Hekaheka iliyotokea mbele ya Makamu wa Rais leo June 16, 2017

June 16, 2017 imetokea Viwanja vya Shule ya Msingi Kinyerezi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Wilaya ya Ilala ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Hekaheka iliyotokea mbele ya Makamu wa Rais leo June 16, 2017

June 16, 2017 imetokea Viwanja vya Shule ya Msingi Kinyerezi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Wilaya ya Ilala ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Suala la nchi za guba na Qatar

Steve RNB afunguka kuhusu ukimya wake, ujio mpya

Mwimbaji staa wa RNB Tanzania ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu Steve RnB amekaa kwenye EXCLUSIVE interview ya Ayo TV na millardayo.com na kueleza ni kwa nini amekuwa kimya kwenye muziki, changamoto alizopitia kwenye ndoa hadi kuachana na mkewe pamoja na safari za nje.

"Hawa wapinzani hawaeleweki kama Popo" – Ulega

Baada ya Rais JPM kukutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Prof. John L. Thorton kitendo hiko kimepongezwa ambapo miongoni mwa waliotoa pongezi kwa JPM ni Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega ambaye amemwagia sifa kwa kitendo hiko.

Wizara Ya Elimu Kujenga Vyou vya Veta Kagera - Eng. Stella Martin Manyanya

Jason Derulo X Ray Vanny Live Performance Nairobi

Mwanamziki jason derulo ameshangazwa na kipaji alichonacho msanii kutoka kwenye lebo ya wasafi classic ray vanny kwa uwezo wake jukwaani

Rich Mavoko: Ay Ndio Alinisaidia Kuingia WCB, Stereo anaweza Akawa Msani...

Good News ya Fifa iliyoufikia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza

Uwanja wa michezo wa CCM Kirumba uliopo Mwanza umepewa hadhi ya kuwa Uwanja wa Kimataifa na tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA limeagiza maboresho ndani ya Vyumba vya kubadilishia nguo… Ayo TV na millardayo.com zimempta Katibu wa CCM Mwanza Raymond Mwangwala ambaye pamoja na mambo mengine ameelezea deni la Simba SC na Yanga SC.

BREAKING: ACACIA wamekubali kulipa pesa yote waliyoiibia TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Prof. John L. Thornton alipofika Ikulu kwa Mazungumzo June 14, 2017

"Watoto wa kike wananyanyaswa, wanabakwa" – Dr. Jasmine

Mjadala wa kuchangia mapendekezo katika Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambapo miongoni mwa waliopata nafasi hiyo leo June 15, 2017 ni Mbunge wa Vyuo Vikuu Dr. Jasmine Bunga ambaye alilieleza Bunge baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili Wanawake na watoto kwa ukosefu wa maji ikiwa ni pamoja na matukio ya kubakwa mara kwa mara…

Mwana FA na Mrisho Mpoto Watoa Neno Zito Kuhusu Ripoti ya Mchanga wa Mad...

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva na filamu, ni miongoni mwa wageni walioalikwa Ikulu wakati mheshimiwa Rais akikabidhiwa ripoti ya kamati ya mchanga wa madini na Tume ya Profesa Ossoro ambapo mbali na kutumbuiza, pia walipata nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu ripoti hiyo.
Kwa upande wake, Mwana FA anayesumbua na ngoma yake ya Dume Suruali, alisema ripoti ya kamati ya pili, imetoa mwanga wa nini cha kufanya katika suala zima la kisheria, ikiwa ni mwendelezo wa kile kilichogundulika na kamati ya kwanza.
Mwana FA alisema Watanzania wote tunapaswa kuwa wazalendo na kumuunga mkono mheshimiwa rais badala ya kuendelea kutishana mitaani kwamba nchi itashtakiwa, wafadhili wataacha kuleta misaada.
Kwa upande wa Mrisho Mpoto, naye aliwataka Watanzania kuwa na umoja na uzalendo na kumuunga mkono mheshimiwa rais kwani kama ataendeleza msimamo huu, Tanzania Mpya, ya maziwa na asali ikiwadia hata kama itakuwa watakaofaidi ni vizazi vijavyo.

Ally Hapi: Kinondoni Siyo Wilaya ya Mashamba Tena

UTATUZI MIGOGORO YA ARDHI KINONDONI WASHIKA KASI
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi ameendelea na juhudi za utatuzi wa migogoro mikubwa ya ardhi ambayo inahusisha wananchi wengi na wenye mashamba.
Hapi ameendelea na vikao mbalimbali vya utatuzi ambapo leo amefanya kikao na wananchi wa maeneo ya Kinondo, Dovya na Mbopo na kuwaahidi kuwa serikali imejipanga vema kumaliza mgogoro huo ili wananchi waishi kwa amani.

Hapi ameelezea dira ya wilaya yake kuwa ni kuhakikisha mashamba yote yanapimwa na kuwa viwanja ili kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi na kukomesha uvamizi wa ardhi uliochochewa na wenye mashamba ama kuyatelekeza mashamba yao kwa muda mrefu au kushindwa kumudu kuyaendeleza. Baada ya upimaji kila mwenye viwanja atalazimika kuwa ameviendeleza ndani ya muda maalum ili kuepusha migogoro.
Migogoro mingine mikubwa inayoendelea kutatuliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ni pamoja na TBA Mabwepande na Nyakasangwe ambao sasa umefikia hatua ya upimaji viwanja.

Mmiliki wa Migodi ya Acacia Uso kwa Uso na Rais Magufuli Ikulu, Akubali ...

Siku chache baada ya Rais John Pombe Magufuli kukabidhiwa ripoti ya kamati ya kuchunguza mchanga wa madini na kubaini kwamba kampuni ya Acacia ilikuwa ikifanya kazi zake nchini bila kuwa na vibali na ilikuwa ikisafirisha mchanga huo wa madini kinyume cha sheria, mmiliki wa migodi hiyo amemuibukia rais Magufuli Ikulu.

Breaking News: Wamekubali kulipa Pesa zetu za Madini - Magufuli amethibi...

Wamiliki wa Kampuni ya ACACIA wakubali kulipa pesa za Tanzania baada ya Mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Prof. John L. Thornton ambaye amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo Juni 14, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam na mazungumzo yao yamehudhuriwa na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja Marais wastaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwahusisha na taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (Makinikia) ambao ripoti zimekabidhiwa kwake na kamati hizo.

“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Juni, 2017

Msichana Mtanzania aliyeshinda Dollar 500 kupitia Facebook

Story kubwa kutoka Mwanza leo June 14, 2017 ni kuhusu msichana Paulina Robart mwenye umri wa miaka 18 aliyeshinda Dollar 500 za Marekani baada ya kuandika wazo kuhusu Afya ya Uzazi kupitia Facebook. Ayo TV na millardayo.com zinaye katika EXCLUSIVE Interview na amefunguka zaidi..

Beka Afunguka ukweli kuhusu Aslay kuwasaliti, Asema Mkubwa Fella hajawag...

Habari za kuvunjika kwa Bendi ya Yamoto, zinazidi kuzagaa lakini habari mpya ni kwamba, miongoni mwa memba wa kundi hilo, Beka One amefunguka kwa kirefu kuhusu maelezo hayo.
Miongoni mwa mambo aliyoyazungumza Beka One, kama ilivyo kwa memba wengine wa kundi hilo, ameendelea kukataa kwamba bendi hiyo haijafa isipokuwa wameamua kufanya kazi mmojammoja baada ya kujiona wamekua.
Beka amekanusha pia madai kwamba Said Fella amewajengea nyumba na kueleza kuwa kwa sasa wanaishi Tabata jijini Dar wote watatu isipokuwa Aslay.
Kuhusu suala la kwamba walikubaliana waondoke Yamoto band kwa sababu maslahi yalikuwa madogo, amekanusha suala hilo na pia kuhusu suala la mwenzao, Aslay kuwageuka na kurudi kufanya kazi na Mkubwa Fella, kwamba pia si kweli.
Yamekuwepo maneno mengi mitaani kuhusu kusambaratika kwa bendi hiyo kwa kile kilichoelezwa kwamba ni wasanii hao kuchoshwa na unyonyaji wanaofanyiwa na uongozi wao lakini si wanamuziki hao wala viongozi wao waliowahi kutamka hadharani kwamba bendi hiyo imekufa.

Kutana naye mtengenezaji programu tumishi mdogo zaidi.

People say you can't live without love....

People say you can't live without love....