UTATUZI MIGOGORO YA ARDHI KINONDONI WASHIKA KASI
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Mh. Ally Hapi ameendelea na juhudi za utatuzi wa migogoro
mikubwa ya ardhi ambayo inahusisha wananchi wengi na wenye mashamba.
Hapi
ameendelea na vikao mbalimbali vya utatuzi ambapo leo amefanya kikao na
wananchi wa maeneo ya Kinondo, Dovya na Mbopo na kuwaahidi kuwa
serikali imejipanga vema kumaliza mgogoro huo ili wananchi waishi kwa
amani.
Hapi ameelezea dira ya wilaya yake kuwa ni kuhakikisha
mashamba yote yanapimwa na kuwa viwanja ili kuweka mpango bora wa
matumizi ya ardhi na kukomesha uvamizi wa ardhi uliochochewa na wenye
mashamba ama kuyatelekeza mashamba yao kwa muda mrefu au kushindwa
kumudu kuyaendeleza. Baada ya upimaji kila mwenye viwanja atalazimika
kuwa ameviendeleza ndani ya muda maalum ili kuepusha migogoro.
Migogoro
mingine mikubwa inayoendelea kutatuliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ni
pamoja na TBA Mabwepande na Nyakasangwe ambao sasa umefikia hatua ya
upimaji viwanja.
No comments:
Post a Comment