CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezungumzia maendeleo ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyejeruhiwa vibaya hivi karibuni baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema, amesema hali ya Lissu imekuwa ikibadilika mara kwa mara na inaonesha alipigwa zaidi ya risasi tano za kivita kwenye mwili wake, zilizomjeruhi vibaya sana.
Viongozi hao wa Kamati Kuu ya Chadema wamesema mbele ya mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi yao iliyoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwamba hawana imani na jeshi la polisi na serikali katika kuwatafuta na kuwabaini waliokula njama za kumshambulia mbunge huyo
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mbunge huyo aliyejeruhiwa Septemba 7 kwa kupigwa risasi tano mjini Dodoma, hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Nairobi nchini Kenya.
Baraza pia limeungana na Watanzania kulaani kwa nguvu zote matendo yote ya vurugu, mauaji na uvunjifu wa amani nchini.
Tamko la baraza hilo lililosainiwa na Makamu wa Rais wa TEC, Askofu Beatus Kinyaiya limetolewa baada ya kikao cha kawaida cha baraza kilichofanyika kwa siku mbili Septemba 9 na 10 jijini Dar es Salaam.
“Katika Taifa letu sasa tunashuhudia matendo ya mauaji ya watu wasio na hatia kama ilivyokuwa kule Mkuranga, Rufiji na Kibiti, utekwaji wa watu na kuteswa, utekaji wa watoto, ulipuaji wa ofisi za watu na hivi karibuni shambulio la mbunge Lissu,” limesema baraza katika tamko hilo.
Imeelezwa vurugu na mashambulizi ya aina yoyote ile yanalifedhehesha Taifa kwa kuwa matendo hayo ni dhambi, uhalifu na si utamaduni wa Mtanzania, hivyo vyombo vinavyohusika havina budi kuyakomesha mara moja.