Msiba: Balozi Cisco Mtiro Afariki Dunia

Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Cisco Mtiro alikuwa Balozi wa Tanzania nchi za Malaysia, Phillipines, Cambodia, Singapore na Laos.

Kwa mujibu wa familia yake, msiba upo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B jijini Dar es salaam ambapo aratibu za mazishi zinaendelea na taarifa zitatolewa mara tu zitapokamilika.

No comments: