Seneta afananisha kauli ya Trump na udikteta
Maseneta wawili wa chama cha Republikan Jumatano wamemshutumu Rais
Donald Trump kwa kuendelea kuchukizwa na habari zinazokosoa uraisi wake,
wakisema kufanya hivyo kunakandamiza misingi ya kidemokrasia katika
jamii, uhuru na uwazi wa vyombo vya habari.
Katika maoni yalioandikwa katika gazeti la Washington Post, Seneta wa
Republikan kutoka Arizona John McCain amesema kitendo cha Trump
kujirudia katika madai ya “habari feki” zinapokuja habari ambazo Trump
hazipendi hutumiwa na viongozi wa nchi nyingine kama ni sababu wakati
wanavinyamazisha vyombo vya habari, “ambavyo ndio moja ya nguzo za
demokrasia.”
Huko katika Bunge la Marekani, Seneta mwengine wa Arizona, Jeff Flake, ambaye amekuwa anamkosoa mara kwa mara Trump, amesema katika hotuba yake kwenye Baraza la Seneti kuwa kitendo cha Trump kukebehi vyombo vya habari ni sawa na kauli za siasa zinazotolewa na madikteta.
“Sio tu mwaka uliopita umeshuhudia rais wa Marekani akitumia lugha ya madikteta kuelezea vyombo huru vya habari, lakini inaokena hivi sasa, amegeuka kuwahamasisha madikteta na watawala wanaotumia mabavu kwa matamko yake. Hili ni jambo la makosa. Hatuko katika zama za habari feki kama anavyoeleza ((Rais wa Syria)) Bashar Assad. Sisi tuko, ukweli ulivyo, katika zama ambazoutashi wa kidikteta unajirudia tena kwa kuwashambulia watu huru na jamii huru kila mahali."