KICHUYA AANZA MAZOEZI BAADA YA KUPATA MAJERAHA




Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Shiza Ramadhan Kichuya, ameanza mazoezi na timu yake baada ya kupata nafuu ya majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata wakati wa mchezo wa mzunguuko wane wa ligi kuu juma lililopita dhidi ya Mbao FC.
Mchezaji huyo aliumia katika dakika ya 44 ya mchezo huo, uliomalizika kwa sare ya mabao mawili kw amawili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Kichuya alifunga bao la kwanza dhidi ya Mbao dakika ya 16 kwa kichwa lakini hata hivyo alishindwa kumaliza kipindi cha kwanza baada ya kupata majeraha kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima.
Kufuatia hali hiyo Kichuya, alikosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Milambo FC, juzi kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, timu hizo zikitoka sare ya 0-0.

CHIRWA AKABIDHIWA MAJUKUMU YA TAMBWE




Kocha Mkuu wa klabu bingwa Tanzania bara Young Aficans, George Lwandamina, amemkabidhi Obrey Chirwa majukumu ya Amissi Tambwe ambaye kwa sasa ni majeruhi.
Chirwa amepewa majukumu hayo kutokana na Tambwe kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti.
Kutokana na kuuguza majeraha hayo, ilisababisha Tambwe akose michezo mitano za kimashindano ambazo tayari Yanga imecheza ikiwa moja ya Ngao ya Jamii na nne Ligi Kuu Bara.

P-SQOURE YAFUNJA NA PETER KUJIITA MR P






Wasanii maarufu wa Hip-hop, nchini Nigeria Peter na Paul Okoye, wanaounda kundi la Psquare kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya vizuri katika muziki wao nchini humo wamevunja mkataba wa kundi hilo mara baada ya Peter Okoye kumtaka mwanasheria wao Festus, Kuvunja kundi hilo.
Peter amesema kuwa inaonekana kuwa ndugu yake Paul hayupo tayari kuendelea kufanya kazi na yeye kwani ameweza kusitisha ziara yao ya US bila ya kuweka sababu yeyote.
Ameongeza kuwa, Paul amekuwa akimtukana mkewe na watoto wake kupitia mitandao ya kijamii na kusema familia yake imekuwa ikitumiwa ujumbe uliokuwa ukiwatishia maisha

RIHANNA AWATAJA MASTAA ANAOWAKUBALI AMBAO ALITAMANI KUOLEWA NAO






Msanii wa muziki wa Pop nchini Marekani Rihanna Fenty ametoa ya moyoni kuhusu wachezaji wa soka ambao anawazimikia na kuwakubali kwa kile wananchokifanya katika soka.
Rihanna amesema kuwa kama ingekuwa kuolewa na mchezaji wa soka duniani basi angemchagua staa wa zamani wa klabu ya Manchester United na Real Madrid , maarufu kama David Beckham
Pia amesema kwa soka la sasa anamkubali sana Cristian Ronaldo na kumuweka pembeni Lionel Messi.
Msanii huyo amedai kuwa Beckham alimfanya apende soka na angekubali kuolewa na mchezaji huyo lakini aliwahiwa na Poah Spice  mke wa Bechkam, Victoria Beckham.

MARUFUKU VIGODORO RPC MKOA WA TANGA ANENA





Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benedict Michael Wakulyamba, amepiga marufuku Vigodoro ndani ya jiji hilo kutokana na vitendo hivyo kuhamasisha uhalifu
Akiongea ofisini kwake Benedict amesema miongoni mwa viashiria vya uvunjivu wa amani ni Vigodoro, ambavyo vinatumika kukusanya vijana wenye umri mdogo wakijiandaa kufanya uhalifu.
“Miziki ya kigodoro ni miziki ambayo ukiangalia namna inavyochezwa na hata washiriki wake ni vijana ambao wanatumia kama sehemu ya maficho kwaajili ya kufanya uhalifu’’ amesema Benedict.

GODBLESS LEMA APELEKA USHAHIDI TAKUKURU




Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka na kudai atakwenda kumuona Mkurugenzi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini Tanzania (Takukuru), Valentino Mlowola ili aweze kumpa ushahidi wa biashara haramu.
Mhe. Godbless Lema amesema hayo leo kupitia ukurasa wake twitter baada ya kupita siku moja tokea Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole kutoa kauli yake iliyokuwa inawataka viongozi wa upinzani kama kweli wanaushahidi wa madiwani saba kununuliwa ili wahamie CCM basi waweke wazi nasiyo kusema sema katika mitandao ya kijamii.
Tutakwenda kumuona Mkurugenzi wa Takukuru na kumpa ushahidi wa biashara mpya haramu ya madiwani”, amesema Lema.

NDALICHAKO ASITISHA AJIRA KWA WALIMU WA SANAA

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ametoa masharti mapya ya ajira za ualimu nchini, huku akisema Serikali haitaajiri walimu wa masomo ya sanaa (arts) kwa kuwa wapo wa kutosha.

Akizungumza mjini Dodoma jana wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Profesa Ndalichako, alisema Serikali kwa sasa haiwezi kuajiri walimu wa masomo hayo kwa kuwa inataka kuajiri walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ambao idadi yao ni ndogo.

“Pamoja na uamuzi huo mpya, ajira za walimu wapya wa masomo ya sayansi nazo zimebadilika kwani wale wote waliohitimu ualimu wa sayansi na hisabati, wanatakiwa watume vyeti vyao kabla ya kupangiwa kituo cha kazi.

“Kuhusu wale walimu wa ‘arts’, kule tuna walimu wa ziada ambao tutajaribu kuwapanga kutokana na shule, kwani wengi walikuwa wamepangwa shule moja. Kwahiyo, tutaangalia utaratibu wa kuwapanga kulingana na mahitaji,’’ alisema Profesa Ndalichako.

Akizungumzia suala la ubora wa elimu nchini, Profesa Ndalichako aliwataka walimu wakuu hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu kwa kuwa wao ndio wanaowaandaa wanafunzi kabla hawajaenda vyuoni.

“Vilevile pelekeni takwimu sahihi za wanafunzi waliopo katika shule zenu kuisaidia Serikali katika kupanga bajeti ili iweze kutoa fedha sahihi.

“Hapa kuna kimbembe, yaani wakati mwingine huwa najifanya nimepoteza takwimu ya shule fulani, nikiziomba na kutumiwa, zinakuwa ni tofauti na zile za mwanzo.

“Hili nawaomba mkalisimamie ili iwe rahisi kwetu kupanga bajeti yenye tija,’’ alisema.

Kuhusu ujenzi wa maabara katika shule za sekondari, waziri huyo alisema kwamba kutokana na nyingi kukamilika, Serikali itatoa vifaa vya maabara kuanzia Januari mwakani baada ya kuwa vimeingia nchini kutoka vilikoagizwa.

Awali, akisoma risala ya walimu hao, Rais wa TAHOSSA, Bonus Nyimbo, aliiomba Serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi shuleni kwa kuwa zimekuwa zikichangia kushuka kwa ufaulu kwa baadhi ya wanafunzi.

“Ili kuboresha elimu, tunaiomba Serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi kwani simu nyingi tunazozikamata tunakuta mule hakuna taaluma,’’ alisema Nyimbo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Molel, ambaye pia kampuni yake ilipewa tuzo ya heshima katika kuendeleza elimu nchini, alisema ni jukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake ili kuiendeleza elimu ya Tanzania.

“Kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu, wazazi, walezi na walimu, waambieni wanafunzi wasiwe na ‘expectation’ (matarajio) makubwa kwani wanapokuwa na matarajio hayo, wakienda vyuo vikuu wanakuwa wasumbufu,” alisema.

Wakati hayo yakiendelea, juzi taarifa ilitolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi, ikisema kwamba, walimu wahitimu wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu shahada na astashahada mwaka 2015, wanatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti vya elimu ya sekondari vya kidato cha nne na sita na taaluma ya ualimu kwa uhakiki

WAFANYABIASHARA SOKO LA MCHIKICHINI WAPEWA ELIMU JUU YA UKATILI WA KIJINSIA


Mwezeshaji wa kisheria kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), Amina Mussa akitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia kwa wafanyabiashara wa Soko la Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo. 
Mfanyabiashara Shikei Ngosi, akielezea changamoto zinazotokana na ukatili wa kijinsia katika soko hilo.
Mwezeshaji Khadija Mohamed akitoa elimu ya upingaji wa ukatili wa kijinsia.
Mfanyabiashara, Mussa Ibrahim, akichangia jambo.
Juma Mohamed akichangia jambo.
Mfanyabiashara wa nguo katika soko hilo, Godrey Milonge akielezea changamoto za ukati wa kijinsia katika soko hilo.
Mwezeshaji wa Sheria kutoka Soko la Temeke Stereo, Batuli Mkumbukwa akichangia jambo.
Mwezeshaji Sheria,wa Soko la Kigogo Kisambusa, Mariam Rashid akitoa mafunzo
Mwezeshaji wa Sheria katika Soko la Ilala Mchikichini, Consolata Cleophas akitoa elimu hiyo.
Mfanyabiashara, Johnson Stephano akisoma moja ya kijarida kinachoelezea ukatili huo.
Mafunzo yakiendelea.
Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Suzan Sitha, akiwaeleza jambo wafanyabiashara wa soko hilo kuhusu kukomesha ukatili wa jinsia.



Na Dotto Mwaibale

WAFANYABIASHARA katika Soko la Ilala Mchikichini wamepatiwa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia masokoni .

Katika hatua nyingine wafanyabiashara wanaume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na wanawake wametakiwa kwenda kushitaki ofisi za masoko husika ili sheria ichukue mkondo wake kwa wahusika waweze kujirekebisha.

Mwito huo umetolewa na Mwezeshaji wa Sheria masokoni, Khadija Mohamed kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG) wakati wanasheria wa shirika hilo wakitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wafanyabiashara wa Soko la Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo hii.

"Wakina baba mnapofanyiwa vitendo vya kijinsia na wanawake katika masoko msione haya nendeni kushitaki kwa viongozi wa masoko ili watuhumiwa waweze kukamatwa na kujirekebisha" alisema Mohamed.

Mohamed alisema vitendo vya ukatili wa jinsia hawafanyiwi wanawake pekee bali hata wanaume wamekuwa wakifanyiwa lakini wanaona aibu kwenda kushitaki.Mwezeshaji wa Sheria Batuli Mkumbukwa alisema vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo vimeshamiri hivyo alitoa mwito kwa wafanyabiashara wa soko hilo kuviacha. 

Mkumbukwa alisema ili kumaliza vitendo hivyo kwa makosa madogo madogo kama kutoa lugha ya matusi, kumshika mtu maunoni bila ya ridhaa yake mtuhumiwa amekuwa akipewa adhabu pamoja na kupigwa faini lakini kwa kosa la ubakaji adhabu yake ni kifungo cha maisha au miaka 30.

Mariam Rashid, ambaye ni mwezeshaji wa kisheria kutoka EfG alitaja ukatili wa kijinsia unaofanyika katika masoko ni ukatili wa kingono, uchumi, kisaikolojia na kimwili.Baadhi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinafanyika katika soko hilo ni pamoja na wafanyabiashara kuwashika sehemu za siri wateja wao wa kike maarufu kama kunawa, kukojoa kwenye chupa za maji na kwenda kuziweka kwenye meza za 

wafanyabiashara, lugha za matusi, kujambisha na kutolipa fedha baada ya kuuziwa chakula na mama lishe.Wafanyabiashara katika soko hilo walisema kuwa kukithiri kwa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo kwa namna moja au nyingine vinachangiwa na wanawake wenyewe kutokana na tamaa zao kwa kuvaa nguo fupi na kujilengesha kwa wanaume ili wapate bure bidhaa wanazozitaka.

"Wanawake wanabakwa na kushikwa maungoni kwa kupenda wenyewe wala hawalazimishwi" alisema Juma Mohamed mfanyabiashara.

Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Susan Sitta alisema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwaongezea uelewa wafanyabiashara ili waweze kuacha kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika masoko ili kutoa fursa kwao kufanya biashara zao bila ya kuwa na bugudha.

Alisema mradi huo umefadhiliwa na Shirika la United Nations Trust Fund na kuwa unafanyika katika masoko ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Temeke.

NEW:MWENYEKITI WA CCM AMBAYE PIA NI RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA

RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu,wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alli Mohamed Shein,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Ndg. Phili Mangula akikaribishwa ukumbini katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe  Magufuli akiwasili ukumbini kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini  Dar es Salaam. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na nyuma ya Makamu  wa Rais ni Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza wa Wakilishi la Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar ss Salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Rodrick Mpogolo kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.