HAWA NDIO WANAWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI YA VODACOM


Shirikisho la Soka Tanzania TFF leo May 17 2017 kupitia tovuti rasmi ya shirikisho hilo imetangaza majina matano ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 na watapigiwa kura hadi May 23 saa 6:00 usiku.
Majina ya wachezaji watano yaliyotajwa na shirikisho la soka Tanzania TFF ni Haruna Niyonzima wa Yanga, Simon Msuva wa Yanga, Aishi Manula wa Azam FC, Shiza Kichuya wa Simba na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba.
Utoaji wa tuzo hizo utafanyika May 25 2017 lakini mshindi wa tuzo hiyo atapatikana kwa kupigiwa kura na makocha wakuu na wasaidizi wa vilabu vya Ligi Kuu Tanzania bara pamoja na wahariri wa habari za michezo ambapo watatumiwa fomu maalum za kupiga kura

No comments: