Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva na filamu, ni miongoni mwa wageni
walioalikwa Ikulu wakati mheshimiwa Rais akikabidhiwa ripoti ya kamati
ya mchanga wa madini na Tume ya Profesa Ossoro ambapo mbali na
kutumbuiza, pia walipata nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu ripoti hiyo.
Kwa
upande wake, Mwana FA anayesumbua na ngoma yake ya Dume Suruali,
alisema ripoti ya kamati ya pili, imetoa mwanga wa nini cha kufanya
katika suala zima la kisheria, ikiwa ni mwendelezo wa kile
kilichogundulika na kamati ya kwanza.
Mwana FA alisema Watanzania
wote tunapaswa kuwa wazalendo na kumuunga mkono mheshimiwa rais badala
ya kuendelea kutishana mitaani kwamba nchi itashtakiwa, wafadhili
wataacha kuleta misaada.
Kwa upande wa Mrisho Mpoto, naye aliwataka
Watanzania kuwa na umoja na uzalendo na kumuunga mkono mheshimiwa rais
kwani kama ataendeleza msimamo huu, Tanzania Mpya, ya maziwa na asali
ikiwadia hata kama itakuwa watakaofaidi ni vizazi vijavyo.
No comments:
Post a Comment