Msaada wa Magari na Bilioni 110 alizokabidhiwa Rais JPM Ikulu leo
Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem
Ibrahim Al Najem na kushukuru kwa kutoa mkopo wa Tsh. Bilioni 110 za
ujenzi wa barabara KM 85 Chaya - Nyahua, Tabora.
Rais Magufuli ametoa shukrani na kupokea msaada wa magari mawili ya kubebea taka ngumu yenye thamani ya Dola 200,000/- yaliyotolewa na Serikali ya Kuwait.
Rais Magufuli ametoa shukrani na kupokea msaada wa magari mawili ya kubebea taka ngumu yenye thamani ya Dola 200,000/- yaliyotolewa na Serikali ya Kuwait.
“Tunaotaka kuwa Viongozi bora tunajaribu kujinasibisha na Nyerere” – Mak...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January
Makamba amesema Kongamano la Mazingira lililofanyika Butiama ni kwa
sababu Mwalimu Nyerere ni mfano wa kuigwa ambaye kila mmoja anatamani
kumuiga katika yale aliyoyafanya
Christina Shusho kuhusu vazi la Jeans...ni sahihi kwa waliookoka?
Moja ya story kubwa ambayo inaendelea kuwa gumzo na ku-make headlines
kwa kuibua mijadala sehemu mbali ni kuhusu mavazi ya jeans kwa
waliookoka ambapo licha ya elimu kutolewa limeonekana kuwa gumu kwa
baadhi ya watu.
Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Mwimbaji staa wa Injili Tanzania, Christina Shusho ambaye anaeleza kama ni sahihi au sio sahihi kwa waliookoka kuvaa vazi la Jeans.
Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Mwimbaji staa wa Injili Tanzania, Christina Shusho ambaye anaeleza kama ni sahihi au sio sahihi kwa waliookoka kuvaa vazi la Jeans.
Mdee, Bulaya wafungiwa mwaka mmoja kwa kumdharau Spika
Bunge limepitisha azimio la Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
ikiwa ni pamoja na kupitisha hoja ya kubadilisha azimio hilo
lililotolewa na Mbunge wa Vitimaalum Juliana Shonza azimio lililowataka
wabunge Ester Bulaya na Halima Mdee kutohudhuria vikao vyote vya Bunge
vilivyobaki vya mkutano wa saba wa bunge la bajeti, Mkutano wote wa nane
wa bunge na mkutano wote wa tisa wa bunge
"Unaweza kuzaliwa Masikini lakini kufa Masikini ni kujitakia" – Mavunde
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na
Walemavu Anthony Mavunde ametoa wito kwa vijana wa kitanzania kuwa
wabunifu bila kujali ni wakati gani na changamoto zipi wanazipitia na
wasikubali kukatishwa tamaa ili kujiwekea mikakati ya kufikia malengo
yao.
Alichokisema Mama Samia kwenye Kongamano la Mazingira Butiama
Makamu wa Rais Samia Suluhu akiwa kwenye Kongamano la Mazingira amewaasa
Watanzania kutumia wajibu wao kukumbushana umuhimu wa kuyatunza na
kuhifadhi Mazingira kwa manufaa na mustakabali wa maisha ya kila siku…
HEKAHEKA: Mama adaiwa kumchapa mwanae hadi kufa...kisa?
June
5, 2017 kwenye Leo Tena ya Clouds FM mtangazaji Geah Habib ametusogezea
Hekaheka ambayo inamuhusu mwanamke mmoja ambaye anashikiliwa na Polisi
akidaiwa kumpiga mtoto wake wa kumzaa hadi kufa baada ya kumshutumu
kuiba hela ya ndani.
Ndugu Wasisitiza Hawatamzika Ndugu Yao Aliyepigwa Risasi na Polisi Mpaka...
Familia ya Salum Almasi, Imamu wa msikiti wa Al-Kheri uliopo Kurasini
jijini Dar es Salaam, aliyepigwa risasi na polisi na kuuawa huku polisi
wakiendelea kushikilia msimamo kwamba alikuwa jambazi, wametoa tamko
kali kwa jeshi la polisi kuhusu mazingira ya kutatanisha ya kifo cha
ndugu yao.
Kivuko kipya cha MV Kazi chapokelewa leo, kina uwezo wa kubeba watu 800
Kivuko hicho kitakachofanya safari kati ya Feri na Kigamboni ujenzi wake
umegharimu Sh7.3 trilioni na kina uwezo wa kubeba watu 800 na magari 22
kwa wakati mmoja
Gwajima Amvua nguo Bashite hadharani. Aliyosema hajawahi kuyasema
Askofu Gwajima amvua nguo Bashite hadharani. Aliyosema hajawahi
kuyasema. Atoa hukumu kwamba amemfuta kwenye Ulimwenye wa Siasa na
Madaraka kwa ujumla mpaka atakapoomba msamah
Msiba: Balozi Cisco Mtiro Afariki Dunia
Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro amefariki dunia katika
Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa
matibabu.
Cisco Mtiro alikuwa Balozi wa Tanzania nchi za Malaysia, Phillipines, Cambodia, Singapore na Laos.
Kwa mujibu wa familia yake, msiba upo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B jijini Dar es salaam ambapo aratibu za mazishi zinaendelea na taarifa zitatolewa mara tu zitapokamilika.
Cisco Mtiro alikuwa Balozi wa Tanzania nchi za Malaysia, Phillipines, Cambodia, Singapore na Laos.
Kwa mujibu wa familia yake, msiba upo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B jijini Dar es salaam ambapo aratibu za mazishi zinaendelea na taarifa zitatolewa mara tu zitapokamilika.
Subscribe to:
Posts (Atom)