Mr Universe, Matukio Chuma Atua Bongo, Ashusha Somo kwa Vijana

Mr Universe Tanzania mwaka 2002, Matukio Chuma, amewataka vijana wa Kitanzania kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ndani na nje ya nchi kuliko kubaki wakilalamika.
Chuma ameyasema hayo, wakati akizungumza na wanahabari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya kuwasili akitokea Marekani anakofanyia shughuli zake za uandishi wa vitabu, mashairi, ujasiriamali na uhamasishaji.
“Nashukuru kwa moyo waliouonesha baadhi ya marafiki na ndugu zangu kuja kunipokea. Ushauri na kilio changu kwa vijana wa Kitanzania ni kuthubutu kutumia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitangazwa dunianikama ambavyo mimi nilithubutu na ninaendelea kuthubutu,” alisema Chuma.

No comments: