MELI YA MFALME WA OMANI YAWASILI DAR ES SALAAM IKIWA NA JUMLA YA WATU 350 NDANI YAKE

Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar

 Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH ikiingia katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Oman ikiwa na Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo,ikiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi  Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi wa Serikali ya Oman.
 Meli ya iliyobeba ujumbe kutoka Oman ijulikanayo kwa jina la Fulk Al Salamah ikiwasili katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa na ujumbe wa watu takribani 350 kutoka Oman.

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussen Mwinyi akimlaki Waziri wa Mafuta na Gesi toka Oman Dkt. Mohamed Hamed  Al- Rumhi ambaye ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman uliowasili na meli ya mfalme ya Fulk Al Salamah katika bandari ya Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi walipokutana katika hafla ya mapokezi ya meli iliyobeba ujumbe kutoka kwa mfalme wa Oman uliowasili katika bandari ya Dar es Salaam leo. Katikati ni Mfanyabiashara wa Tanzania Seif A. Seif.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussen Mwinyi akiwa na kiongozi wa ujumbe kutoka Oman Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohammed Hamed Al-Rumhi wakitazama ngoma toka kwa moja ya kikundi cha watumbuizaji mara baada ya meli ya Fulk Al Salamah ikiwa na ujumbe wa watu 350 kutoka kwa mfalme wa Oman kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam leo. Picha na: Frank Shija - MAELEZO

Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika Zanzibar Oktoba 12, 2017, imeng’oa nanga leo mchana kuelekea Dar es Salaam kuendelea na safari yake ya kusambaza ujumbe wa ‘Amani na upendo’ duniani. 

Taarifa kutoka ubalozi mdogo wa Oman zimeeleza kuwa, meli hiyo itakaa Dar es Salaam kwa siku nne kabla kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo hayo. 

Akizungumza baada ya kuagana na ujumbe wa meli hiyo bandarini Zanzibar, Balozi Mdogo wa Oman Dk. Al Habsi, ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzbar chini ya Rais wake Dk. Ali Mohamed Shein na wananchi wote kwa mapokezi mazuri na ukarimu mkubwa waliouonesha kwa ndugu zao wa Oman. 

Ameomba hali hiyo iendelee, akisema mahaba na ukarimu ndiyo mambo yanayowafungamanisha Wazanzibari na Waomani ambao kihistoria ni ndugu wa miaka mingi.

SERIKALI YAHIMIZA KUNAWA MIKONO KWA SABUNI

www.kwanguleo.blogspot.com

SERIKALI imewataka wananchi kuunga mkono juhudi za usafi kwa kunawa mikono na sabuni ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu ili kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora.

Akizungumza katika kilele cha wiki ya unawaji mikono kwa maji na sabuni iliyofanyika Kata ya Kiwalani, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Ubora wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(DAWASA), Dk Sufiani Masasi alisema kama Taifa ni muhimu kuwekeza nguvu katika kuelimisha jamii hasa umuhimu wa kunawa mikono na majisafi na sabuni ili kujenga Taifa lenye afya bora.

Akizungumza na jumuiya ya wananchi, waalimu na wanafunzi wa shule za msingi Umoja, Yombo, Mwale na Bwawani, Dk Masasi alisema DAWASA ni mdau muhimu wa usafi wa mazingira ndio sababu waliamua kuadhimisha wiki hiyo kwa kutoa elimu kwa walimu 44 kutoka katika shule hizo pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa ili wawe mabalozi
wazuri katika kuwaelimisha wanafunzi juu ya umuhimu wake.

Alisema kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni ‘Mikono safi kwa manufaa ya sasa na baadae’ inaikumbusha jamii kuona umuhimu wa kunawa mikono na sabuni ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu.

Hivyo alitaka juhudi za pamoja zichukuliwe kuhakikisha wanafunzi wanaelewa umuhimu wa kunawa mikono kwani wao ndio wazazi wa siku zijazo na kwamba DAWASA itaendelea kuunga mkono kampeni za usafi hasa kwa kuendelea kubuni na kutengeneza miundombinu ya majisafi katika Maeneo mbalimbali ya jiji.

Dk Masasi alisema tayari DAWASA imefanikiwa kufikisha mradi huo wa majisafi kwa shule hizo ambapo utanufaisha wanafunzi 5123 pamoja na zahanati ya eneo hilo na kwamba itaendelea kufadhili miradi ya aina hii ili kuunga mkono juhudi hizo za usafi wa mazingira.

Mkufunzi wa mafunzo kwa walimu wa shule hizo, Juhudi Nyambuka ambaye ni Afisa Afya Manispaa ya Temeke alipongeza juhudi za DAWASA katika kusaidia jamii kupata huduma za majisafi na kueleza zitasaidia kupunguza magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji.

Katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma rasmi za maji ya bomba DAWASA, jumuiya za wananchi pamoja na wadau wa maendeleo wamekuwa wakijenga miradi ya maji kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira kwa jamii. 

Miradi hiyo ipo katika maeneo mbalimbali kama vile Ukonga, Yombo, Kitunda, Mbagala, Kijichi, Feri,Kigamboni.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Wanafunzi wa Shule za Msingi zilizopo Kata ya Kiwalani wakishiriki igizo lenye lengo la kuelimisha jamii umuhimu wa kunawa mikono na majisafi na sabuni wakati wa kilele cha wiki ya unawaji mikono kwa maji na sabuni yaliyofanyika Kiwalani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

DC MSHAMA AMALIZA MGOGORO WA WAFANYABIASHARA SOKO LA LOLIONDO




MKUU wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Bi. Assumpter Mshama amemaliza mgongano wa Wafanyabiashara wenye ubao upande wa ndani na wanaouzia kandokando ya Barabara.

Mgongano huo uliokuwepo kwenye soko la Mnalani Maarufu Loliondo kati ya Wafanyabiashara hao ambapo wanaouza ndani kwenye mbao wanadai wateja wanaishia nje hivyo hawapati wateja.

Wafanyabiashara Godruck Mwafrika na Anelista Mbaga kila mmoja amwelezea changamoto iloyopo kwenye soko hilo hali inayoleta mgongano kati yao.Mwafrika alisema kuwa waliowengi wamekimbia meza za ndani na kwenda kupanga nje kwa lengo la kupata wateja kwani wengi wanaishia nje hivyo wao kubaki wakipunga upepo tu.

Kauli hiyo ilipingwa na Bi. Aneliata ambaye alisema wote wanafanyabiashara sawa na kwamba malalamiko hayo hayana msingi huku akisema kwamba wateja wanafika kununua bidhaa sawasawa.

Baada ya kupata malalamiko ya pande mbili, Mshama ameagiza wanaofanyia biashara pembeni mwa soko wote waingie ndani na kwamba meza zote zina upana wa mita 30 hivyo kila moja watakaa watu wawili kwa maana mita 15. 

Aidha amevunja aoko la siku za Jumatano akisema hatua hiyo ni ya ujanja wa watu ambapo alisema zuio hilo litaanzia Jumatano ya wiki inayoanzia Oktoba 25 akieleza kwa kiwa agizo hilo limekujanghafla kwani wapomm watu ambao wapo maeneo mbalimbali kutafuta biashara.
 MKUU wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Bi. Assumpter Mshama akizungumza na Wafanyabashara wa soko la Loliondo.
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa soko la Loliondo wakifurahia mara baada ya mgogoro wao kutatuliwa na MKUU wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Bi. Assumpter Mshama.

OFFICE ZA BAKWATA ZAHAMIA KWA MUDA JENGO LA TIGER TOWER MTAA WA TOGO

www.kwanguleo.blogspot.com

Ndugu zangu Wanahabari,

Assalaamu Alaykum (Amani ya Mwenye ezi Mungu iwe kwenu)

Napenda kuufahamisha umma wa kiislamu kuwa kufuatia kuanza mradi wa ujenzi wa msikiti wa Mohammed VI unaojengwa katika eneo la Bakwata makao Makuu Kinondoni Road.

Hivyo basi napenda kuchukua nafasi hii kuufahamisha umma kuwa ili kupisha mradi huo Bakwata Makao Makuu imehamisha ofisi zake na kuzipeleka katika mtaa wa Togo jengo linalotambulika kama TIGER TOWER na shughuli zote zinaendelea kama kawaida.

Mwisho kabisa tunaomba radhi kwa usmbufu wowote uliojitokeza katika kipindi hiki cha ujenzi.

Wabillahi TTaufiiq

USTAADH TABU KAWAMBWA

MKURUGENZI HABARI NA MAHUSIANO.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25,2016. PICHA NA MAKTABA

WANANCHI WASISITIZWA KUTUNZA MAZINGIRA KWA KIPATO ENDELEVU


Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola akiongea na washiriki wa mradi wa Uchumi wa Kijani ndani ya Hifadhi ya Hai (GEBR) wakati akifungua mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO iliyofanyika mjini Tanga. Lengo la mradi huo ilikuwa ni kupunguza umaskini, kuhifadhi bionuwai na maendeleo endelevu katika nchi za kushini mwa Jangwa la Sahara - Usambara ya Mashariki, Tanzania. P
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi ambaye alimwakilisha mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella akifungua rasmi na kumkaribisha mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO.
Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza wakati akifungua mkutano wa majadiliano wa kufunga mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya Ushirikiano wa Kimataifa (KOICA) chini ya Programu ya UNESCO iliyofanyika mjini Tanga. Meza kuu...
 Mhifadhi wa Mazingira ya asili ya Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi.
Washiriki wa mradi huo wakiuliza maswali...
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola ameitaka jamii kujenga tabia ya kutunza mazingira katika maeneo yao kwa faida ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo. Katibu mkuu Profesa Kamuzola ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akifunga mafunzo ya mradi wa uchumi wa kijani chini ya jangwa la Sahara, yaliofanyika jijini Tanga. Alisema kuwa ni vyema wananchi wakajua umuhimu halisi wa kutunza mazingira na kuyatumia katika kujiongezea kipato. Mradi wa uchumi wa kijani chini ya Jangwa la Sahara ulikuwa ukifadhiliwa na taasisi ya Korea ya ushirikiano wa kimtaifa KOICA chini ya Programu ya UNESCO. Kwa upande wake Katibu tawala wa mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi ameisisitiza jamii kupokea vizuri miradi wanayokuwa wakiletewa na wafadhili ili iwaongezee kipata na elimu zaidi katika utunzaji wa mazingira. "Wananchi ni vyema mkabadirika na kuacha kuishi bila kutambua kuwa mazingira ukiyatunza yanakuletea kipato cha juu kabisa, ukiangalia unaona unaweza kutengeneza mkaa kwa kutumia magunz ya mahindi baada ya kuwa umeshavuna hiyo ni faida tosha kabisa," alisema Mhandishi Zena Saidi. Naye Mhifadhi wa Mazingira ya asili ya Amani, Bi. Mwanaidi Kijazi aliwashukuru sana wafadhili wa mradi huo kwa kuweza kutoa elimu kwa wananchi ... elimu ambayo imekuwa endelevu na kuwazalishia kipato cha hali ya juu. Bi. Mwanaidi alisema kuwa wananchi baaada ya kupewa elimu wameweza kujiendeleza katika miradi mbali mbali ikiwemo kutengeneza mkaa kwa kutumia majani ya mimea/magunzi, ufugaji wa vipepeo ambao wamekuwa wakiwazalisha kwa kutengeneza mapambo, kilimo cha uyoga, kilimo cha asali. Hifadhi ya mazingira ya amani inaendeleza ikolojia na baionowai ambazo ni hadimu duniani na zinapatikana katika milima ya usambara mashariki, na ina jumla ya vijiji 72.

SHEIKH PONDA AACHIWA NA POLISI KWA DHAMANA

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Pondà ameachiwa leo Jumamosi jioni baada ya kushikiliwa na Jeshi hilo tangu jana Ijumaa asubuni akituhimiwa kutoa lugha za kichochezi katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano iliyopita.Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba amesema: "Sheikh Ponda ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kuripoti tena polisi."Awali, Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema uchunguzi dhidi ya Ponda ulikuwa ukiendelea na kama ungekamilika angepewa dhamana."Upelelezi unaendelea na ukikamilika tutaangalia kama atapata dhamana au tutampeleka mahakamani," alisema Mambosasa kabla ya Sheikh Ponda kuachiwa.
Wakili wa Ponda, Profesa Abdallah Safari amesena: "Ni kweli Sheikh Pondà ameachiwa, ni lini atarudi tena sijajua ila sidhani kama watampeleka mahakamani."

NAPE AICHACHAFYA CCM KWA MARA NYINGINE

NAIBU WAZIRI WA AFYA AZINDUA KITUO CHA AFYA KIPYA PEMBA MNAZI MMOJA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

 Dr. Faustine Ndugulile akizindua kituo cha afya cha Pemba Mnazi wilaya ya Kigamboni jijini Dar es salaam.

Hospitali na zahanati za manispaa ya kigamboni zimeendelea kufanya vizuri katika utoaji wa huduma za afya hadi kufikia kuwa na kiwango cha nyota tatu japo kuwa halmashauri yake bado ni changa.



Hayo yamesemwa mapema leo na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto Mh. Faustine Ndugulile alipokuwa akizindua kituo cha afya cha Pemba Mnazi kilichopo halmashauri ya manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam.

Katika  uzinduzi huo wakazi wa eneo hilo walipata nafasi ya kutoa kero zao mbele ya naibu waziri na miongoni mwa malalamiko hayo ni upungufu wa Zahanati, vifaa tiba kama mashine za X-ray pamoja na Outro sound, magari ya wagonjwa, mashimo ya kutupia taka taka n.k
Mkuu wa wilaya ya kigamboni Mh Hashim Mgandilwa akimkaribisha naibu waziri wa afya, 

Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

 katika uzinduzi wa kituo cha afya cha Pemba Mnazi manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam.

Lakini pia changamoto nyingine ni ubovu wa bara bara hali inayofanya kushindwa kupitika wakati wa mvua pamoja na upungufu wa watumishi katika kituo hicho alichokizindua leo kwani kina jumla wa watumishi wawili ambao ni mganga mmoja na muuguzi mmoja.

Akijibu maswali ya wakazi hao naibu waziri huyo alisema kuwa kwa sasa tatizo la madawa halipo kwa zaidi ya asilimia 80 kwani serikali imetenga fedha za kutosha kuhakikisha dawa zinapatikana katika hospitali za serikali na wagonjwa hawalalamiki tena kuhusu madawa kwani bohari ya taifa ya madawa ina dawa za kutosha.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

 Dr. Faustine Ndugulile akiongea na wakazi wa pemba mnazi katika uzinduzi wa kituo cha afya kilichopo kata ya Pemba Mnazi Kigamboni jijini Dar es salaam.
Lakini pia Dr. Faustine alisema kuhusu tatizo la umeme ametoa maagizo kwa mkurugenzi wa manispaa kuwasiliana na mkurugenzi wa Taneso ili jumatatu waje wafanye tathini ya kiwango gani kinahitajika ili atoe na huduma hiyo iendelee kupatikana kituoni hapo.

Aidha naibu waziri huyo aliendelea kusema kuwa hospitali ya Vijibweni pale ilipo ni padogo hivyo kuna eneo lililotengwa kwa ajiri ya ujenzi wa hospitali hiyo na mwakani mwanzoni ujenzi huo utaanza na kwa vifaa tiba kama X ray ataongea na wizara yake mpaka mwakani mashine hizo zitakuwepo ili kuepuka tatizo la kwenda mpaka wilaya nyingine kufuata huduma hizo.

mobetto aitafuta amani ya zari

www.kwanguleo.blogspot.com


Mwanamitindo maarufu Tanzania ambaye kwa sasa anazungumziwa sana mitandaoni kwa sakata la kuzaa na msanii Diamond Platinumz, Hamisa Mobetto ametoa siri ambayo watu wengi walikuwa hawaifahamu kuhusu mahusiano yake na Diamond.
Mobetto alipohojiwa na baadhi ya vyombo vya habari ametaja kuwa tangu awe katika mahusiano ya kimapenzi na msanii Diamond Platinumz sasa ni takribani miaka tisa na huu unaingia mwaka wa kumi wawili hao kuwa pamoja.
Aidha ameeleza chanzo cha kumfungulia kesi mzazi mwenzake Diamond Platinumz mnamo oktoba 5 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto, amesema kuwa Diamond Platinumz ndiye aliyemshauri wafungue kesi ili kuhakikisha mtoto wake anapata haki yake ya msingi kutoka kwa baba.

ASKOFU: WANAOSEMA MAGUFULI AONGEZEWE MUDA NI WAPUUZI

Huyu ni askofu wa dayosisi ya iringa ambaye anazunguzia swala la kuongezewa muda kwa rais magufuli kuwa ni ujingawww.kwanguleo.blogspot.com/mpya

WASIRA AIKOSOA SERIKALI

Aliyekuwa Mbunge wa Bunda na waziri wa serikali za awamu zilizopita mhe Stephen Wasira amesema si kosa la jinai kuikosoa Serikali bali kuitukana serikali ndio kosa kwa mujibu wa sheria za nchi.


Hata hivyo Wasira amesema watu waikosoe Serikali kwa hoja na sio kutukana hivyo haoni sababu yeyote ya watu kuikosoa Serikali tena kwa hoja alafu wakamatwe,ameongeza kuwa ipo tofauti kubwa kati ya kukosoa na kutukana.

Amezungumzia pia kuhusu viongozi wa upinzani wanaokamatwa ara kwa mara na vyombo vya dola pale wanapoikosoa Serikali, ameongeza kuwa ni sawa wakamatwe lakini wapelekwe mahakamani , mahakama ndio inaweza kuamua haki kwa mujibu wa sheria kuwa kama kuna kosa au hakuna kosawww.kwanguleo.blogspot.com/mpya

RAY C AKASIRISHWA NA NANDY BAADA YA WIMBO WAKE KUIMBWA KWENYE STAGE

Wadada na ma masperstar wa Tanzania nandy na ray c wamekuwa kwenye kuto kuelewana na hii ni baada ya mwanamziki nandy kutumia wimbo wa ray c kkwenye stage ya fiesta inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.baada ya kutokelewana huku mwanamziki nandy kupitia ukurasa wake wa instagra ameandika post ambauyo ilisomeka kuwa"sitakusalimia ila nitakuheshimu"www.kwanguleo.blogspot.com/udaku

SUGU AONYESHA HOTELI ALIYOJENGA UZUNGUNI MJINI MBEYA

Ni moja ya hoteli ambazo zinaonekana ni moja ya hoteli nzuri kwa sasa mkoani mbeya,hoteli hiyo inayomilikiwa na mbunge wa mbeya mjini kupitia chadema.akieleze anasema hoteli hiyo iimejengwa kwamkopo kutoka bankwww.kwanguleo.blogspot.com/udaku

VIJUE VITU VITATU AMBAVYO MR TRUE AMBAVYO AMEAWAITA WAANDISHI

Hii ni baada ya kuwakarisha mashabiki wake kwa muda mrefu pasipo kutoa chochote huku ikikumbukwa kuwa alitoa ahadi kwa mashabiki wake kuwa watarajie makubwakwanguleo.blogspot.com/udaku

''NIMEVIONA VYA DIAMOND KULIKO YEYOTE' '- HAMISSA MOBETTO



HARMONIZE FT KOREDE BELLO - SHULALA (OFFICIAL VIDEO)

Huu hapa wimbo mpya wa harmonize ambao amemshirikisha superstar kutoka nigeria korede bello

PESA YA UCHAGUZI YASAINIWA NA RAIS UHURU KENYATA


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameidhinisha mswada wa bajeti ndogo ambapo ametenga Kiasi cha shilling za Kenya 12 bilioni (Dola 120 milioni) za kutumiwa na Tume ya Uchagizi katika uchaguzi mkuu mpya tarehe 26 Oktoba.
Kadhalika, kutengwa kwa Kshs 25 bilioni za kutumiwa kufadhili mpango wa elimu ya sekondari bila malipo ambao Rais Kenyatta alikuwa ameahidi kwenye kampeni kwamba utaanza kutekelezwa Januari mwaka ujao.
Aidha, kuna Kshs 6.7 bilioni za kufadhili ununuzi wa mahindi kuhakikisha kuuzwa kwa unga wa bei nafuu.

MNADA WA TANZANITE WASITISHWA


Wizara ya Madini imesema kuwa imesitisha mnada wa madini aina ya Tanzanite uliokuwa umetangazwa kufanyika katika mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara tarehe 12 hadi 15 Oktoba 2017.
Aidha, taarifa iliyotolewa kwa umma imesema kuwa kuahirishwa kwa mnada huo kunatokana na kuridhia kwa maombi ya wadau wa mnada ambao waliomba kupata muda zaidi wa maandalizi ili wapate fursa ya kushiriki kwa wingi.
Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa  uongozi wa Wizara na Mkoa wa Manyara watapata muda zaidi wa kuandaa mazingira salama na bora zaidi ya kufanyia mnada huo katika mji wa Mererani.
Hata hivyo, Wizara ya Madini imewaomba radhi wadau wote wa Sekta hiyo ndogo ya madini ya vito hususani Tanzanite ambao wameathirika kutokana na kuahirishwa ghafla kwa mnada huo..

MAHAKAMA YAAMURU RAIS JACOB ZUMA KUSHITAKIWA


Mahakama ya juu ya rufaa nchini Afrika Kusini imeamuru kwamba Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma lazima akabiliane na mashtaka ya rushwa, kugushi na kujihusisha na mtandao wa utakatishaji fedha.
Mahakama hiyo ilikubali uamuzi wa mahakama ya chini katika uamuzi wake ilioutoa mwaka uliopita, mahakama hiyo ikiwaamuru waendesha mashtaka wanaweza kuyarejesha mashitaka 783 ya rushwa inayohusiana na makubaliano ya kununua silaha ya mwaka 1999.