MSIKILIZE ROMA MKATOLIKI NA SIMULIZI YA KUTEKWA


Rapa staa Roma Mkatoliki ambaye ali-make headlines kwenye mitandao mbalimbali baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana na kushikiliwa kwa siku kadhaa amesema bado hajakaa sawa tangu tukio hilo ingawa analazimika kufanya kazi ili apate riziki.
Akizungumza kwenye XXL ya Clouds FM May 17, 2017 Roma amesema waliathirika zaidi baada ya vifaa kuchukuliwa kwenye Studio za Tongwe Records huku yeye akipoteza album nzima na kushindwa kurejea kwenye muziki kwa sasa kwa sababu muziki ni hisia, hivyo anatakiwa kutuliza akili kwanza kabla hajaandika wimbo.
“Hatuko poa sana, lakini lazima tutoke tufanye kazi. Tulipata madhara makubwa kwenye Studio yetu Tongwe Records, baada ya kuchukuliwa vifaa vyetu. Nimepoteza album nzima na muziki ni hisia. Hivyo mpaka nitulie ndio nitaandika ngoma nyingine. Kwa sasa naomba msupport zilizopo. Mdogo wangu Moni Centrozone ana ngoma kali ametoa, inaitwa Tunaishi nao

No comments: