jana wakati Chelsea ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City.
Morata alifunga bao la kwanza dakika ya 2 baada ya mchezo kuanza akipokea pasi nzuri kutoka kwa Cesar Azpilicueta kabla ya Pedro kufunga bao la pili dakika ya 30 kisha Morata akafunga dakika ya 70 na 82.
Hii ni hat-trick ya kwanza kwa Morata tangu ajiunge na Chelsea kwa ada ya pauni milioni 60 akitokea Real Madrid, mshambuliaji huyo anaonekana kuanza kuonyesha uwezo mkubwa ikiwa ni siku chache baada ya Chelsea kukubali kumuuza Diego Costa.

PSG YASHINDWA KUTAMBA BILA NEYMAR JR


1 min ago Comments Off on PSG yashindwa kutamba bila Neymar
Klabu ya Paris St-Germain ikicheza bila mshambuliaji wake Neymar Jr imeshindwa kupata pointi tatu katika ligi kuu ya Ufaransa ‘League 1’ kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kupata sare ya 0-0 na klabu ya Montpelleir.
Neymar ambaye hivi karibuni alitofautiana na Edinson Cavani kuhusu ni nani angepiga penati katika mechi yao ya mwisho dhidi Lyon, anasumbuliwa na jeraha dogo la mguu.
Wakati PSG wakiambulia sare katika mchezo huo, Monaco ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Ufaransa wameibuka na Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya klabu ya Lille.

Wachezaji wa ligi ya marekani wagomea kuimba wimbo wa taifa



Wachezaji wa ligi ya Marekani ya ‘NFL’ waligoma kusimama wakati wimbo wa taifa wa Marekani ulipokuwa ukipigwa katika uwanja wa Wembley ikiwa ni inshara ya kuonyesha Umoja wa kupinga sera za Donald Trump dhidi ya wanamichezo.
Tukio hilo limetokea wakati wa mchezo baina ya timu za Baltimore Ravens na Jacksonville Jaguars za marekani ikiwa ni siku chache baada ya rais Donald Trump kutaka wachezaji wanaokaidi kuheshimu wimbo wa taifa kufukuzwa kazi.
Wakati wimbo wa taifa ukipigwa baadhi ya wachezaji walisimama huku wakiwa wamekunja mikono ya na wengine walipiga magoti kitu ambacho hakiruhusiwi wakati wa wimbo wa taifa.

ijue biashara ya kwanza aliyokuwa anafanya nick wa pili

>Biashara aliyokuwa anafanya Nikki Wa Pili kabla yakuwa msanii Biashara aliyokuwa anafanya Nikki Wa Pili kabla yakuwa msanii Msanii Hip hop kutoka Kampuni ya Weusi Nickson Simon maarufu kwa jina la Nikki Wa Pili aeleza ukweli wa baadhi ya mashairi ambayo yanapatikana kwenye wimbo wake mpya wa Kihasana wimbo ambao umetoka hivi karibuni akiwa amemshirikisha msanii Chin Bees kutoka Wanene Entertainment. Nikki amesema kuwa Mashairi ambayo yanapatikana kwenye wimbo wake mpya na iliyopo katika wimbo wake huo yana uhusiano na maisha yake ambayo ameyapitia wakati ambao alikuwa bado yupo Arusha na wala hajaanza kujihusisha na muziki . ”Wimbo wangu mpya wa Kihasara ambao nimefanya na Chin Bees mashairi yaliyomo mule yana uhusiano mkubwa na maisha yangu ambayo nimeyapitia hasa suala la mimi kufanya biashara ya kuuza sambusa kwenye Bar, Sehemu wanazo uza pombe za kienyeji pamoja na maeneo mbali mbali mpaka usiku wa saa tatu ni kweli kabisa nimepitia maisha hayo” amesena Nikki Wa Pili.

simba wakanusa kumfukuza omog

Uongozi wa klabu ya Simba SC umekanusha taarifa za kumfukuza kazi kocha Joseph Omog, kama ilivyoripotiwa katika mitandao ya kijamii mapema hii leo. Kwa niaba ya uongozi wa klabu ya Simba, mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu hiyo ya Msimbazi Haji Manara amezungumza na Dar24 na kusema, Simba haijatoa taarifa yeyote kuhusiana na mabadiliko yanayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii. Manara amesema anaamini wanaotoa taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii hawaitakii mema klabu ya Simba, ambayo bado inamuamini kocha huyo kutoka nchini Cameroon. ‘Nimeshaeleza toka awali kuwa, hakuna mechi tano wala huo mpango wa kumwondoa kocha Omog au benchi zima la ufundi, klabu ya Simba haina mpango huo.

ZUNGU: 'Hakuna sheria itayotungwa na bunge itakayozuia mimba mashuleni'

kwako kija mwenzangu ambaye unatarajia kupata kazi pindi pale utakapomaliza elimu yake ya chuo,sasa mpya ni hii kuwa usitarajie kuwa utapata kazi mara baada tu utakapo maliza elimu.mheshimu idd azani zungu asema hayo kwenye moja ya maafali yaliyofanyika ili kuwaaga wahitimu wa shule ya babra.huku akisema hakuna sheria itakayotungwa kuhusuana na mimba

Joh Makini aongelea Kiki za bongo, views ndogo Youtube na mengine

mwanamziki superstar wa bongo kwenye rap,joh makini anaelezea kiki za bongo kwenye youtube.anasema kwa sasa wimbo wake wa katakata leta ambayo ameimba na davido ambaye ni moja ya masuperstar wakubwa nchi nigeria.anelezea kuwa ni kiki tu.ambazo zinafanya kuwa viewers wengi kwenye youtube.

Dear visitors from all over the place in the world i would like you to subcribe more in my  blog and make advertisement in my blog let be  and work  together

"MAKONDA ANAHUSIKA KUMPIGA LISSU RISASI"' ni kauli iliotol...

JAMII YAHIMIZWA KUJALI WATOTO NJITI

jamii ya Tanzania imeshauriwa kujali watoto njiti.maneno hayo yamesemwa na mmoja wa wa wauuguzi wa kulea watoto hao katika hospitali ya muhimbili dar-es-salaam

Mashabiki wataka kocha wa simba kutimu

Mashabiki kadhaa wamekuwa wakitaka uongozi wa Simba kufanya kila linalowezekana ili kumuondoa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog kwa kuwa wanaamini kikosi ni kikubwa kuliko yeye. Sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mbao FC, iliamsha mjadala mpya na mashabiki wameanza tena kutaka Mcameroon huyo aondoke. Manara amesema, uongozi unapaswa kutafakari kila jambo kwa kuwa mwisho, kama ni sifa au lawama huenda kwa uongozi. “Unajua mashabiki wanapaswa kujifunza na ikiwezekana kuwa watulivu na kuiacha taalum ifanye kazi. Mfano suala la sub linaweza kuwa limewaudhi, lakini hawajawahi kwenda mazoezini. “Walimu ndiyo wanajua nani anafanya vizuri, nani wakimtumia kwa wakati gani itakuwa sahihi na si mashabiki wanamshabikia nani,” anasema. “Lakini hiyo haitoshi, kila mmoja anakumbuka, sisi ndiyo tulikuwa tunaongoza kuwafukuza makocha na ikawa si kitu kizuri. Sasa hatuwezi kuwa kitu kidogo, kocha aondoke. “Tunaweza kupata kocha mzuri kabisa na maarufu, lakini pia asipate matokeo tunayotaka. Hii nayo itaturudisha nyuma na kuongeza maneno tena, hivyo ni lazima kutafakari mambo na ikiwezekana kuangalia utatuzi sahihi wa tatizo. Kufukuza au kuajili si njia pekee ya kumaliza tatizo,” alisema.

ZITTO AANIKA MAJIBU ALIYOWAJIBU WAJUMBE WA KAMATI ILIYOMHOJI,ZIPO HOJA KUMI NZITO HAPA

Maelezo ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (Mb), mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati, Mnano tarehe 13 Septemba, 2017 nilipata wito wa kufika mbele ya Kamati yako kutoa ushahidi wa masuala mbalimbali. Nilipata wito husika saa nane na dakika 40 mchana, nikitakiwa kufika mbele ya kamati yako, hapa Dodoma saa saba mchana siku hiyo hiyo. Nililetewa wito huo na RCO Mkoa wa Kigoma nikiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kigoma Ujiji. Sikuweza kufika, isingewezekana katika mazingira hayo niwe na uwezo wa kusafiri kutoka Kigoma na kufika mbele ya kamati yako hapa Dodoma. Kwanza muda ulishapita, lakini hata taratibu za kiusafiri pamoja na umbali kati ya Kigoma na Dodoma hazikuwezesha Jambo hilo. Siku iliyofuata nilipata ajali, ambapo nyumba yangu iliwaka moto wakati nikiwa njiani kwenda Nairobi kumuona mbunge mwenzetu mgonjwa, ndugu Tundu Lissu. Jana tarehe Septemba 20, 2017 nikiwa natokea Kigoma ili kuja kwenye Kamati nilikamatwa na Polisi ili kufikishwa mbele ya Kamati yako. Leo nimefika mbele yenu na nitajibu wito wenu kama ifuatavyo: A: Kwamba maoni yangu kwenye mtandao wa Twitter kuwa "Bunge siku hizi ni Idara ya Tawi la Utawala" yanadhalilisha Mhimili Wa Bunge. Maneno hayo ni ya kwangu na nimeyatoa kama raia wa Tanzania. Ninaamini kwa dhati kuwa Bunge la Kumi na Moja limekuwa likifanya kazi kwa kuingiliwa na Serikali chini ya ndugu Rais John Pombe Magufuli. Maneno na vitendo vya Rais yanaashiria kuwa Bunge halina Uhuru wake, na mimi kama Mbunge nina wajibu wa kuonyesha kutopendezwa kwangu na hali hiyo. Nina mifano kumi (10) kuthibitisha maelezo yangu hayo kama ifuatavyo: 1. Kuzuiwa kwa "Bunge Live" kwa kisingizio cha kupunguza gharama za uendeshaji wa mhimili wa Bunge, wakati Mikutano yote ya mhimili wa Serikali, hasa ya Rais ikirushwa live (mubashara) ni dalili ya wazi ya kufifisha sauti ya Bunge na kupandisha sauti ya serikali. Hata vituo binafsi ambavyo vilipanga kurusha bunge Live bila malipo (na hivyo kutokuwa na gharama) vilizuiwa, lakini vinarusha Live mikutano ya Rais. 2. Kitendo cha Uongozi wa Bunge kurudisha serikalini shilingi Bilioni 6 bila ridhaa ya wabunge kwa kisingizio kwamba zimebaki kutokana na kubana matumizi. Hii ni dalili ya wazi ya Bunge "kujipendekeza" kwa serikali. Wakati Uongozi wa Bunge ukirejesha kiwango hicho cha Fedha, kuna taarifa kwamba kamati nyingi za Bunge zinashindwa kutekeleza wajibu wake kwa sababu ya ukata. 3. Maelekezo ya mhimili wa Serikali kwa mhimili wa Bunge, kupitia maagizo ya Rais Magufuli kwa Spika Ndugai kuwa "Awashughulikie wabunge" (kwa kuwafukuza bungeni) aliowaita " waropokaji" ili waje wazungumze nje ya Bunge na yeye Rais (Serikali) apate nafasi ya kuwashughulikia. Kauli hii ya Rais aliyoitoa wakati akipokea Ripoti ya Prof. Osoro kuhusu Mikataba ya Madini, Juni 12, 2017 inaonyesha picha iliyo dhahiri kuwa Bunge linapokea Maelekezo kutoka Serikalini ya kuwadhibiti wabunge hasa wanaoiwajibisha serikali. Na hatuwahi kuliona Bunge likiyakana maelekezo hayo ya Rais kwa Spika. 4. Kitendo cha Bunge kuhariri hotuba za kambi ya upinzani kwa kushinikiza kuondolewa kwa vipengele vinavyoikosoa Serikali. Mathalani, Wakati wa Bunge la Bajeti, hotuba ya Msemaji wa Kambi ya upinzani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ndugu Godbless Lema, iliamriwa kuondolewa maneno yanayohusu kashfa ya Mkataba wa Lugumi, kumhusisha Rais na kuuzwa kwa nyumba za Serikali, Mauaji ya wanasiasa, pamoja na Bunge kulinda wahalifu. 5. Kauli ya Rais Magufuli ya Novemba 4, 2016 akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuwa "mzizi wa mhimili wa serikali ni mrefu zaidi kuliko mihimili mingine" mara baada ya kuulizwa juu ya matumizi ya Serikali Nje ya Bajeti iliyoidhinishwa na bunge, unaonyesha dhahiri fikra ya Rais na Serikali yake juu ya ukuu wa mhimili wa Serikali dhidi ya Bunge. 6. Kitendo cha Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Tanzanite na Almasi kusomwa nje ya Bunge na kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu na Rais bila kuwasilishwa na kujadiliwa Bungeni ili kuwekewa azimio la Bunge. Kitendo hiki kinaifanya Kamati hiyo kuonekana kuwa ya Serikali badala ya Kamati ya Bunge. 7. Kauli ya Rais kuwa Spika alimpigia simu kumuuliza juu wajumbe wa kuwaweka kwenye Kamati za Bunge za Tanzanite na Almasi inaonyesha dhahiri kuwa Spika anafanya kazi kwa maelekezo ya Rais. Na Bunge na Spika hawajawahi kuikana kauli hii ya Rais. 8. Kwa mara ya kwanza kwenye Historia ya Nchi yetu tumeshuhudia Mbunge akishambuliwa kwa risasi wakati Mkutano wa Bunge ukiwa unaendelea. Haijapata kutokea katika historia ya Bunge letu, Wabunge kukamatwa hovyo mbele ya mageti ya Bunge na kusafirishwa usiku usiku bila hata Spika kujulishwa kama taratibu za Mabunge ya Jumuiya ya Madola zinavyotaka. Kitendo cha 'Watu Wasiojulikana' kummiminia risasi zaidi ya thelathini Mbunge wa Singida Mashariki, ndugu Tundu Lissu, wakati akitokea Bungeni, tena kwenye makazi yake, ambayo kwa mujibu wa sheria ni sehemu ya Bunge, ni dharau ya hali ya juu kwa Mhimili huu. Ni tukio linalolenga kuliziba mdomo Bunge . Makala yangu ya Nani alitaka kumwua Tundu Lissu (kwa lugha ya Kiingereza) naiambatanisha katika maelezo yangu haya. 9. Kitendo cha Serikali kutowasilisha 'Taarifa za Utendaji wa Robo Mwaka' kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti ya mwaka 2014 ni dharau kubwa kwa Mhimili wa Bunge. Ni dharau zaidi kwamba Serikali ilileta Muswada wa sheria kuondoa kifungu kinacholazimisha Waziri wa Fedha kutoa Taarifa hizo, na Bunge kupitisha kuwa Sheria, hivyo kuondoa kabisa Uwajibikaji wa kibajeti wa Serikali ndani ya Bunge, hivyo kudunisha hadhi ya bunge. 10. Bajeti ya Bunge kutowekwa kwenye Mfuko wa Bunge kwa mujibu wa sheria, na Spika kutakiwa kuomba vibali vya safari za Wabunge kwa Mkuu wa Tawi la Utendaji (Serikali) ni maelezo tosha kuwa Bunge ni Tawi la Utendaji na sio Mhimili unaojitegemea. Ninayo mifano mingine mingi tu ya kuonyesha kama ushahidi wa jambo hili, kwa sasa hiyo 10 naomba itoshe. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , nchi yetu ina mihimili mikuu mitatu ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama . Katiba na Sheria mbalimbali za nchi zimewekwa kuhakikisha kila mhimili unafanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa na mhimili mwingine. Kikatiba, mbali na wajibu wake wa kutunga sheria, Bunge lina wajibu wa kuisimamia serikali. Kwa lugha nyingine, katika utekelezaji wa majukumu yake, Bunge ni "Kiranja" wa kuibana na kuisimamia Serikali. Tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano, kumekuwepo na kauli na matendo ya viongozi wa serikali na Bunge yanayoashiria uelekeo wa serikali kuminya na kuingilia uhuru wa Bunge. Baadhi ya vitendo hivi vimefanywa hata na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kutambua wajibu wangu katika kulinda heshima, uhuru, hadhi, haki, ufanisi na madaraka ya Bunge katika kutekeleza majukumu yake, mara kadhaa nimekumbusha na ilipobidi kuonya ndani na nje ya Bunge dhidi ya vitendo hivi. Maoni yangu yaliyonifanya niitwe hapa, pamoja na Mifano kumi (10) niliyoitoa hapo juu vinaonyesha wazi nia yangu njema ya kuonya na kutaka kulindwa kwa hadhi, heshima, haki na madaraka ya Bunge letu tukufu. Naamini bunge lilipaswa kunipongeza ni kunishajiisha kwa kazi hiyo, na si kinyume chake ninapotuhumiwa na kuletwa mbele ya Kamati yako kuwa nimelidhalilisha bunge pamoja na spika wa bunge. Jambo hili litavunja morali ya wabunge kutetea hadhi ya bunge letu. Mheshimiwa Mwenyekiti (Mzee George Huruma Mkuchika), Wewe ni miongoni mwa wazee ninaowaheshimu sana hapa nchini, nilivyo sasa kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya malezi yako kwangu hapa bungeni, umeshiriki kunifinyanga niwe mbunge imara kwa busara na hekima zako, pamoja na kunipa ujasiri wa kuisimamia kutokana na uzoefu wako. Nakutambua kama muumini wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, iliyotangazwa kupitia Azimio la Arusha. Napenda ninukuu sehemu ya Azimio la Arusha kuhusu Uhuru wa mawazo. Azimio linasema "kwamba TANU inaamini: kila Raia wa Tanzania ana haki ya Uhuru wa Mawazo..." Napenda kusisitiza kuwa kama Mtanzania ninao Uhuru wa Mawazo na Maoni, hiyo ni kwa mujibu wa Katiba yetu, Ibara ya 18. Kitendo cha mimi kuitwa mbele ya Kamati yako kwa maoni yangu haya, naamini ni mwendelezo wa kufinywa kwa haki na uhuru wa mawazo na maoni ya raia. Mimi kama mtanzania ninaruhusiwa kuwa na maoni yangu, na pia nina haki ya kutoa maoni yangu hayo. Kunituhumu kwa maoni yangu binafsi kuwa yanavunja heshima, hadhi, haki na mamlaka ya bunge, na kuwa maoni yangu hayo ni kulidhalilisha Bunge na Spika si sahihi kabisa, ni uonevu dhidi yangu, ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kinyume na Haki za Binadamu, hasa kwa kuwa mifano hiyo 10 niliyoitoa imeonyesha usahihi wa maoni yangu hayo. Maoni yangu yalilenga kulinda hadhi, haki, heshima na madaraka ya bunge letu tukufu. Ni maoni yaliyolenga kulinda heshima ya spika, ili azitumie nguvu alizonazo kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Bunge kulinda heshima na hadhi ya Bunge isiporomoke, ni maoni yaliyolenga kuonyesha imani niliyokuwa nayo juu yake (Spika), ni maoni yaliyolenga kulizindua Bunge juu ya hali ya kukosa mshawasha/msisimko ambao Watanzania wameuzoea. Tafsiri kuwa maneno yangu kuwa Spika hajafikia viwango vya Maspika waliotangulia kabla yake kuwa ni kumdharau si sahihi. Maoni yangu hayakulenga kuonyesha dharau, bali yalilenga kutaka Bunge liyalinde yale mambo mazuri yaliyosimikwa na Maspika hao wa nyuma katika kuisimamia Serikali. Jambo hili (la kutaka kuendelezwa na kulindwa kwa mambo mazuri ya maspika wa nyuma yaliyoimarisha hadhi ya Bunge) ni ahadi ya Spika wetu, ndugu Ndugai, wakati wa kikao maalum cha Bunge cha msiba wa Spika wa Bunge la 9, ndugu Samuel John Sitta. Hivyo ni dhahiri, mimi kukumbushia ahadi hiyo ya Spika mwenyewe haiwezi kwa namna yoyote ile kuwa ni kudhalilisha Bunge na kumdhalilisha Spika, bali kitendo cha kuitwa hapa mbele ya kamati yako kwa maoni yangu binafsi nje ya bunge, maoni yaliyolenga tu kukumbushia ahadi husika, hakika kinalidhalilisha Bunge na Spika wa Bunge Kuona mawazo huru haya yangu kuwa ni kudhalilisha Bunge si sawa. Ni kinyume kabisa na misingi ya TANU iliyoasisi Utaifa wetu, ni kinyume na Utanzania wetu. Wananchi wangapi wataletwa mbele ya Kamati yako kuhojiwa kwa kutoa maoni yao juu ya hadhi ya mhimili wa Bunge? Imani yangu ni kuwa, Hadhi, Heshima, Haki na Madaraka ya Bunge haitotokana na kuhoji wanaotoa maoni juu ya mwenendo wa bunge, kutumia maguvu ya Jeshi la Polisi, wala vitisho vya Kiongozi wa Mhimili wetu huu dhidi ya wabunge, bali ni mwenendo wake wa kuisimamia Serikali mbele ya umma ndio utakaojenga hadhi, heshima, haki na madaraka ya Bunge kwa wananchi. Mheshimiwa Mwenyekiti Iwapo Bunge litaendelea kuwa 'paraded ' Ikulu kila wakati na kupewa maelekezo na wakati mwengine kusimangwa na Serikali, kupitia Rais, umma utaona sio Bunge lao bali ni Tawi tu la Serikali, na kamati yako itakuwa na kazi ya kuita maelefu ya Watanzania. Nawashukuru sana kwa kunisikiliza. Naomba Kuwasilisha. Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mbunge, Kigoma Mjini - ACT Wazalendo , Dodoma . Septemba 21, 2017.

MSEMAJI WA SERIKALI AWAJIBU CHADEMA: WAMEKUFA WATU WANGAPI KIBITI HATUKUITA WAZUNGU?

Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji watu wangapi wamekufa na wazungu hawakuja. Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu? Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio. Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu". Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na waru wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D' Dodoma alipokuwa akitokea bungeni mchana.

mbowe aanika ukweli juu ya sakata la lissu

MBOWE;-kwenye kikao tulichokaa dodoma mimi pamoja na waziri wa afya Ummy Mwalimu,waziri wa mambo ya ndani,katibu wa bunge,naibu spika na spika wa bunge. MBOWE.-Serikali iliweka msimamo kuwa kama lissu atapelekwa nairobi badala ya muhimbili haitakuwa tayari kugharamia matibabu ya lissu. MBOWE;-Spika alitamka wazi kuwa bunge haliko tayari kugharamia matibabu ya lissu kama atapelekwa nairobi na spika alisema anajitoa na ananawa mikono. MBOWE;-huyu Ummy mwalimu aliyesema jana kuwa serikali ipo tayari kugharamia matibabu ya lissu ndiye aliyeweka msimamo kuwa kama lissu atapelekwa nairobi basi serikali haiko tayari kugharamia matibabu yake. MBOWE;-ummy mwalimu anasema wanaochangisha pesa za matibabu ya lissu ni matapeli mwambieni sisi hatuko kama wao waliokula pesa za rambirambi za kagera tutawatolea hesabu ya pesa zote za michango. MBOWE-;mpaka sasa pesa ambazo wabunge walitoa nusu ya posho zao spika wa bunge amezitia mfukoni pamoja na kwamba aliomba acaunt ya hospital aziingize lakini mpaka leo spika hajaingiza hizo pesa ambazo wabunge walitoa kwa ajili ya matibabu ya lissu. MBOWE;-Jaji mkuu suala ya uchunguzi si la mahakama ni la polisi wewe usubiri mahakamani tunakuheshimu sana ,tunapoomba uchunguzi kutoka nje ya nchi inamaana hatuna imani na vyombo vya ndani ..Kwa hiyo si vema sana jaji kutuingilia kwa hili..tunakuheshimu sana nisingependa kumvunjia heshima jaji huyu. MBOWE-;spika alinipigia simu juzi kuwa wapo tayari kuhudumia kwa masharti matatu..Sharti la kwanza ni mbowe uandike barua ya maombi,,Sharti ya pili ni lissu lazima apelekwa india,,-Sharti la 3 familia iandike barua ya maombi. MBOWE -;mbunge kutibiwa stahiki yake..mbunge hapaswi kuandika barua ya maombi kutibiwa kwake labda kama anaumwa mke wake au mtoto. MBOWE-;mpaka sasa gharama za lissu kutibiwa ni zaidi ya milion 122,michango ya lissu ni dolla elfu 22 kutoka kwa watanzania wanaokaa nje,watanzania wa ndani wamechangia milion 54 za acaunt ya CRDB kwa njia simu ni milion 24. MBOWE;-kuhusu ulinzi wa lissu msiwe na shida lissu analindwa 24 hours. MBOWE-;Sisi kama binadamu tuna hisia kutokana na unyama tunaofanyiwa na serikali iliyopo madarakani ,Tuna hisi kuwa waliomshambulia lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama.